Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
15 December, 2014
MATOKEO YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2014
UCHAGUZI wa serikali za mitaa uliofanyika jana nchini kote ambapo chama tawala CCM, kimepata upinzani mkubwa dhidi ya vyama vya upinzani katika kujenga nguvu kwa ajili ya kushinda uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Ushindani mkubwa kabisa upo baina ya CCM na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi, (UKAWA), vya Chadema, CUF na NCCR - Mageuzi.
Mwandishi wa habari hizi aliyetembelea baadhi ya vituo vya kupigia kura aliona misururu mirefu ya wananchi wakiwa katika hatua za kupiga kura.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wanasema wamejitokeza kupiga kura ili kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika sekta mbalimbali.
Maeneo mengi nchini kumeripotiwa kufanyika uchaguzi katika hali ya amani na utulivu isipokuwa katika maeneo machache jijini Dar es Salaam ambapo kumetokea vurugu kutokana na mambo mbalimbali.
Katika Kata ya Kijitonyama katika kituo cha kupigia kura cha Kalimaua ‘A’, mgombea wa CCM amekamatwa na polisi baada ya kuiba masanduku ya kura na kutaka kuyatupa baada ya kuona mambo sio mazuri kwake.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa nchi ambao utafanyika Oktoba mwakani.
Kijiji cha Muungano Kata ya Chahwa mkoani Dodoma: CHADEMA 196, ADC 38
Mbozi; Mtaa wa Masaki: CHADEMA 99, CCM 44
Kigoma Mjini; Mtaa wa Gezaulole: CHADEMA 240, CCM 198
Ukonga; Mtaa wa Kivule Majohe: CHADEMA 231, CCM 77
Musoma Vijijini; Kijiji cha Muhoji: CHADEMA 197, CCM 464
Ubungo; Mtaa wa Msewe: CHADEMA 683, CCM 356
Kinondoni; Mwenge Nzasa: CHADEMA 344, CCM 318
Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35
Mererani: CHADEMA imeshinda mitaa 7 kati ya 8
Kitongoji cha Endulele: CHADEMA 170, CCM 130
Monduli; Kitongoji Kambi ya Mkaa: CHADEMA 27, CCM 13
Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35
Arumeru Magharibi, Kitongoji Endulele: CHADEMA 170, CCM 130
Ushirombo Mjini: CHADEMA inaongoza vitongoji 10, CCM inaongoza vitongoji 4
Moshi Manispaa, Kitongoji Longuo A: CHADEMA 206, CCM 66
Mbozi Mtaa wa Mbugani: CHADEMA 227, CCM 160
Kata ya Mji Mpya, Morogoro yenye mitaa 12, CCM imeshinda mitaa 9, CHADEMA wakishinda mtaa 1 huku mitaa miwili vurugu zilitanda baada ya kura kudaiwa kuzidi huku watu kadhaa wakituhumiwa kupiga kura mara mbili.
Kagondo, Kata ya Muhutwe, Kagera: CHADEMA imeshinda mitaa 4 kati ya 5
NAKUPENDA TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Josephine is passionate, dedicated, reliable, responsible, and hardworking. Team worker and able to face all challenging situations. Can ...
No comments:
Post a Comment