Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Humphrey Kisika (32)
Katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu
afisa habari na mahusiano wilaya ya Iringa Hafley Kisika ametangaza
kugombea ubunge katika jimbo la Mbinga mashariki kupitia tiketi ya
chama cha mapinduzi CCM, ili kuleta maendeleo katika jimbo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari KISIKA amesema kuwa sababu
inayompelekea kugombea ubunge katika jimbo hilo ni pamoja na kuleta
siasa safi pia kuunganisha wananchi na wataalamu mbali mbalimbali ili
kusaidia jimbo hilo kuendelea hasa katika maswala ya miundombinu.
Aidha amesema kuwa chama cha mapinduzi kina sera nzuri na kwamba
ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ikiwamo vijana,wazee na makundi
mengine katika jamii kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua jimbo la
Mbinga mashariki kimaendeleo.
KISIKA amekanusha uvumi unaodai chama cha mapinduzi kimepoteza dira na kuongeza kuwa Ccm ni chama imara na kuwataka vijana watambue
wanafanya nini na kuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko ya
kimaendeleo na sio kuleta machafuko.
Ameendelea kusema kuwa pamoja na kuwa na ushindani mkubwa katika siasa lakini ilani na sera za chama husika pamoja na mgombea ndizo ambazo
zinaweza kumtambulisha mtu kama anauwezo wa kuwa kiongozi.
Hata hivyo KISIKA anatarajia kugombea ubunge katika jimbo la Mbinga
mashariki huku akiwa ni mjumbe wa chama cha mapinduzi katika chuo
kikuu cha Tumaini,Mbunge kwa miaka mitatu pamoja na katibu katika
kamati mbalimbali chuo kikuu cha Tumaini mbali na hayo KISIKA ni afisa
habari katika halmashauri ya wilaya ya Iringa.
KWA vyovyote iwavyo, mapigo ya moyo ya Mbunge wa Jimbo la Mbinga
Mshariki mkoani Ruvuma, Gaudance Kayombo yataongezeka mara dufu baada ya kijana msomi; Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
Humphrey Kisika (32) kutangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo
katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Kisika, msomi mwenye shahada ya kwanza ya uandishi wa habari ambaye
pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, anayesoma shahada ya pili
ya uandishi wa habari na utawala anataka kuwania nafasi hiyo kupitia
chama chake Chama cha Mapinduzi (CCM).

No comments:
Post a Comment