Asema Sakata la Escrow Lawafanya Wazomewa Kila Kona
Jana Katika mkutano wa hadhara mjini Babati wakati akihutubia umati wa watu wachache waliojitokeza, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ndugu Musukuma ambae ameambatana naibu katibu mkuu wa CCM bara mh Mwigulu.
Nikimnukuu.
."Hatuwezi kutembea tangu asubuhi hadi jioni tukizomewa kama watoto kwa ajili ya watu wachache, ni lazima serikali ichukuwe hatua kwa suala hili la Escrow"
Naye Mwigulu akihutubia Amesema serikali itawachukulia hatua watumishi wote watakaobainika kukiuka maadili katika halmashauri zote nchini bila kusita.
Kauli ya Ndg Musukuma mwenyekiti CCM mkoa wa Geita inaashiria kwamba wamekumbana na hali ambayo hawakutarajia na ameonyesha kumtumia ujumbe mwenyekiti wao taifa ili achukuwe hatua madhubuti kwani hali huko site sio shwari tena.
No comments:
Post a Comment