Sarafu mpya ya Tsh. 500/= inayotumika sasa
Baada ya kuonekana noti ya shilingi 500 ina mzunguko mkubwa wa
matumizi na inachakaa kwa haraka huku kiwango chake cha kuhimili
mizunguko ni miezi sita, Benki kuu ya Tanzania (BOT) imekubadili
kubadili noti hiyo na kuifanya sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 imesha anza kutumika ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha ambapo inaarifiwa sarafu hii inatarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya
miaka 20 na kubaki na ubora wake uleule, yani ni imara kuliko noti.
Noti ya 500 iliyokua ikitumika awali
Afisa mkuu wa benki kitengo cha idara kurugenzi za kibenki Patrick Fata amesema “Tunafanya hivi kwasababu noti ya
500 inachakaa haraka kulinganisha na mzunguko wake na kuwafikia watu
wengi pia huchakaa haraka kutokana na mzunguko wa kushikwa na watu
wanaofikia mpaka milioni moja kwa siku, hiyo ni idadi kubwa kuliko ya
wanaoshika noti ya elfu 10 kwa siku’

No comments:
Post a Comment