Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
20 January, 2015
DAKTARI ALIYECHAPWA NA WAGONJWA ASEMA ATAUA MWANDISHI WA HABARI
Pichani ni Daktari wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat Msafiri akipata kichapo baada ya kukutwa akilewa muda wa kazi-picha kutoka maktaba Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoa wa Geita Jackline Masinde,ametishiwa kuuawa na Daktari wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat Msafiri. Inaelezwa kuwa tarehe 23 Desemba mwaka jana Mwandishi huyo aliripoti taarifa za Daktari huyo kuwafungia nje wagonjwa kisha kwenda kulewa pombe na kuacha wagonjwa wakiwa wamezidiwa katika kituo alichokuwa akifanyia kazi cha Nyakabale hapo awali . Hali hiyo ilisababisha wagonjwa kumfuata baa alikokuwa akilewa pombe kisha kumwadhibu kwa viboko ,ambapo taarifa hiyo ilisababisha daktari kuvuliwa madaraka yake kisha kuhamishwa kituo chake cha kazi na kupelekwa kituo cha Nyankumbu na mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Magreth Nakainga. Mwandishi huyo alisema juzi majira ya saa 5:23 asubuhi alimpigia Daktari huyo ikiwa nimoja wa wajibu wake wa kazi akihitaji taarifa za kitaalam kuhusu madhara ya sumu ya Zebaki ofisini kwake . “Nilimpigia simu daktari nikihitaji taarifa za madhara ya sumu ya Zebaki ,alipokea simu na kuanza kunitolea lugha za matusi (tunazihifadhi kwa sababu ya maadili) huku akinitishia kuniua kwa kusema "nikionana nawewe sehemu yoyote haki ya mungu nakuua”,alimnukuu Daktari huyo. Alisema alipomuhoji kwanini anamtishia kumuua,daktari huyo alisema ana uchungu na taarifa alizozitangaza nchi nzima kuhusu yeye kupigwa na wagonjwa ,kuwa imemuathiri katika maisha yake. Mwandishi huyo alisema kuwa kauli hiyo ya Daktari ilimpa mashaka kisha kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Geita mkoani humo na kufungua kesi namba GE/RB/366/2015 ya kutishiwa kuuawa kwa njia ya mtandao. "Niliamua kutoa taarifa polisi na mtuhumiwa mpaka sasa amekamatwa ,alipohojiwa alikiri kufanya kosa na kuomba msamaha mbele ya polisi"alisema Masinde. Mwandishi huyo wa habari sasa yuko katika wakati mgumu kutokana na kufichua maovu mengi katika jamii na amekuwa akipata vitisho mbalimbali kutoka kwa baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakimtishia kumpeleka mahakamani kwa kile kinachoelezwa kuwa anawaandika vibaya,huku pia akinusurika kupigwa na kuharibiwa vifaa vyake vya kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Josephine is passionate, dedicated, reliable, responsible, and hardworking. Team worker and able to face all challenging situations. Can ...
No comments:
Post a Comment