Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,na
Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii
ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Mh. Aggrey
Mwanri, akiendesha shughuli za mkutano huo uliomalizika hivi karibuni
katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC).
MTAALAMU
mmoja wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, ameishauri
serikali kutumia neema ya gesi kutoa hifadhi ya kutosha kwa wananchi
wake.
Dhliwayo
alisema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu waziri Afya na Ustawi wa
jamii, Dk Kebwe S. Kebwe namna ya kufikia lengo la hifadhi ya jamii kwa
wote kwa kasi kuliko ilivyo sasa ambapo inafikiriwa ifikapo mwaka 2025
ndio tutakuwa tumefikia asilimia 75 ya hifadhi ya jamii.
Dk.
Kebwe alisema hayo wakati wa kujadili mada ya uchokozi iliyotolewa na
Dhliwayo mtaalamu wa uchumi ambaye alishawahi kufanyakazi nchini
Zimbabwe na Msumbiji.
Alisema kwamba mataifa mengi yametumia raslimali zao kufanya mambo makubwa kwa wananchi wao na Tanzania inaweza kufanya hivyo.
Ofisa
anayeshughulikia sera za hifadhi, UNICEF Tanzania, Bi. Usha Mishra
akitoa mrejesho walichojifunza washiriki siku ya kwanza na kutoa
mwongozo wa mambo mapya wanayotakiwa kujifunza katika mkutano
uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.
Alisema
ipo nchi ambayo ilitumia utajiri wake wa almasi kutengeneza miundombinu
ya barabara na si vibaya kwa Tanzania kutumia utajiri wake wa gesi
kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii. Alisema kama taifa
linaweza kuamua asilimia Fulani kutoka katika sekta ya gesi kuingia
katika kuwezesha hifadhi ya jamii ambayo itahakikisha uwapo wa huduma
sawa kwa wote.
Alisema
uchumi wa Tanzania kutoka mwaka 2000 hadi sasa umekuwa ukikua kwa kasi
ingawa kasi hiyo haionekani kwa wananchi ambapo wengi wamejikuta wakiwa
katika umaskini wa kukithiri. Alisema kutokana na tatizo hilo la
umaskini wa kukithiri kutoondoka kwa hali hiyo kunasababisha na sekta
husika kutotoa ajira za kutosha ambazo zingewezesha watu kuneemeka na
uchumi unaokua kwa kasi.
Mtaalamu
wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa mada chokonozi
wakati wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa
na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ambao umemalizika hivi
karibuni jijini Arusha.
Alisema
aidha kaya nyingi zimekuwa na idadi kubwa ya watu ikiakisi umaskini
unaoambatana na kaya zenye watu wengi na uzazi wa mapema unaowakuta
wasichana.
Alisema
pamoja na mpango mzuri wa serikali kupitia TASAF kupunguza umaskini wa
kukithiri ukishirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ipo haja kwa
serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu unawezesha mipango ya
kupunguza umaskini inafanikiwa.
Alisema
iwapo TASAF inashughulikia elimu na afya ni dhahiri itahitaji kuwapo
kwa shule na walimu na katika afya hospitali na wauguzi na madaktari na
dawa.” Ni lazima kuwepo na uratibu ili kufanikisha yote yaliyolengwa”
alisema Dhliwayo. Alisema Tanzania inaweza kujifunza kutoka mataifa ya
Rwanda na Eritrea ambayo yamefanikiwa hifadhi ya jamii eneo la afya
kufikia zaidi ya asilimia 90 huku wakitumia mifumo thabiti ya afya ya
jamii kwa kaya.
Kuki Tarimo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akitoa mada chonokonozi wakati wa mkutano huo.
Aidha
amesema kwamba mataifa hayo yamefanikiwa katika malengo ya millennia na
kupunguza idadi ya vifo vya wanawake katika uzazi. Katika mkutano huo
ambao uliitishwa na serikali ili kupata misingi ya utengenezaji wa sera
na sheria ili kuwezesha watanzania wote kuwa na haki katika kei ya taifa
kw akuwezeshwa kuondokana na umaskini wa kukithiri ulihudhuriwa na
watalaamu 150 kutoka nchi mbalimbali duniani.
Pia
ulifunguliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi
ambaye alisema Tanzania kwa sasa inapojianda kuwa na uchumi wa kipato
cha kati ipo haja ya kuimarisha sekta za hifadhi ya jamii.
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao
makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster akichangia hoja wakati wa mkutano
huo uliomalizika hivi karibuni.
Meneja Mwendeshaji wa Shirika la Under The Same Sun, Gamariel Mboya
akiuliza swali kuhusiana na serikali imejipangaje katika kuhakikisha
watu wenye ulemavu wa ngozi wanapataje mafuta ya kuzuia mionzi ya jua
inayopelekea ugonjwa kansa ya ngozi.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe, akijibu swali
kuhusiana na serikali imefanya nini kwa walemavu wa ngozi katika
kuhakikisha mafuta kuzuia mionzi ya jua kwa watu hao yanapatikana
kiurahisi ili kupunguza athari za kansa kwa walemavu hao. Kulia ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
Mwakilishi
wa wazee waliostaafu akiuliza swali kwa Wizara ya afya na ustawi wa
jamii kuhusiana na uboreshwaji wa huduma za afya kwa wazee ambapo
imekuwa changamoto kubwa kwao.
Ujumbe wa Makatibu wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ukishiriki wa mkutano huo.
Mtaalamu wa mawasiliano wa Shirika la UNICEF Tanzania, Jacqueline Namfua akifurahi jambo wakati wa mkutano huo.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, watengeneza
sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya
Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini,
Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania uliomalizika
hivi karibuni jijini Arusha.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
akifuatilia kwa umakini maoni mbalimbali yaliyokuwa yakiwasishwa kwenye
mkutano.
No comments:
Post a Comment