Johnson Lukaza
HATIMAYE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachilia huru
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesiga
Lukaza waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh.Bilioni Sita Katika
Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu(EPA), baada ya kumuona Hana hatia
Katika Kesi iliyokuwa ikimkabili.
Hukumu hiyo Imetolewa Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu Mkazi Pamela Mazengo.
Lukaza
ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) alikuwa
akitetewa na Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana
na Wakili Alex Mshumbusi.
Akisoma
hukumu hiyo Jaji Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama
imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili Na kupitia vielelezo
mbalimbali, Mahakama yake Imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru
washitakiwa wote Wawili kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta
ushahidi thabiti ambao ungeishawishi Mahakama hiyo iwakute na hatia
washitakiwa Hao.
No comments:
Post a Comment