– Je ni kweli UKIMWI husababishwa na Virusi Vya Ukimwi (V.V.U)?
– Je ni kweli UKIMWI ni ugonjwa wa kuambukizana?
– Je ni kweli watu wanapona UKIMWI?
‘’Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwakuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, Mimi nami nitawasahau watoto wako – Hosea 4: 6’’.
Ukweli Kuhusu UKIMWI ni maelezo yanayoipinga dhana inayosema ugonjwa wa UKIMWI husababishwa na Virusi Vya Ukimwi (V.V.U) kupitia maandiko kadhaa ambayo yameshaandikwa na wanasayansi wengine duniani.
Maelezo haya yanatolewa kama elimu tu kwa umma na si lengo la mwandishi kumuondoa daktari wako au chaguo lako la matibabu unayopendelea, matumizi ya taarifa zilizomo humu yanabaki kuwa jukumu la msomaji, mwandishi wa makala hii hatoi dhamana yeyote juu ya yale yawezayo kutokea katika afya yako kutokana na taarifa au ujuzi utakaoupata toka hapa, badala yake ubadilishanaji wa taarifa na maarifa yaliyomo humu na daktari au jamaa zako wengine unahimizwa sana kwa ustawi wa dunia yetu
UKIMWI ni nini?
Neno UKIMWI ni kifupi cha maneno: Upungufu wa Kinga Mwilini. Tumeambiwa ni ugonjwa unaotokana na virusi vya UKIMWI (V.V.U) au Human Immunodeficiency Virus (H.I.V) kwa lugha ya kikoloni.
Tumefundishwa kuwa virusi hao wakiingia katika damu ya binadamu huenda kuishi katikati ya seli na kuzidhuru chembe chembe hai nyeupe za damu ambazo ndizo huhusika na kinga ya mwili na hivyo kumuweka mhusika katika hali ya kupatwa na magonjwa mengi nyemelezi zaidi ya 30 na kuwa hadi sasa hakuna dawa inayoweza kutibu virusi hivyo au kwa maneno mengine UKIMWI hauna dawa!
Tumefundishwa kuwa virusi vya UKIMWI vinaweza kuambukizwa toka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa sehemu KUBWA kupitia tendo la ndoa ambapo damu ya aliyeathirika na virusi hivi ikikutana na ambaye hajaathirika wakati huo wa tendo la ndoa basi virusi navyo humwingia mtu huyo, njia nyingine ni kwa kushirikiana vifaa vyenye ncha kali kama vile nyembe, sindano, mikasi na kadharika, nyingine ni mama mjamzito kumwambukiza mwanaye wakati wa kujifungua au anaponyonyesha, mgonjwa aliyechangiwa damu yenye virusi na kadharika.
Tangu kuanza kutangazwa kwa ugonjwa huu mwanzoni mwa miaka ya 1980 maelfu ya watu wamekufa duniani kote huku mamilioni wengine wakisemwa wanaendelea kuishi kwa matumaini wakitumia dawa za kupunguza makali kundi la ARV’s.
Hivyo ndivyo tulivyofundishwa na kuaminishwa kuhusu UKIMWI.
Je ni kweli UKIMWI husababishwa na virusi vya UKIMWI?
Ingawa kwa miaka mingi tumefundishwa kuwa UKIMWI husababishwa na virusi vya ukimwi (v.v.u) ukweli ni kuwa jambo hilo si la kweli na hapa chini tutaona sababu 10 za kisayansi zinazoeleza kwanini virusi vya ukimwi/HIV vilivyo havina uwezo wa kusababisha ukimwi mwilini au hata ugonjwa mwingine wowote.
SABABU 10 ZA KISAYANSI KWANINI HIV/VVU HAVIWEZI KUSABABISHA UKIMWI/AIDS:
“Kile kila mtu anajua na kukiamini” wakati mwingine kinaweza kuwa si cha kweli. Yanapokuja masuala yanayohusiana na sayansi, ikiwa ni pamoja na sayansi ya matibabu, historia inaweza hata kupendekeza kwamba kile kila mtu anajua wakati wowote kinaweza kugeuka baadaye na kuwa siyo sahihi kwa kiwango fulani: ufahamu wa kisayansi umeongezeka, na pamoja na kuendelea huko kwa sayansi, mara nyingi maendeleo hayo yametokea kwa kupindua nadharia zilizotangulia.
Lakini pamoja na kutambua kuwa sayansi imezidi kupaa, huku kila mmoja akiamini hivyo, mara nyingi watu wamesahau kwamba maendeleo hayo yametokana na kukanusha au kupindua nadharia zilizokubalika kabla za kisayansi. Na dhana kwamba nadharia iliyotangulia yaweza kuwa si sahihi, inaweza kuchelewa sana kukubaliwa na watu wengi.
Hivyo madai kwamba Virusi Vya Ukimwi (VVU/HIV) havina uwezo wa kusababisha UKIMWI mwilini, wakati kila mtu anajua kwamba virusi hao husababisha UKimwi, yanachukuliwa na vyombo vya habari, umma, na sayansi tawala kama si vitu vya kuvitilia mkazo. Hata hivyo ushahidi kwamba HIV haiwezi kuwa sababu ya UKIMWI umejitokeza katika maandiko ya kisayansi, na katika dazani kadhaa za vitabu, tovuti na video zikielekezwa kwa sehemu kubwa moja kwa moja kwa umma.
Ni vema kutozingatia kutoa tu ushuhuda kwamba V.V.U havisababishi UKIMWI, bali mhimu iwe kutoa maelezo mhimu na ya kweli mbadala ya kutosha kufafanua UKIMWI (AIDS) ni nini na VVU (HIV) ni nini.
Hivyo majibu ya aya hiyo hapo juu yanatakiwa kuonesha kwanini nadharia inayosema VVU (HIV) = UKIMWI (AIDS) ilivyo si sahihi.
1. VVU/HIV huvunjwavunjwa na kinga ya mwili (antibody immunity):
Wakati mtu amepimwa na kukutwa positive (+) kwa V.V.U, humaanisha mtu huyo anayokinga dhidi ya V.V.U (yaani anao uwezo binafsi wa kuviangamiza virusi, anayo kinga). Hili ni wazi kutokana na ukweli kwamba ni virusi wachache huweza kupatikana katika mwili wa aliyekutwa na kinga positive (+) kwa VVU/HIV *, Kinga ya mwili imefanya kazi yake na virusi wanawekwa vizuri chini ya ulizi na kutafunwa. Hakuna na hakujawahi kutokea virusi wanaojulikana ambao wamewahi kusababisha ugonjwa kwa mtu huku kinga ya mwili ikijitokeza kwa muda mrefu, Bali hivi ndivyo UKIMWI ulivyotafsiriwa!.
Mtu anaweza kujiuliza kwanini zaidi ya miongo mitatu sasa, mabilioni ya fedha yameelekezwa kutafiti chanjo dhidi ya V.V.U wakati chanjo bora tayari ipo wakati mtu anapopima na kukutwa positive (+)?.
2. VVU/HIV huwa haviiui T-Seli yake inayoiambukiza:
V.V.U/H.I.V vinaweza tu kuiua T-Seli yake kwa nadra sana katika majaribio ya kimaabara. Kusema ukweli, watafiti wa V.V.U Hutumia T-Seli ili kukuza virusi sababu T-Seli huishi katika mfanano na V.V.U.
3. V.V.U/H.I.V havina uwezo wa kuzidhuru T-Seli vya kutosha na kusababisha UKIMWI:
V.V.U kamwe hazidhuru T-Seli zaidi ya 1 kati ya T-Seli 1000. Kwa kawaida V.V.U huweza kudhuru T-Seli 1 tu kati ya T-Seli 10,000*, Mwili huzarisha asilimia 5% ya T-Seli zake kwa siku. Hesabu rahisi inaonyesha kuwa V.V.U hawawezi kuzidhuru T-Seli za kutosha na kuzifanya (T-Seli) zife zote mpaka kuishusha chini kinga nzima ya mwili.
Hata wafuasi wa nadharia ya VVU / UKIMWI hukubali kwamba hiki kiwango cha chini cha udhurikaji wa T-Seli kutokana na VVU ni changamoto kwao kuielezea.
4. VVU/HIV hakina Jeni (gene) ya kusababisha UKIMWI:
VVU/HIV hakina gene maalum au sababu ya kipekee ya kusababisha UKIMWI. Retrovirus wote wana jenetiki jeni 3 tu kuu, GAG, ENV na POL na gene zingine ndogo 6 tu. Kwa sababu jeni na utaratibu wa kimfuatano wa kijenitiki katika viumbe hawa rahisi ni mdogo, huhitaji gene zao ili kujirudufu. VVU/HIV hakina tofauti na retrovirusi wengine wote kivinasaba. Kuna retrovirusi 50 hadi 100 tofauti ambao wanaweza kupatikana katika kila mwili wa mtu yeyote mwenye afya. Retrovirusi wote hao 50 mpaka 100 wapo chini ya ulinzi wa kinga ya mwili (antibody). VVU/HIV hakina tabia tofauti yoyote ambayo retrovirusi wengine hawana. Kama retrovirusi hawa wengine hawawezi kusababisha UKIMWI, kwa nini virusi vya ukimwi/HIV? Na kinyume chake, kama HIV husababisha UKIMWI, kwanini hao wengine 50 mpaka 100 hawasababishi Ukimwi? Hivyo hakuna sababu inayoweza kueleza jenetiki ya VVU iwezavyo kusababisha UKIMWI.
5. Hakuna kitu kimewahi kutokea kinaitwa “kirusi cha polepole”:
VVU/HIV vinadaiwa kuchukua miaka 10 hadi 20, kipindi kinachomchukuwa mtu kutoka alipoambukizwa virusi hadi kuugua Ukimwi. Njia pekee ya kuelezea hili ni kuvipa uwezo VVU wa kiuchawi wa kujiamsha (reactivate), uwezo wa kujibadili (mutate), uwezo wa kuhama (migrate) na uwezo wa kupumbaa (hibernate).
Nadharia hizi za virusi vinavyoshambulia polepole zilibuniwa na wanasayansi waliovitumia kununua muda wakati ambapo virusi wao waliposhindikana kuthibitishwa. Watetezi wa virusi vya polepole wanatumia mifano ya virusi kama wa malengelenge (herpes viruses) ambao huunguza polepole na kujificha na kisha kujitokeza tena katika watu wenye virusi hao wakati kinga zao zinapotikiswa na kuishiwa uwezo wa kutosha kuvidhibiti.
Zoezi hili hutofautiana sana katika VVU kwa sababu kiasi kikubwa sana cha virusi wanaweza kupatikana na kusababisha dalili fulani maalum. Kinyume chake, virusi wa taratibu ni uvumbuzi unaoelekeza uwezo wa virusi kusababisha ugonjwa miaka mingi tu baada ya maambukizi – wanakiita kipindi cha kuishi kwa matumaini – katika watu wenye afya bali wanaishi na VVU, bila kujali hali yao ya kinga. Dhana hii inaruhusu wanasayansi kulaumu virusi vilivyokwisha kuvunjwavunjwa baada ya ugonjwa wowote unaojitokeza miongo kadhaa baada ya kuambukizwa VVU. VVU kilishavunjwavunjwa ulipopima na kukutwa positive (+), lakini bado VVU kinasadikika kusababisha zaidi ya magonjwa 30 tofauti miaka hata 10 baadaye.
Hakuna ugonjwa hata mmoja katika haya magonjwa 30 na zaidi wenye uhusiano maalumu hata na VVU vyenyewe. Kwa kawaida ugonjwa utokanao na maambukizi ya virusi lazima ujitokeze ndani ya siku au majuma kadhaa au si zaidi ya mwezi 1, na hili siyo la kujadiliana, muda ambao virusi huhitaji kujirudufu na kusababisha ugonjwa ni lazima utokee ndani ya muda huo isipokuwa kama ugonjwa huo hautokani na virusi. Kwahiyo pengine kuna wanavirusi wa polepole (slow virologists) lakini siyo kirusi cha polepole.
6. VVU/HIV si kirusi kipya, hivyo hakiwezi kusababisha ugonjwa mpya:
Pengine watu wanadhani VVU/HIV kiligunduliwa miaka ya 1980 ulipoanza kutajwa Ukimwi.
Kesi za UKIMWI zilianza kutoka sifuri mwaka 1980 hadi kuripotiwa kesi nusu milioni katika Amerika ya Kaskazini peke yake mpaka kufika mwaka 1995. Kwa hiyo, wanasayansi wengine wanadai VVU/HIV lazima kitakuwa ni virusi kipya la sivyo tungekuwa na janga la ukimwi miaka ya karne iliyopita. Hata hivyo, madai haya yanaangushwa na kanuni za mwanasayansi Farr.
Kanuni ya Farr kwa magonjwa ya kuambukizana kwa njia ya virusi huenea kwa uwiano sawa katika idadi ya watu. Nchini Marekani maambukizi mapya ya VVU yameripotiwa kuwa zaidi au chini ya milioni 1 kila mwaka tangu vipimo vya kwanza mwaka 1984. Hivyo VVU/HIV hakiwezi kuwa kirusi kipya.
7. VVU/HIV kimefeli kanuni za Koch:
Kanuni ya kimataifa inayotumiwa na wanasayansi kutambuwa iwapo ni kweli ugonjwa umesababishwa na maambukizi, ilitengenezwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita na mwanasayansi Robert Koch.
Kanuni hiyo ya Koch inasema:
Kiumbe (kirusi):
- Lazima kipatikane katika matukio yote ya ugonjwa huo.
- Lazima kijipoteze kutoka kwa mwenyeji wake na kujikuza binafsi
- Lazima kisababishe ugonjwa ule ule sawa wakati kimedungwa kwa mwenyeji mpya mwenye afya.
- Lazima kipatikane kinakua tena katika ugonjwa wa mwenyeji wake (host/cell).
- Lazima mbegu za kirusi kupatikana katika matukio yote ya magonjwa. VVU/HIV KIMEFELI.
- Asilimia 10 na 20 ya wagonjwa wa UKIMWI hawana VVU/HIV.
- Ni kiasi kidogo tu cha VVU, kwa kawaida virusi mfu (dormant), ndiyo vinaweza kupatikana katika watu wenye UKIMWI.
- Kadhalika ni lazima mbegu ya kirusi (germ) pekee itoke kwa mwenyeji na kukua na kuwa kirusi binafsi. Hili VVU/HIV KIMEFAULU – lakini katika baadhi tu ya watu sababu ya kiteknolojia:
- Kiasi kikubwa cha tishu za seli zinahitajika ili kupata VVU. VVU/HIV kinahitaji mchakato wa kikemikali ikiwa ni pamoja na kuamka, kinyume chake, kiasi kikubwa cha virusi walioamshwa wanaweza kupatikana pamoja na virusi wengine.
- VVU/HIV havisababishi UKIMWI/AIDS katika majaribio kwa wanyama kama sokwe.
- Wahudumu wa afya ambao kwa bahati mbaya huambukizwa VVU wakati wakitimiza majukumu yao mara chache huugua Ukimwi isipokuwa kama ni watumiaji wa madawa ya kulevya au AZT.
- Kadhalika ni lazima mbegu kupatikana ikiongezeka tena katika ugonjwa mpya unaoletwa na kirusi hicho hicho cha aina moja. VVU/HIV KIMEFELI Kanuni hii – kutokana na kuferi kanuni namba 3.
Wanasayansi wa VVU/UKIMWI wanadai kwamba Kanuni za Koch ni za zamani na zipo nje ya wakati (outdated) katika sayansi za kisasa. Lakini wao wamesimama na mitihani ya muda. Nadharia za magonjwa amabayo yamepuuza kanuni za Koch, zote zimefeli; nadharia ya kuambukiza ya kiseyeye (scurvy), pellagra, beriberi, SMON na utafiti juu ya virusi wa kansa, magonjwa haya yote yamefeli sababu za kupuuza kanuni za Koch. Na sasa VVU / UKIMWI?
8. UKIMWI umebakia ugonjwa wa makundi yale yale ya awali hatarishi kwa zaidi ya miongo 3:
Ikiwa ugonjwa hausambai, lazima uwe umesababishwa na kitu kingine kisicho cha kuambukiza. Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC) kimethibitisha hilo katika taarifa yake mwaka (1997) kwamba UKIMWI hauenei sawa katika jamii nzima.
UKIMWI katika makundi hatarishi (Marekani, 1995/96):
- Mashoga wanaume 54%
- Watumiaji wa madawa ya kulevya (IV drug users) 32%
- Hemofilia 1%
- Waongezewa damu 1%
- Mapenzi ya jinsia tofauti 9%
- Watoto 1%
IKiwa ni kweli UKIMWI unasababishwa na virusi vya Ukimwi, wagonjwa wa UKIMWI wasio katika makundi hatarishi walitakiwa wawe wanaongezeka zaidi ya wastani wa asilimia 10% kadiri ugonjwa unavyosambaa.
Kumbuka kwamba wakati jeshi la Marekani lilipokuwa likifanya vipimo kwa makuruta liligundua kuwa matokeo ya watu waliopima na kukutwa na VVU yalikuwa yamegawanyika hamsini kwa hamsini, asilimia (50%) wanaume na wanawake asilimia (50%). Hata hivyo, asilimia 85% ya wagonjwa wa UKIMWI nchini Marekani ni wanaume.
Kumbuka pia kwamba nchini Marekani wanaume hutumia zaidi ya asilimia 80 ya madawa yote makali ya kulevya. Kati ya wanawake wenye UKIMWI, asilimia 60% wanakiri kutumia madawa makali ya kulevya.
9. Uwiano wa watu wenye Ukimwi kimataifa unatofautiana sana.
Ugonjwa wa kuambukizana kadhalika utaleta uwiano wa idadi ya watu katika njia hiyo hiyo duniani kote. kuzuka kwa kipindupindu katika India na Honduras kutakuwa na kiasi hicho hicho. Lakini UKIMWI ni tofauti kabisa katika Marekani au katika nchi za viwanda za magharibi na nchi za Afrika
UKIMWI katika Afrika ulipaswa kuwa mara 14 juu kuliko katika Marekani. Badala yake, watu wenye VVU Marekani huanza kuugua UKIMWI kwa kasi zaidi mara10 hadi 20 kuliko katika Afrika. Hii ina maana kwamba, wakati muda wa kuishi kwa matumaini ukikadiriwa kuwa miaka 10 hadi 15 nchini Marekani, katika bara la Afrika ni angalau miaka 100-150!
10. UKIMWI hutokea bila ya maambukizi ya VVU na watu wengi wenye VVU kamwe hawaoneshi kuugua UKIMWI:
Ushahidi wa nadharia isemayo VVU = UKIMWI imeegemea tu juu ya uhusiano (correlation). Sababu virusi/hiv hupatikana katika wagonjwa wengi wa UKIMWI, ikadhaniwa huenda hiv/vvu husababisha UKIMWI. Lakini mantiki ya dhana hii ina dosari kwa sababu uhusiano (correlation) hauwezi kuthibitisha Usababisho (Causation), ni kama kusema kila anayefaulu mitihani basi anajisomea sana!
Utokeaji wa kawaida wa VVU/HIV katika wagonjwa wa UKIMWI si ushuhuda tena kwamba VVU husababisha UKIMWI, ni sawa na kusema pia kunguru akisimama kwenye nyanya za umeme ni uthibitisho wa kukatika umeme!.
Hivyo, kama VVU na UKIMWI havihusiani, ni rahisi kupata watu wenye UKIMWI bila kuwa na VVU na watu wenye afya ambao wanaishi na VVU lakini kamwe hawauguwi UKIMWI. Na hicho ndicho kinachotokea.
Katika Afrika utafiti umeonyesha zaidi ya asilimia 65% ya wagonjwa wa UKIMWI hawana VVU. Katika Afrika vipimo chanya kwa HIV katika kinga ya mwili havina muhimu kwa ajili ya kuripoti wagonjwa wa UKIMWI; dalili za kuugua muda mrefu zinatosha.
Kesi 4,621 za UKIMWI bila VVU zimejitokeza katika Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC), ripoti ya hadi 1993. Na idadi inaweza kuwa kubwa zaidi lakini tafsiri rasmi ya UKIMWI imeundwa ili kuondoa kabisa UKIMWI bila ya V.V.U.
UKIMWI unatofautiana karibu na ugonjwa wowote ambao umewahi kutokea duniani kutokana na ukweli kuwa hauna dalili maalumu za ukweli za kudumu. UKIMWI ni neno mwamvuli kwa ajili ya magonjwa mengine zaidi ya 29 ya zamani na mmoja ambao siyo ugonjwa (wa chembechembe za seli T4 wa chini ya 200/ul ya damu) wakati mtu amekutwa na kinga dhidi ya VVU anapofanya vipimo vya ukimwi.
Namna tafsiri ya UKIMWI ya CDC inavyofanya kazi:
- Kaposi sarkoma + HIV = UKIMWI
- kaposi sarkoma – VVU = kaposi sarkoma
- Pneumonia + HIV = UKIMWI
- Pneumonia – VVU = Pneumonia
- Dementia (matatizo ya akili) + HIV = UKIMWI
- Dementia – VVU = Dementia
- Chembechembe chini ya 200 za seli T4 + HIV = UKIMWI
- Chembechembe chini ya 200 za seli T4 – VVU = hakuna ugonjwa
Hakuna ugonjwa ambao husababishwa na VVU/HIV pekee. HIV/VVU inasemwa husababisha magonjwa 29 ya zamani wakati inapokuwepo sasa inapojitokeza sambamba na magonjwa mengine. Wakati HIV/VVU hakijaanza kusemwa husababisha ukimwi, sababu za magonjwa hayo zaidi ya 29 zinajulikana, si VVU/HIV tena.
Tafsiri rasmi ya UKIMWI inajenga uhusiano wa asilimia 100% kati ya Ukimwi na virusi vya UKIMWI. Uhusiano (correlation) huo siyo lengo au jambo la kisayansi, bali ni usanii na ghiriba zilizojaa maslahi binafsi.
Je ni kweli UKIMWI ni ugonjwa wa kuambukizana?
Si kweli. Kwa miaka mingi watu wengi wamekuwa wakiamini kuwa ukimwi ni ugonjwa wa kuambukizana jambo ambalo si kweli. Tunachoamini ni kuwa, ni kweli kinga ya mwili huweza kupungua mwilini kiasi cha kusababisha magonjwa lakini si kweli kuwa V.V.U ndivyo vinavyohusika na kushuka kwa kinga hiyo.
Kama tulivyoona kwenye aya kadhaa hapo juu namna sayansi ya kweli inavyokataa V.V.U kuwa na uwezo wa kusababisha UKIMWI, kwahiyo kama V.V.U havina uwezo wa kusababisha ugonjwa wowote mwilini basi tunaweza kuhitimisha kuwa UKIMWI au Upungufu wa Kinga Mwilini si ugonjwa wa kuambukizana, kama kinga ya mwili wako itashuka basi itaanzia mwilini mwako na kuishia mwilini mwako humo humo, wewe huna uwezo wa kumwambukiza mwingine wala mwingine yeyote hana uwezo wa kukuambukiza wewe.
V.V.U au H.I.V ni nini?
“V.V.U ni kipande tu cha tishu pole mfu chenye ukubwa wa 1 ya 1000 ya ukubwa wa seli ya kawaida, siyo kama vilivyo virusi aina ya retrovirusi vingine vingi vilivyomo katika miili yetu …”
Watetezi wa dhana ya Virusi Vya Ukimwi kusababisha ukimwi wanadhani kwakuwa ukimwi umesambaa kwa kasi tangu mwaka 1981 basi V.V.U ndivyo vitakuwa vimesababisha hilo.
Lakini sayansi imefeli kuuliza swali moja rahisi; Je H.I.V imekuwepo katika mwili wa binadamu tangu mwaka gani?.
Tukitumia kile sayansi hukiita kanuni ya mwanasayansi Farrs (Farrs’ law) tunaweza kuona kuwa H.I.V imekuwepo kwa karne nyingi zilizopita.
Alichokisema mwanasayansi Farr kilikuwa kwamba wakati kirusi kinapojitokeza kuleta ugonjwa kwa binadamu huenea kwa kasi na kwa wote kama tulivyoona katika janga la virusi vya mafua ya ndege. Lakini kwa sababu tangu HIV ilipogundulika ni waMarekani milioni 1 tu ambao ndio wanasemwa kuwa na H.I.V kila mwaka kwa zaidi ya miaka 20 sasa na haionyeshi dalili ya kukuwa na kusambaa kwa wote, kirusi cha H.I.V hakiwezi kuwa ni kitu kigeni katika mwili wa binadamu. H.I.V ni kitu cha zamani kuliko hata nchi unayoishi, kimekuwepo katika miili ya watu wengi na watoto wao kwa karne kadhaa kwa mjibu wa Farrs’ Law.
Hebu tuone sasa tangu mwanzo namna H.I.V ilivyogunduliwa na kusemwa husababisha ugonjwa usioponyeka wa UKIMWI.
Luc Montagnier daktari na mwanasayansi wa Ufaransa ndiye alikuwa wa kwanza kukibaini kirusi cha H.I.V mwaka 1982 na matokeo ya utafiti wake yakatumwa katika maabara huko Califonia Marekani kwa uchunguzi zaidi ambako daktari mwingine Robert Gallo mwenyewe binafsi akaeleza kuwa amekigunduwa kirusi hicho na akakipa jina HTLV 1, kwahiyo mwanasayansi huyo mfaransa akaamua kufunguwa mashtaka kwa upotoshaji wa Robert Gallo na wanasayansi hawa wawili wote ndio wanaosemwa kuwa waligunduwa aina hii ya kirusi cha kiretrovirusi kiitwacho H.I.V.
Muda mchache kabla ya janga la UKIMWI kutangazwa katikati ya miaka ya 1980 Dr.Robert Gallo alikuwa ni mwanasayansi aliyekuwa akiendelea na utafiti juu ya ugonjwa wa kansa. Utafiti wake huo katika kansa ulifanana kwa karibu na utafiti wa UKIMWI. Dr Robert Gallo alikuwa akijaribu kuthibitisha kuwa kirusi kile kile kinachofanana na cha UKIMWI (HTLV 1) ndicho kilikuwa kikisababisha ugonjwa wa kansa. Utafiti wake huo upande wa kansa haukuzaa matunda na akashindwa kuthibitisha kwamba HTLV 1 ndicho kilikuwa kikisababisha kansa.
Dr.Robert Gallo akapata nafasi nyingine mwanzoni mwa 1980 tena kuthibitisha nadharia ya kirusi chake dhidi ya UKIMWI ambapo yeye na baadhi ya wanasayansi wengine jamaa zake walikuwa wakidai kwamba kirusi kiitwacho H.I.V kilikuwa kikizishambulia na kuziua T-Cells ambazo ni seli maalumu zinazounda mfumo wa kinga ya mwili wa binadamu. Na hata sasa Gallo ameendelea kudai H.I.V na virusi vingine vimekuwa vikiziuwa T-Cells na siyo H.I.V peke yake.
Kutoka katika kitabu kiitwacho Deadly Deception cha dr Robert E. Willner M.D., Ph.D:
‘H.I.V haisababishi UKIMWI…. Kitu ambacho kila mtu anakikosa ni kwamba hizo karatasi zote Gallo ameziandika kuhusu H.I.V na UKIMWI zimegundulika kuwa ni za uongo na nadharia kuhusu UKIMWI imeegemea katika hizo karatasi zake. — Dr. Peter Duesberg’.
Namna uongo ulivyoanza:
Mwaka 1980, Dr. Robert Gallo ambaye ni mwanaretrovirusi akiwa katika taasisi ya taifa ya kansa ya Marekani alidai alikuwa amegunduwa kirusi katika kundi la retrovirusi kiitwacho HTLV-I. Kirusi hiki cha retrovirusi kinatofautishwa na virusi vingine vya kawaida kutokana na sifa ya R.N.A yake kuweza kubadilika kuwa D.N.A kwa kimeng’enya (enzyme) kiitwacho kwa kiingereza ‘reverse transcriptase’.
Kujizalisha, kuongezeka na kuishi kwake kwa retrovirusi kunategemea uhai wa seli ambayo hiki kirusi kimo ndani yake. Ikitokea seli inayokishikiria hiki kirusi inakufa basi hata kirusi nacho hufa pia. Dr. Gallo alikuwa akiujuwa ukweli huu ingawa kwa haraka na kwa makusudi aliamua kuudharau ukweli huu ili kutimiza malengo yake binafsi kwa kudai kwamba kirusi hicho kilikuwa ni kirusi cha maajabu sana kuwahi kutokea. Akaendelea kudai kuwa kirusi hicho cha ajabu kingeweza kudumu kimaajabuajabu kwa kuwaua mamilioni ya watu kitu ambacho hakijawahi kutokea. Ikumbukwe kabla huyu jamaa alishindwa kuuthibitishia ulimwengu kuwa kirusi kile kile chake sawa cha HTLV 1 kilikuwa kikisababisha kansa ya damu (leukemia) nchini Japani. Sababu ya kuwa na nguvu za kimadaraka zile za kuwa mtu mkubwa na mwanasayansi serikalini, ndizo ziliruhusu kosa la lebo ya kirusi wa leukemia kukubaliwa kuwa ndicho kilikuwa kikisababisha leukemia hata baada ya jopo la wanasayansi kuikataa nadharia hiyo.
Mwaka 1980, ilikuwa ikipendekezwa kuwa upungufu wa kinga mwilini (acquired immune deficiency) ulikuwa ndiyo msingi wa dalili ya ugonjwa mpya ujulikanao kama UKIMWI ambao ulikuwa ukionekana kuwatokea zaidi wanaume mashoga na wale waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya hasa yale ya kujidunga kwa sindano.
Dr. David Durack wa chuo kikuu cha DUKE, ambaye ni bingwa katika magonjwa ya kuambukiza na mfumo wa kinga ya mwili, anasema ingawa anakubaliana na uhusiano wa madawa ya kulevya kama ‘poppers’ na ‘amyl nitrites’ na maambukizi ya kujirudiarudia, alidharau hivyo vitu vinavyojulikana wazi kusababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kutangaza kuwa hizi dalili mpya za kushuka kwa kinga ya mwili lazima ziwe zinaletwa na ‘jambo jipya’. Kundi hili la wanasayansi hawa wamejifungia katika nadharia yao hiyo pasipo kuwa na ukweli wowote wa kisayansi kwamba ni kwa namna gani kirusi chao cha ukimwi (H.I.V) kinaweza kusababisha matendo machafu yote hayo mwilini. Neno ‘inasadikika au kufikirika’ ndilo hutumika kila mara katika majibizano ya kawaida au katika majarida, magazeti na vitabu visivyo vya kisayansi. Katika majarida ya kisayansi au mafunzo ya kisayansi nadharia huwasilishwa kama ukweli uliothibitishwa na kwahiyo unakubalika hivyo na wanasayansi wengi ikijumuisha wanafizikia pia. Kumbe hicho kinachoitwa kirusi cha ukimwi (H.I.V) bado kinawasilishwa kama ni kirusi ‘kipya’ pamoja na ukweli usiopingika kuwa hakuna upya wowote hapo. Kwa uongo mkubwa kirusi hicho kimekuwa kikielezwa kuwa ni kirusi kinachoshambulia na kudhuru kinga ya mwili wakati ukweli ni kuwa hilo haliwezekani kwakuwa kirusi hicho si kiumbe au kitu chenye uhai na wala hakina uwezo wa kushambulia kitu chochote mwilini. Virusi aina ya Retrovirusi humezwa na kujumlishwa katika maisha ya kila siku ya seli na kuwa na ukubwa wa 1/1000 ya ukubwa wa seli ya kawaida.
Mwaka 1983, Dr. Gallo alianzisha mpango mwingine wa kuwashawishi wanasayansi rafiki zake wengine bila kuwepo kwa ushahidi au uthibitisho wa kimajaribio ya kisayansi kwamba alikuwa amegunduwa kirusi kingine ambacho kilikuwa kikisababisha UKIMWI.
Kwenye mkutano mkubwa kabisa uliofanyika Washington, D.C. tarehe 23 aprili 1984, Dr. Gallo akatangaza kwamba amegunduwa kilichokuwa kinasababisha ugonjwa wa UKIMWI. Dr Gallo akanena juu ya ugunduzi wake wa kirusi kipya kundi la retrovirusi ambacho alikuwa amekipa jina HTLV-III, hivyo na kuhitimisha kwamba kirusi hicho kilikuwa ni miongoni mwa virusi kundi la retrovirusi alivyokuwa amevigunduwa kabla. Madai yake haya yaliungwa mkono na Margaret Heckler, aliyekuwa Waziri wa afya na huduma za jamii ambaye alikuwa katika presha za kisiasa na kuja na jibu la ‘janga’ jipya. Waziri Heckler alitangaza; ‘Leo tunaongeza muujiza mwingine katika heshima ya muda mrefu katika dawa na sayansi ya kimarekani’, akaahidi pia kuwa kinga ya ugonjwa huo itakuwa imepatikana ndani ya miaka miwili inayokuja, bilashaka yeyote kama matokeo ya Dr. Gallo kulazimisha uongo kuwa ukweli.
Siku hiyo hiyo Dr. Gallo akajaza leseni ya kifaa cha kupimia UKIMWI ambacho kilikusudiwa kumtengenezea mamilioni ya pesa. Dr. Gallo mtu mwenye ujuzi mkubwa usiotiliwa shaka yeyote katika fani ya retrovirusi akachagua kuuweka ukweli pembeni na kuhalalisha baya kuwa zuri. Faida kwa Dr. Gallo ni pesa na nguvu lakini gharama kwa ubinadamu ni mateso na maelfu ya vifo visivyo vya lazima. Kinyume chake, wanawake malaya wa barabarani ni wakarimu zaidi – unakijuwa nini unachopewa na unayajuwa matokeo au gharama yake – na kwa hakika UKIMWI si mojawapo ya matokeo au gharama hizo.
Kwa haraka Margaret Heckler akatoa mkataba wenye faida kwa utengenezeaji wa dawa ya kupunguza makali ya UKIMWI iitwayo AZT kwa kampuni ya Burroughs-Wellcome Pharmaceutical Company kabla hata ya chapisho la kwanza la kisayansi kuhusu ugunduzi huo kutokea/kuchapwa kwenye majarida ya Marekani.
AZT ilikuwa ni dawa ikitafuta ugonjwa wa kutibu na ilikuwepo kwenye makabati ya taasisi ya taifa ya kansa ya Marekani tangu mwaka 1960. Dawa hiyo ilikuwa imetumika kwenye majaribio ya kutibu kansa na ikashindwa, kisha ilitolewa kwenye matumizi kufuatia kugundulika kuwa ina sumu nyingi sana kwa matumizi ya binadamu. Fani ya Retrovirusi ilipata umhimu wakati huo kutokana na vita dhidi ya kansa kwa kampeni iliyoenda kwa jina la Nixon’s “War on Cancer” na imani kuwa retrovirusi ndiyo sababu au ndiyo chanzo cha kansa kwa binadamu. Imani hiyo ilionekana kuwa na mashiko kwa wakati huo kwa sababu retrovirusi vina tabia ya kuchochea seli kujizidisha au kuongezeka idadi – ambayo ni sifa mojawapo katika kukua kwa kansa. Hii ni tofauti ya moja kwa moja kwa uharibifu wa seli ambao kwa kawaida hutokea katika maambukizi yatokanayo na virusi.
Siyo kwamba ni hiyo vita pekee dhidi ya kansa ndiyo iliyofeli, AZT ilifeli pia, na wataalamu hao katika masuala ya retrovirusi wakaja mikono mitupu hata baada ya miaka 20 ya utafiti huo mkubwa na mzito. Cha kushangaza, Bila sababu yoyote ya mhimu (without a reason d’etre!) kundi zima la wanasayansi, kama ambavyo ungetegemea, mwaka 1986 katika mkutano mkuu wa kimataifa wa wataalamu wa retrovirusi (The International Committee of Retrovirologists) wakaitaja H.I.V (V.V.U) kama ndiyo chanzo au ndicho kitu kinachosababisha ugonjwa wa UKIMWI (AIDS).
Kwa kuisadiki nadharia hiyo ya H.I.V kusababisha UKIMWI bila uwepo wa uthibitisho wa kisayansi wanamkutano huo wote wakawa ni sehemu ya hii njama chafu. Ni kama vile kila mmoja angeweza kutegemea nini kitatokea pale Mbweha waliochanganyikiwa kwa kukosa kitoweo kwenye mawindo yao wanapoachwa peke yao kulinda banda la kuku.
Ukiongeza sasa kwenye fujo za Dr. Gallo kwa kudharau umhimu wa kuthibitisha kisayansi madai yake, ilikuja kugundulika kuwa HTLV-III ilikuwa ni retrovirusi ambacho kilitumwa na daktari mwingine mfaransa Luc Montagnier wa Pasteur Institute ya Paris kwenda kwa Dr. Gallo zaidi ya mwaka mmoja kabla. Katika nyakati tofauti Montagnier alikuwa akituma sampuli za virusi alivyokuwa amevigunduwa katika damu za waathirika wa UKIMWI kwenda kwa Gallo kwa ajili ya utafiti zaidi. Skendo hiyo ikavuma na ugomvi huo ulizuka juu ya mwenye kustahili kupewa cheo na hati miliki ya ugunduzi. Ilipelekea kuingilia kati kwa aliyekuwa waziri mkuu wa ufaransa wakati huo Jacques Chirac na rais wa Marekani Ronald Reagan ili kufikia makubaliano ambayo yalikuwa ni umiliki wa pamoja wa mapato yatokanayo na ugunduzi huo (hivi karibuni ufaransa ilitoa changamoto tena baada ya Gallo kukiri huenda alikuwa amefanya makosa), hii ni tabia ya kweli ya watu matapeli au watu wafanyao mambo maovu kwa maksudi ya wazi kugombana juu ya mali waliyoipata kilaghai.
Ni mhimu kuelewa hapa kuwa tangu mwanzo neno UKIMWI linawakilisha kifupi cha maneno ‘Upungufu wa Kinga Mwilini’ ambao ndio unaojadiliwa, kupelelezwa na kuhakikiwa katika makala hii. Hitimisho lisilopingika ambalo ongezeko kubwa la wanasayansi maarufu pia wamefikia ambalo nina uhakika ndilo utakalolifikia wewe pia, ni kwamba UKIMWI kamwe hauwezi kutafsiriwa na kukubalika kama ni ugonjwa au dalili za ugonjwa wa aina yeyote ile. UKIMWI ni kusanyiko na ongezeko la pamoja la idadi ya magonjwa na dalili zaidi ya 25 (kutegemea na chanzo) kwa ajili ya kujengea hoja ya kitapeli kwamba janga hilo lipo kweli.
Kitu kingine unachotakiwa kuelewa ni kuwa Gallo na kundi lake wamekuwa wakikimbia hatua moja ya msingi na mhimu kabisa katika sayansi, nayo ni kukataa kufanya majaribio yanayodhibitiwa ambayo matokeo yake ndiyo yatakuwa ni ukweli unaokubalika na wanasayansi wote kote duniani. Majaribio kama hayo yangeuanika ulaghai wao peupe. Badala yake wamekuwa ni watu wanaotegemea hofu, vitisho, vioja, tama za vyeo, uroho, husuda na tamaa ya umaarufu. Katika hali hii wamefanikiwa kulazimisha kutia ujinga jeshi kubwa la wafuasi katika kuamini kile ambacho miaka ya nyuma kingekuwa ni kitu cha kuchekwa tu au kuchukuliwa kama hadithi tu za kawaida.
Binadamu wote tumekuwa tukijijuwa zaidi ya nusu karne sasa kwamba wote tunaishi na kutembea na bakteria wengi na virusi katika miili yetu. Wote tunajuwa kuwa kwenye miili yetu tunaishi na vijidudu hatari muda wote wa maisha yetu vikisubiri tu usawa wa mwili kuwekwa katika hali ya kuvutia ugonjwa fulani. Magonjwa kama Streptococcus, kifua kikuu na vichomi, ni magonjwa yanayoweza kumpata yeyote muda wowote. Vijidudu vya ugonjwa wa kifua kikuu kwa mfano vinaweza kuonekana karibu katika kila mapafu ya kila mtu. Lakini hata hivyo ni watu wachache kati yetu wanaugua ugonjwa wa kifua kikuu. Huu ni moja ya mifano mhimu kati ya magonjwa mengi yanayoitwa nyemelezi kwa watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi magonjwa ambayo mengi kati yake kila mmoja amewahi kuugua mara moja au mbili katika kuishi kwake.
Hebu jiulize maswali yafuatayo kwa sasa:
Wakati mlipuko wa homa ya mafua makuu ya mwaka 1919 ulipochukua maisha ya mamilioni ya watu wa Marekani, kwanini hayakudhuru waMarekani wote kwa pamoja?
Wakati ugonjwa wa tauni ulipoangamiza theruthi moja ya idadi ya watu wa bara la Ulaya, kwanini theruthi zingine mbili ya watu hawakufa pia?
Kanuni kumi za ulaghai:
1. Ulinganifu ni uthibitisho wa chanzo na matokeo yake.
2. Ushahidi bila kithibitisho ni ukweli wa moja kwa moja.
3. Mfano mmoja tu unathibitisha kanuni.
4. Kisio (Dhanio) moja likisaidiwa na kisio jingine linatengeneza ukweli.
5. Kwa kukisema tu kitu kiko hivi, tayari hicho kitu lazima kiwe hivyo.
6. Usichanganye habari na ukweli.
7. Uthibitisho si kitu cha lazima na ni lazima uepukwe.
8. Ongopa, ongopa, ongopa na mwisho wataamini tu.
9. Wezesha ukimya, dharau na kanusha ukweli.
10. Weka imani (kitu kisichohakikiwa), ulaghai na upofu wa uwoga mahali pa mantiki.
Kurudiwarudiwa kwa matumizi ya hizi kanuni 10 za ulaghai na wala njama za H.I.V kuleta UKIMWI ndiko kulimpelekea T. C. Fry ambaye ni mwandishi wa kitabu kiitwacho The Great AIDS Hoax (Uongo Mkubwa kuhusu ukimwi), kuandika: “Uwepo wa kile wanachokiita H.I.V katika ugonjwa wa UKIMWI si uthibitisho tena wa kinachosababisha UKIMWI zaidi ya uwepo wa inzi kwenye takataka kuwa si uthibitisho kwamba inzi ndizo zilizosababisha uwepo wa takataka hizo.” Ingawa hilo lingewezekana kama utawachukulia hawa wahuni kina: Robert Gallo, Anthony Fauci, William Haseltine, Max Essex, James Curran, Flossie Wong-Staal, Dani Bolognesi, Margaret Fischl, Margaret Heckler na jamaa zao wengine kuwa ni ma-inzi na kwa hakika basi hata takataka (UKIMWI) zilitengenezwa na wao!.
MWANGAZA WA MATUMAINI:
Tabia ya kumchafua mtu kama matokeo ya changamoto anazozitoa kwako ni ushahidi wa wazi wa nafasi au habari isiyolindika/hifadhika. — Robert Willner
Kuanzia mwaka 1987, mwangaza wa ukweli ukaanza kupenyeza juu ya unafiki wao. Kwa hawa wala njama, ilikuwa ni dalili ya mwanzo ya kuanguka kwao (ikiwa haki hushinda). Ilianza wakati Dr. Peter Duesberg, mwanasayansi nguli wa kimataifa katika masuala ya retrovirusi, alipoandika chapisho katika utafiti wa kansa ambalo lilitikisa ule msingi kabisa wa nadharia ya V.V.U/UKIMWI. Wanasayansi wengi waliachwa na mshangao kutokana na nafasi aliyokuwa nayo lakini walivutiwa sana na ukweli wake. Wengine wakapata tulizo kwamba walau hatimaye mtu mmoja amepata ujasiri wa kusema kwa uwazi. Matokeo yake wenye nguvu na wanao faidika na uongo huu na wawekezaji wao wakamshambulia daktari huyu na tena siyo kwa kutumia kweli za kisayansi bali kwa kulichambuachambua jina lake, akapakwa matope na tuhuma kibao, wakamuaziri, wakamkejeli na kuanza kumshusha kisiasa na kiuchumi. Matendo na maneno yao kwa daktari huyu yakadhihirisha hatia zao.
Kisha mwezi februari 1989, Dr. Duesberg akawasilisha mwendelezo wa ripoti yake pana zaidi ya uchambuzi kwa waandamizi wa taasisi ya sayansi ya taifa ya Marekani (National Academy of Sciences). Kundi hili lenye hadhi kubwa katika umma halikuchukuwa hatua yoyote zaidi ya kuudharau ujumbe wake njia ambayo ni salama kabisa katika ulimwengu wa kisiasa na kisayansi ijulikanayo kama ‘funika kombe mwanaharamu apite’. Na ikiwa ikatokea mwanaharamu akaonekana basi kila mara jibu litakalomfaa ni kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai yake. Na wakati huo huo mamilioni ya watu wameendelea kufa!
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la dalili au idadi zaidi ya magonjwa ambayo hujumishwa ili kuupata UKIMWI kwa watu waliopima na kukutwa positive, hii imetokana na ukweli kuwa walaghai walikuwa na haraka haraka mwanzoni katika madhanio yao juu ya kile kinachosababisha ukimwi na kwamba sasa ni kama wanataka kutuambia kuna aina nyingine tena ya virusi vinavyoleta UKIMWI tofauti na H.I.V ili tu ulaghai wao usije ukagundulika huku wakiukwepesha ukweli mhimu unaokubalika kisayansi wa kile kinachosababisha upungufu wa kinga mwilini ambacho ni Madawa yenyewe ya hospitalini yanayotumika katika kutibu magonjwa nyemelezi na maambukizi yanayojirudia mara kwa mara (repeated infections).
Sasa walaghai wanakiri wazi kuwa VVU peke yake haviwezi kusababisha majanga yote haya katika ugonjwa wa UKIMWI na kwamba kuna washirika wengine mhimu wanaohusika. Hata hivyo sisi sote tunajuwa tangu zamani kwamba hawa washirika wengine wanaoharibu kinga ya mwili wamekuwa wakiyafanya haya karne nyingi zilizopita kabla ya H.I.V kuhusishwa. Ni V.V.U/H.I.V ambavyo havina uhusiano wowote na UKIMWI/AIDS.
LAKINI NI KWA JINSI GANI HATA WAKAFANIKIWA KUUPITISHA ULAGHAI HUU USIOFIKIRIKA?
Inawezekanaje hata jambo hili likatokea? Kwa hakika, haiwezekani kwamba ulaghai wa kiwango hiki ungeweza kupenyeza ndani ya umakini na uchunguzi wa maelfu ya wanasayansi kote duniani ambao wamekuwa wakichunguza mambo mengi katika majanga mengi ya kiafya katika ulimwengu huu wa kisasa.
Lakini yote hayo yalianzia kwa wanasayansi wachache wajuvi katika fani ya retrovirusi (retrovirologists) fani ambayo ni wanasayansi wachache wana ujuzi nayo. Mimi binafsi nilikuwa nikisoma na kukubali kwa asilimia zote machapisho ya awali katika majarida ya kisayansi, magazeti, na majarida mengine maarufu.
Kwa hakika nani angetilia shaka matamko ya vitengo, mawakala na taasisi nyeti za serikali? Hakuna. Hata hivyo matamko mengi kuhusu virusi hivi hayakupokelewa kirahisirahisi sana kwangu, ilikuwa miaka kadhaa kabla sijaanza kuwa na wasiwasi wa dhahiri juu ya kile nilichokuwa nikikisoma. Nadhani ilikuwa ni sababu ya miongo miwili na nusu ya kufanya kazi ya utabibu na kule kushindwa wazi taratibu kwa matibabu ya UKIMWI ya kulazimishwa bila kuhoji nikajifunza kuhoji mafunzo niliyokuwa nimefunzwa na kuamini juu ya ugonjwa huu.
Kwa ufupi hivyo ndivyo H.I.V ilivyobuniwa.
Wanasayansi wengine wa ukweli wanasemaje kuhusu VVU/UKIMWI?
WASEMAVYO WANASAYANSI KUHUSU V.V.U/UKIMWI.
Utata
• Dr Kary Mullis, mwanazuoni wa biokemia (Biochemist), Mshindi wa tuzo ya nobel ya mwaka 1993 katika Kemia, anasema:
“Kama kuna ushahidi kwamba V.V.U husababisha UKIMWI, kulipaswa kuwepo waraka wa kisayansi ambao aidha waraka mmoja mmoja au kwa pamoja ukionyesha ukweli huo walau kwa uwezekano mkubwa. Hakuna waraka au dokumenti hizo”. (Sunday Times (London) Novemba 28, 1993.)
• Dr Heinz Ludwig Sanger, Profesa wa molekuli Biolojia na Virolojia, katika taasisi ya biokemia ya Max Planck, München. Ambaye ni mshindi wa tuzo ya Robert Koch ya mwaka 1978, anasema:
“Hadi leo hakuna ukweli hata mmoja wa kisayansi wenye kushawishi ushahidi wa kuwepo kwa V.V.U. Hata pale Retrovirusi huyu alipotengwa (cultured) na kutakaswa kwa njia ya ‘’classical virology”. (Barua ya Süddeutsche Zeitung 2000)
• Dr Serge Lang, Profesa wa Hisabati, Chuo Kikuu cha Yale, anasema:
“Siuamini uhusiano wowote baina ya V.V.U na maradhi yoyote kama ambavyo tumeelezwa. Nimeona ushahidi namna takwimu zisizo za kweli kuhusu V.V.U na UKIMWI zikipitishwa kama sayansi, na kwamba wanachama wa juu katika sayansi kwa makusudi kama si kukosekana kwa uwajibikaji , wakijiunga na vyombo vya habari katika kueneza taarifa potofu juu ya asili ya UKIMWI”. (Yale scientific, Fall 1994)
• Dr Harry Rubin, Profesa wa Molekyuli na seli Biolojia, Chuo Kikuu cha California Berkeley, anasema:
“Haijathibitishwa iwapo UKIMWI unasababishwa na maambukizo ya V.V.U, tena bado haijathibitishwa kama V.V.U vina jukumu lolote katika dalili za UKIMWI”. (Sunday Times (London) Aprili 3, 1994)
• Dr Richard Strohman, Profesa mstaafu wa Seli Biolojia katika Chuo Kikuu cha California Berkeley, anasema:
“Katika siku za zamani ilikuwa inahitajika kuwa mwanasayansi atoe pia uwezekano wa kuithibitisha nadharia yake kuwa ya kweli vile vile kama si ya kweli. Sasa hakuna hilo katika V.V.U/UKIMWI pamoja na mabilioni yote ya dola yanayoelekezwa katika utafiti”.
‘’Tunahitaji utafiti juu ya sababu zinazoweza sababisha UKIMWI kama vile madhara ya kutumia madawa ya kulevya na mabadiliko ya tabia, siyo kuegemea nadharia zilizofilisika’’. – Sunday Times (London), Aprili 1994
• Dr Harvey Bialy, mwanabiolojia wa molekyuli, aliyekuwa mhariri wa Bio / Teknolojia na Nature Biotechnology, anasema:
“V.V.U ni retrovirusi wa kawaida. Hakuna kitu kingine kuhusu virusi retrovirusi hawa ambacho ni cha kipekee. Kila kitu kinachogunduliwa kuhusu V.V.U kinafanana na kile kinagunduliwa katika retrovirusi wengine waliopo mwilini ambao hawasemwi kusababisha UKIMWI. VVU ina inamiliki sehemu ndogo sana ya taarifa za kijenetiki. Hakuna njia yoyote virusi hawa wanaweza kufanya mambo haya yote wanayosema kirusi hiki huyafanya mwilini”. (Spin juni 1992)
• Dr Gordon Stewart, Profesa mstaafu wa Afya ya Umma, Chuo Kikuu cha Glasgow, anasema:
“UKIMWI ni ugonjwa wa tabia. Ni suala mtambuka, huletwa na jumla ya matokeo ya maisha ya kisasa katika mfumo wa kinga – Madawa ya kulevya, dawa na burudani, magonjwa ya ngono na maambukizi mengine ya virusi”. (Spin juni 1992)
• Dr Alfred Hässig, (1921-1999), aliyekuwa Profesa wa elimu ya kinga mwili (immunology) katika Chuo Kikuu cha Bern, Uswisi na mkurugenzi wa zamani wa benki ya damu ya chama cha msalaba mwekundu (Red Cross), anasema:
“Hukumu ya kifo inayosindikizwa na matibabu ya UKIMWI inapaswa kukomeshwa”. (Sunday Times (London) Aprili 3, 1994)
‘’Katika tafiti zinazohusu virusi, fedha nyingi sana huwekezwa, na watafiti wanatamani kubaki eneo hili la kutafiti virusi sababu ikiwa utabadili mwelekeo mwingine wa utafiti kuna uwezekano watu wengine wa upande mwingine kuingizwa katika utafiti badala yao’’
‘’Wanavirusi hawana jingine jipya la kuleta. Hawachoki kuja na visingizio, wanauona ukuwaji usiobadilika na ubadilikaji wa umbile la kirusi; kinashambulia, kinapumzika, ni kitu kigeni, lakini hakuna hata mmoja wao mwenye ujasiri wa kuelezea namna mambo yote hayo yanavyoweza kutokea’’
‘’AZT (dawa ya kudhibiti virusi au ARV kwa waathirika wa ukimwi) imeripotiwa katika kesi zisizo hesabika juu ya matendo yake yasiyoepukika ya kuzinyima pumzi seli za mgonjwa. Madaktari kimakosa wako bize kutibu madhara yatokanayo na matumizi ya AZT kufuatia maambukizi ya awali ya H.I.V. Matibabu kwa kutumia AZT na dawa sumu zingine zinazoambatana nayo inaweza kuwa ni sawa na watu maelfu waliovalia mabomu ya kujitoa mhanga wakisubiri dakika za kujiripuwa kwa ajili ya maelfu wengine’’
‘’Ni wajibu wa daktari yeyote kuokoa maisha ya mgonjwa kwa gharama yeyote na siyo kukupa kifo – Watu wenye bahati mbaya kwa mjibu wa vipimo wanavyovichukuwa huishiwa nguvu na kuchanganyikiwa na mwisho wanajiuwa wenyewe. Ninajisikia huzuni kusema kuwa uchawi huu kupitia hizi mbinu za matibabu ulifanyika hata ingawa hakukuwa na uthibitisho kwamba kuonekana kwa kinga mwili katika damu (antibodies) ni kiashirio cha vifo katika wagonjwa wote wanaotibiwa kama waathirika wa UKIMWI. Ninalichukulia suala hili kama zoezi baya la matibabu kuwasukuma wagonjwa katika kufa kwa kuwatabiria wafu watarajiwa. Sisi ni wanasayansi waganga, siyo Manabii!’’. – Contunuum Jan/Feb 1996
• Dr Charles Thomas, aliyekuwa Profesa wa Biokemia katika vyuo vikuu vya John Hopkins na Harvard, anasema:
“Imani ya V.V.U kusababisha UKIMWI inawakilisha utapeli na pengine ndio udanganyifu pekee mkubwa zaidi wa kimaadili uliowahi kutokea na kufanywa dhidi ya vijana na wanawake wa dunia ya Magharibi”. (Sunday Times (London) Aprili 3, 1994)
“UKIMWI umekuwa ni ugonjwa wa tafsiri (definition). Kama tukisema kwamba H.I.V haipo na kwamba hakuna sababu ya kupoteza pesa za walipakodi, UKIMWI utapotea wenyewe kimya kimya nyuma ya vifo vya kawaida’’. – Penthouse April 1994
‘’Nadhani kwamba kwa wanasayansi kubaki kimya mbele ya nyuso hizi zote za mashaka, ni sawa na jinai ya uzembe wa hali ya juu’’ – Spin June 1994
• Dr Joseph Sonnabend, Daktari wa New York na mwanzilishi wa mfuko wa Marekani wa utafiti wa UKIMWI (American Foundation for AIDS Research – AmFAR), anasema:
“Utangazwaji wa UKIMWI, kupitia taarifa za vyombo vya habari na taarifa, kwama virusi vya VVU pekee husababisha UKIMWI bila ya haja ya kuzitaja sababu nyingine yoyote, kumepelekea tafiti na matibabu ambayo yanaweza kuwa ndiyo sababu ya mateso na vifo kwa maelfu ya watu”. (Sunday Times (London) Mei 17, 1992)
• Dr Andrew Herxheimer, Profesa mstaafu wa famakolojia (Pharmacology) katika UK Cochrane Centre, Oxford, anasema:
“Nadhani zidovudine [AZT] haijawahi kamwe kutathminiwa vizuri na kwamba ufanisi wake haujawahi kuthibitishwa, lakini sumu yake ndicho kitu muhimu. Na nadhani AZT imeshauwa watu wengi hasa watu waliopo katika viwango vya juu vya matumizi yake. Mimi binafsi nadhani kuwa AZT haina thamani yoyote kutumika peke yake au katika mseto wa aina yoyote katika ugonjwa wowote”. (Continuum Oktoba 2000)’’.
•Dk Roger Cunningham, mwanazuoni wa kinga mwili (Immunologist), Mubailojia ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha kinga mwili katika Chuo Kikuu cha Buffalo New York, anasema:
“Kwa bahati mbaya, inaonekana wazi uanzishwaji wa UKIMWI ulikuwa na lengo la kuzikataa changamoto hasi juu ya nadharia ya UKIMWI na mara nyingi ikisisitizwa kuamini nadharia zisizokubalika na upande mwingine’’ – Sunday Times, London Aprili 3, 1994
•Dr Mohammad Ali Al-Bayati, mtaalamu wa masuala ya sumu (Toxicologist) ambaye pia ni mwanazuoni katika fani ya magonjwa (Pathologist), California, anasema:
“V.V.U si sababu ya UKIMWI. Hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba V.V.U inaweza kuziua chembechembe seli T4 zilizoathirika. Tatizo la kweli ni kwamba waanzirishi wa dhana ya V.V.U = UKIMWI wamekuwa wakizipuuza kweli za kisayansi, na kama ni vipofu vile wamekipa lawama kirusi cha H.I.V/V.V.U juu ya ugonjwa wao wa UKIMWI. Ni jambo la kuhuzunisha na kukatisha tamaa kujua kwamba waanzishaji wa UKIMWI wanatoa dawa zenye sumu nyingi kama vile AZT kwa wanawake wajawazito hata hata baada ya tafiti nyingi kuonesha kuwa kupunguwa kwa kinga ya mwili kunaweza kurekebishwa kwa kula lishe sahihi. Kuendelea kutoa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV/AZT) kwa waathirika wa UKIMWI ni kumwaga petroli katika moto”.
•Dr Walter Gilbert, Profesa katika Molekyuli za Biolojia ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobel ya kemia kwa mwaka 1980, anasema:
“Haitakuja kushangaza kama kulikuwa na kitu kingine ambacho ndiyo sababu ya UKIMWI na hata kuwa V.V.U havihusiki”. – Omni Juni 1993
“Dokta Duesberg yupo sahihi kabisa kusema kwamba hakuna mtu ameonyesha kwamba UKIMWI unasababishwa na virusi vya UKIMWI. Yupo sahihi kabisa pia anaposema kwamba virusi waliobuniwa katika maabara hawawezi kuwa sababu ya UKIMWI.” – Hippocrates Septemba /Oktoba 1988
“Jamii kwa ujumla haiwasikilizi kwa subira na umakini wakosoaji ambao wamekuwa wakileta maoni mbadala. Ingawa somo kubwa la historia ni kwamba elimu imeendelea kupitia migongano ya kimaoni”. – Meditel 1990
•Dr Albert Sabin, Mwanazuoni katika fani ya Virusi, anasema:
“Nadhani maoni ya mtu kama Dr Duesberg ni ya mhimu, mhimu sana, na ni lazima kuyapa kipaumbele maoni yao”. – Oakland Tribune Januari 31, 1988
•Dr Rush Wayne, MA, Molekyuli Biolojia, Chuo Kikuu cha Harvard, PhD, Biokemia, Chuo Kikuu cha California, anasema:
“Wakati mwanzo naanza kujifunza kuhusu utata juu ya UKIMWI, nilisoma chochote mimi ambacho ningeweza katika pande zote mbili. Bado sijapata namna, wakati pande zote mbili zilipoweza kumaliza kesi yao, pale ambapo maelekezo yaliyotangulia ya dhana ya VVU/UKIMWI yanapokuwa yameaminika na kukubalika kamili. Kinyume chake, sehemu kubwa ya maoni ya dhana tangulizi na inayotawala ya ukimwi inaonekana kuegemea tafiti mbovu na hoja za uongo’’.
•Michael Ellner, Medical hypnotherapist, Rais wa Ponyeni New York, anasema:
“Nimemuona gaidi asiyeyumba na programu ya kupata ugonjwa na kufa, katika watu wenye bahati mbaya kuonyesha kushuka kwa kinga ya mwili. Ninamini katika dhana inayosema matumizi ya muda mrefu ya madawa ya kulevya ni wa msingi wa sababu ya kile nini sasa kinaitwa UKIMWI ina uwezekano zaidi ya kuwa ya kweli kuliko dhana iliyofilisika isemayo UKIMWI unasababishwa na kirusi. – Sunday Times, London Aprili 3, 1994
•Dk Steven Jonas, Profesa wa Tiba za Kuzuia (Preventive Medicine), Suny Stony Brook, NY, anasema:
“Ushahidi unajikusanya kwa kasi kwamba nadharia ya awali ya V.V.U siyo sahihi. – Sunday Times London Aprili 3, 1994
•Dr Lawrence Bradford, Professa wa Biolojia, Atchinson Kansas, anasema:
“UKIMWI ni ugonjwa wa sababu mtambuka (multifactorial disease). V.V.U havihusiki, havina umuhimu wa kutosha kuhusianishwa’’. – Sunday Times London, Aprili 3, 1994
•Neville Hodgkinson, Mhariri wa zamani wa jarida la sayansi (Former Science Editor), The Times of London, anasema:
“Aina ya mkusanyiko wa ukichaa wa pamoja juu ya V.V.U na UKIMWI umeathiri viongozi wa taaluma ya sayansi na matibabu. Wameacha tabia za kiuanasayansi, badala yake wamekuwa kama watu wa propaganda za kisiasa, Wakijaribu mno kuiweka hai nadharia iliyofeli”.
•Dr Beverly Griffin, Mkurugenzi wa Idara ya Virusi (Virology), Royal Postgraduate Medical School, Hammersmith Hospital London, anasema:
“Itapelekea kwa hakika jamii yenye afya njema kisayansi kama mzigo wa kuthibitisha V.V.U kama adui anayeleta mauti utarudishwa kwa wamiliki wake – Wale wote wanaoshikilia kwamba VVU husababisha UKIMWI – na wengine waruhusiwe kutumia njia mbadala katika vita ya kujinasua na ugonjwa huo – Nature Aprili 20, 1989’’.
•Dr Etienne de Harven, Profesa wa Magonjwa, Chuo Kikuu cha Toronto, anasema:
“Inaongozwa na vyombo vya habari, na makundi ya shinikizo na kwa maslahi ya viwanda vya madawa, waanzilishi wa UKIMWI wamepoteza mawasiliano na sayansi inayosema ukweli/yenye kudadisi na uthibitisho wa pamoja (peer review science) tangu dhana isiyothibitika ya VVU / UKIMWI ilipoanza kupokea asilimia 100% ya fedha za utafiti huku nadharia tofauti zingine zote zikipuuzwa. Ni nguvu kiasi imepotezwa, ni mabilioni mangapi ya dola ya tafiti kuhusu UKIMWI yamepotea bure…inatisha”.
Hawa ni baadhi tu ya wanasayansi na madaktari kati ya wengi ambao wamekuwa tayari kuiweka wazi misimamo yao juu ya dhana hiyo ya uongo kuhusu V.V.U/UKIMWI.
Vipi kuhusu vipimo vya UKIMWI, je tuviamini?
Vipimo vya UKIMWI vimetengenezwa katika mtindo ule katika lugha ya kikoloni huitwa ‘trial & error’ kwa maana ya kwamba havina uhakika wa jibu vitakalolitoa, vinaweza kutoa jibu la positive (una UKIMWI) na muda mchache baadaye vikatoa jibu la negative (hauna UKIMWI), ili kuthibitisha hili jaribu kupima UKIMWI katika vituo tofauti tofauti kama vitano hivi halafu utaniambia kama umepata majibu yanayofanana.
Hii ndiyo sababu kumetokea katika ndoa mme kukutwa ameambukizwa na mke hajambukizwa au mke ameambukizwa na mme hajaambukizwa huku wakiwa wameshirikiana tendo la ndoa mara kadhaa! Kwahiyo majibu yeyote ya vipimo vya UKIMWI yawe ni positive au negative hayana uhusiano wowote na afya ya mwili wako.
Ni nini hasa ambacho huleta Upungufu wa Kinga Mwilini?
Ni ukweli uliowazi kwamba watu wanaugua na wanakufa maelfu kwa maelfu. Je baada ya kuona namna VVU/HIV visivyohusika na janga hili ni nini hasa kinapelekea vifo hivi vyote vitokanavyo na UKIMWI?.
Zifuatazo ni sababu za kweli za kushuka au kupungua kwa kinga ya mwili mwilini:
- Madawa ya hospitalini – Madawa karibu yote ya hospitalini huwa na madhara ya aina mbili, yani madhara chanya (ya kuponya) na madhara hasi (ya kudhuru), madhara haya hasi kwa kawaida lazima kwa namna moja ama nyingine huishusha nguvu kinga yetu ya mwili katika kupigana na maradhi mbalimbali.
- Maambukizi ya kujirudiarudia (repeated infections) – Kuna watu haiwezi kupita mwezi au miezi miwili bila kuugua, sasa inapotokea unakuwa mtu wa kuuguaugua kila mara hata kama ni malaria au taifodi tu basi huko kuuguaugua kila mara lazima kwa namna moja au nyingine kutapelekea kushuka kwa kinga ya mwili.
- Madawa ya kulevya – Sidhani kama inahitajika kuelezea namna madawa ya kulevya yanavyoathiri kinga ya mwili, namna pekee ni wewe kuacha kuyatumia, basi. Hii ndiyo sababu ya UKIMWI katika nchi zilizoendelea hasa Marekani, Ulaya na Afrika ya Kusini kwa hapa Afrika.
- Chanjo mbalimbali za magonjwa – Huku Afrika bado kuna chanjo nyingi zinaendelea kutolewa kwa watoto na mama wajawazito, baadhi ya hizi chanjo zimesemwa huharibu kinga yetu ya mwili kwa taratibu kadri siku zinavyoenda hivyo kutuua taratibu, wenyewe wazungu huziita ‘silent killer’ yaani muuwaji wa taratibu.
- Mfadhaiko/stress – Hapa ndiyo penyewe. Mfadhaiko au stress unachangia kushuka kwa kinga ya mwili kwa karibu ya asilimia 90, inasemwa kuna zaidi ya magonjwa 50 ambayo hutokea mwilini kwa sababu tu ya mwili kuwa katika hali ya mfadhaiko kwa muda mrefu. Ni kweli ulio wazi kuwa ukitaka kukonda basi uwe na mawazo. Sasa hebu fikiri umejiona unauguaugua kila mara tayari unaanza kujihisi huenda utakuwa na UKIMWI, unaamua kwenda kupima na unaambiwa una UKIMWI na huku unajuwa wazi kuwa UKIMWI hauna dawa, kwakweli mfadhaiko utakaoupata kama ni mtu mwenye roho nyepesi basi lazima kweli utaugua UKIMWI. Kwahiyo ni mhimu sana kwa kila mmoja wetu kudhibiti hali ya kuwa na mawazo mawazo kichwani kwa muda mrefu.
- Pombe, tumbaku – Pombe tumeshaambiwa tayari kuwa ‘kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako na tafadhali kunywa kistaarabu’, kadharika tumbaku, bangi na sigara siku nyingi tumejulishwa kuwa ni hatari kwa afya zetu.
- Lishe duni – Hapa inatugusa zaidi sisi watu wa bara la Afrika na hii ndiyo sababu kwanini wagonjwa wengi wa UKIMWI wapo zaidi Afrika na si kwingineko duniani. Inasemwa asilimia 60 ya wagonjwa wote wa UKIMWI duniani wanapatikana Afrika kusini mwa jangwa la sahara, hii inamaanisha kwa kila wagonjwa kumi wa UKIMWI duniani wagonjwa sita wanapatikana Afrika kusini mwa sahara, hivyo basi wagonjwa wengine wanne waliobaki katika kumi mmoja anaweza kuwa yupo Ulaya, mwingine akawa Amerika ya kusini, mwingine akawa Amerika ya kaskazini na mwingine wa nne akawa bara la Asia. Tujiulize kwanini hapa Afrika kusini mwa sahara wawepo wagonjwa wengi hivyo wa UKIMWI? Jibu ni kuwa umasikini uliokithiri katika eneo hili la dunia ndiyo sababu ya lishe duni, lishe ya mlo mmoja au miwili kwa siku tena bila hata kushiba, maji yasiyo safi na salama na makazi yasiyo salama kwa matumizi ya binadamu.
- Lishe isiyo sahihi – Maendeleo katika viwanda yameleta aina mpya ya vyakula na ulaji ambao umepelekea magonjwa yasiyoambukiza kujitokeza kwa wingi miaka ya karibuni, magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu, uzito na unene kupita kiasi ni matokeo ya hayo yote. Vyakula vingi vya kisasa vinatengenezwa vikiwa vitamu zaidi na wakati mwingine vinakuwa havina lishe ile mhimu ambayo mwili unaihitaji zaidi ya kuwa na utamu uliozidi kwa ajili ya kujaza tumbo tu na kujaza sumu mwilini kila kukicha. Watu wameacha kula ugali wa dona na badala yake wamehamia kula ugali wa sembe ambao ni ugali mweupe usio na lishe yeyote ndani yake zaidi ya kujaza tu tumbo, watu wanakunywa zaidi vinywaji baridi vya viwandani, chai ya rangi na kahawa kuliko maji. Lishe nyingine mhimu iliyosahaulika miongoni mwa watu wengi ni Mazoezi; Mazoezi ni mhimu sana katika kuuweka mwili katika hali ya afya nzuri, huwezi kuwa na afya nzuri kwa kula na kunywa vizuri tu bila kujishughulisha na mazoezi na hii ndiyo sababu wagonjwa wa UKIMWI hushauriwa kupenda kufanya mazoezi ili kuongeza nguvu ya mwili na kinga yao. Kwa hakika utaona kuwa yale maisha anayoshauriwa mtu mwenye UKIMWI kuyaishi ndiyo yale yale kila mtu mpenda afya anavyotakiwa kuyaishi kila siku.
- Uzinzi – Uzinzi ni hali ya mtu kupenda kushiriki tendo la ndoa mara nyingi zaidi na wakati mwigine na wapenzi wengi zaidi, kuishi hivyo ni kujiweka karibu na magonjwa mengine ya zinaa jambo litakalopelekea kushuka kwa kingi ya mwili au kushuka tu kwa kinga ya mwili kutokana na kuwa mchovu kutokana na kufanya kazi hiyo kila siku. Wagonjwa wa UKIMWI hushauriwa kupunguza au kuwa na kiasi katika kushiriki tendo la ndoa na wanaofuata ushauri huo hubaki na afya nzuri kwa muda mrefu. Hivyo utaona katazo la Mungu la kutoikaribia zinaa ni la haki na kweli kwa ustawi wa maisha yetu. Wapo baadhi ya waathirika ambao kisha kupimwa na kugundulika wameathirika huathirika kisaikolojia na kutaka kulipiza kisasi cha kuambukizwa UKIMWI kwa kutembea na watu wengine wengi kwa kujifariji kuwa atakufa au na yeye awaambukize wengine, matokeo yake ni afya zao hudhoofika mapema kutokana na kukata tamaa huko. Kwa kupinga kuwa V.V.U havileti UKIMWI au kupona UKIMWI si tiketi au ruhusa kwa wewe kupenda uzinzi kuliko hata Elimu au kazi tena pasipo hata kumuogopa Mungu, hilo ulielewe kuanzia sasa. Utukufu ni wa Mungu.
No comments:
Post a Comment