Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ akiwa na Garder.Stori: Gladness Mallya
Funguka! Kwa
mara ya kwanza, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo
‘Jide’ ameanika kisa cha kummwaga mumewe, Gardner Gabriel Habash
‘Kaptein’ akieleza mateso aliyokutana nayo kwenye ndoa yao
.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ akipozi.
Akizungumza
na Kituo cha Radio Times FM cha jijini Dar, wikiendi iliyopita, Jide
alifunguka kuwa yeye ndiye aliyeamua kummwaga Gardner.
Katika
mahojiano hayo, Jide alisema kwamba alikuwa kwenye uhusiano na mtu
aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa
ni Gardner lakini alisema alikuwa akiteswa (hakuna mwanaume mwingine
zaidi ya Gardner)
About
Contact
More
Menu
December 1, 201422:45:15
twitter
facebook
google
rss
linkedin
dribbble
pinterest
SHEBBY D BLOG
NI BLOG INAYOJIUSISHA NA JAMII YOTE KWA UJUMLA
Home
KITAIFA
KIMATAIFA
SIASA
ENTERTAINMENT
AUDIO
VIDEO
KISURA
SOKA
facebook
contact
Hisia za Mwananchi
Home » KITAIFA » SIASA » Escrow yazamisha watatu Urais 2015
Escrow yazamisha watatu Urais 2015
12/01/2014 10:12:00 AM Shaban R Dege 0 KITAIFA, SIASA
KASHFA ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta
Escrow, imewachafua viongozi watatu ambao walishaanza harakati za
kuusaka urais kwa mwaka 2015.
Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mbunge wa
Sengerema, William Ngeleja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Kwa upande wa Pinda, ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC) iliyowasilishwa bungeni, ilionyesha kiongozi huyo wa shughuli za
Serikali bungeni alilidanganya Bunge kwa matamshi yake.
Mara kadhaa Pinda alisikika akiueleza umma kuwa fedha hizo hazikuwa za
umma bali mali ya Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya IPTL.
Katika maazimio ya PAC, Pinda alitakiwa pia kuwajibika kutokana na
kushindwa kusimamia Serikali kwani katika hatua zote za kutolewa kwa
fedha hizo, alikuwa akijulishwa.
Pinda ambaye alitangaza kuanza harakati za urais kimya kimya, akiwa
jijini London, Uingereza alipohojiwa na Kituo cha Televisheni cha BBC,
alijikuta kwenye wakati mgumu pale Bunge lilipopitisha azimio la
kumpeleka kwa mamlaka ya uteuzi kabla baadae jina lake kuondolewa.
Hali hiyo ilijitokeza pale Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alipolishauri
Bunge kupeleka majina ya watu wote waliotakiwa kuchukuliwa hatua kwa
mamlaka zao za uteuzi ili hatua zaidi zichukuliwe.
Baada ya kauli hiyo ya Zitto, Spika wa Bunge Anne Makinda alilihoji
Bunge na kwa sauti moja likakubali kabla ya Mbunge wa Simanjiro, Ole
Sendeka kusimama na kuomba mwongozo wa Spika ambaye baadaye alitengua
uamuzi wake.
Akizungumza na Mtanzania, Zitto alisema jina la Pinda kupelekwa kwa rais
ingetosha kuonyesha Bunge halina imani naye, hivyo mamlaka yake hiyo ya
uteuzi ingebidi itengue nafasi ya kiongozi huyo wa shughuli za Serikali
bungeni.
Alisema pia kamati yake ilikubali kuondoa jina la Pinda kwenye orodha ya
vigogo waliopaswa kushughulikiwa baada ya mazungumzo kati ya wabunge wa
upinzani na wale wa CCM.
Kutokana na hali hiyo, Pinda ambaye anajulikana zaidi kama ‘mtoto wa
mkulima’, harakati zake za kwenda Ikulu zimetiwa doa kwani mwanzo
alihesabika kuwa ni kati ya wagombea wasio na kashfa.
Kwa upande wake, Ngeleja ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na
Madini, anadaiwa kupewa Sh milioni 40.4 kutoka kwenye akaunti ya Escrow
huku Profesa Tibaijuka ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, akidaiwa kupewa Sh bilioni 1.6.
Viongozi wote hao wawili ambao hawajawahi kutangaza rasmi kuwania urais
mbali na majina yao kutajwa kwenye orodha hiyo, Bunge limeazimia
wachukuliwe hatua.
Kwa upande wa Profesa Tibaijuka, rais ametakiwa kumvua wadhifa wa
uwaziri huku Ngeleja ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Katiba, Sheria na Utawala, spika akishauriwa kumchukulia hatua ya kumvua
wadhifa huo.
Akichangia bungeni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu,
Steven Wasira, aliwataka wote wanaotumia suala la ripoti ya PAC kwa
vigezo vya kuwaondoa wenzao katika mbio za urais hawastahili kupewa
nafasi hiyo.
“Wanaotaka urais kama wapo ni pamoja na mimi, ambao wanaona mbinu ni
kuwaondoa wengine kwa nguvu, hao hawafai kupewa urais wa nchi hii. Urais
ni lazima ushindaniwe kwa haki na vyama vyote vipewe nafasi ya
kushiriki. Kama unataka urais ushindani uwe kwa njia sahihi,” alisema.
Alisema ni bora kuwa maskini anayeheshimika kuliko kukubali kuwa tajiri
anayedharauliwa na kutukanwa kutokana na mapato yasiyokuwa halali.
Wasira alieleza kwa kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) imesema baadhi ya watu walikwenda kuchukua fedha wakiwa na
magunia, mifuko ya sandarusi, rumbesa na maboksi katika moja ya benki,
ni vyema uchunguzi ukifanyika ili kuwatambua watu hao na hatua zaidi
zichukuliwe.
“Ni lazima tufuatilie na vyombo vyetu vya sheria vituambie ni kina nani
hao, vinginevyo hatuna nchi. Tukubali hawa watu wabebe mizigo yao,
hakuna CCM ya wezi, ila kuna wezi ndani ya CCM, hivyo wezi ni lazima
wabebe mizigo yao,” alisema.
Alisisitiza kwamba ripoti hiyo ya PAC inatakiwa kuheshimiwa na kwamba
hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuihoji uhalali wake kwa kuwa inatokana na
kamati maalumu inayotambuliwa na Bunge iliyokusanya taarifa kutoka kwa
vyombo vinavyoaminika vya Serikali, ambavyo ni Takukuru na CAG.
Credit:Mtanzania
Share to:
Next
This is the most recent post.
Previous
Kama hujasoma Magazeti ya Leo Desemba 01 nimekuwekea hapa zile story
kubwa zote.
Related Posts
Kama hujasoma Magazeti ya Leo Desemba 01 nimekuwekea hapa zile story
kubwa zote.Kama hujasoma Magazeti ya Leo Desemba 01 nimekuwekea hapa
zile story kubwa zote.Dec 01, 2014
Taarifa rasmi kutoka Ikulu kuhusu mabadiliko kwenye nafasi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, CAGTaarifa rasmi kutoka Ikulu
kuhusu mabadiliko kwenye nafasi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali,
CAGDec 01, 2014
Askari wa JKT akutwa mferejini akiwa kalewa chakari .....Pombe
Ilipozidi alianza kujisaidia ndani ya basiAskari wa JKT akutwa mferejini
akiwa kalewa chakari .....Pombe Ilipozidi alianza kujisaidia ndani ya
basiDec 01, 2014
Watendaji 17 Waswekwa Rumande kwa Kushindwa Kusimamia Agizo la Rais
Kikwete kuhusu Ujenzi wa MaabaraWatendaji 17 Waswekwa Rumande kwa
Kushindwa Kusimamia Agizo la Rais Kikwete kuhusu Ujenzi wa MaabaraNov
27, 2014
Baada ya Ishu ya Escrow, haya ni Majibu Mawili ya Waziri Mkuu Pinda
ikiwemo KujiuzuluBaada ya Ishu ya Escrow, haya ni Majibu Mawili ya
Waziri Mkuu Pinda ikiwemo KujiuzuluNov 27, 2014
#Exclusive Staa mwingine wa Tanzania alietangaza kugombea Ubunge
2015.#Exclusive Staa mwingine wa Tanzania alietangaza kugombea Ubunge
2015.Nov 19, 2014
Kinana na Dr. Slaa kesho watashiriki katika Mjadala wa Rais wa
Tanzania anayetakiwa 2015Kinana na Dr. Slaa kesho watashiriki katika
Mjadala wa Rais wa Tanzania anayetakiwa 2015Nov 11, 2014
Rais Kikwete Aomba Yasimkute ya Jaji Warioba.....Polisi watoa tamko,
CUF Waapa kulinda midahalo ya Jaji Warioba!Rais Kikwete Aomba Yasimkute
ya Jaji Warioba.....Polisi watoa tamko, CUF Waapa kulinda midahalo ya
Jaji Warioba!Nov 04, 2014
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment
Emoticon
Live streaming video by Ustream
Blog Rafiki
JOHVENTURE MUSIC
Official Video | Ommy Dimpoz -Tupogo Remix | Download -
3 days ago
Total Pageviews
349874
Populars
Comments
Archive
widgeo.net
widgets
SHEBBY D BLOG © 2013. All Rights Reserved.
Share on Hisia za Mwananchi. Powered by Hisia
Top
SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA
X
FacebookTwitterEmailPrintGmailStumbleUponFavoritesMore... (294)
Sign In
AddThisPrivacy
Make Money at : http://bit.ly/copy_win
Make Money at : http://bit.ly/copy_win
No comments:
Post a Comment