16 January, 2015

DUBAI INATISHA KWA UAMINIFU


                                                Mavumba yaliyokuwemo hayakuguswa 


Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa  pochi iliyoangushwa mtaani,na mara ikarejeshwa kwa mhusika mara moja.   Katika utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili ya Uingereza  katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa  makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi  hiyo kwa mmiliki wake. Daniel Jarvis, mwenye miaka 26,akiwa ameificha kamera yake na kurekodi  mfululizo wa matukio hayo ya makusudi akiwa pamoja na rafikiye  aliyejipachika jina la utani la 'Digi' ama Dan, mwenye miaka 25,  walibarizi katika viunga vya Downtown na Bur vilivyoko Dubai,siku za  karibuni na kuweka swali je unaweza kuiba Dubai? Kutaka kuichunguza  jamii na kurushwa vipande vyake katika YouTube ambapo mpaka kufikia jana  usiku watazamaji walikuwa ni zaidi ya 70,000 . Jarvis aliiambia 7DAYS walishangazwa na utafiti huo na kikubwa  kilichowasangaza ni kwamba waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha  kutazama ndani kuna nini? Wakati pochi hiyo ilikuwa imesheni euro za  kutosha na fedha ya Falme za Kiarab dirham kadhaa. Mtaa wa kwanza walioufanyia majaribio ni mtaa uliko katika barabra ya  Sheikh Zayed karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara  wa Emirates lakini kila aliyeiona pochi hiyo aliirejesha,lakini baadaye  tukafikiri sababu ya kurejeshwa pochi hiyo kuwa walioko eneo hilo ni  matajiri. Basi utafiti wetu tukauhamishia eneo la Bur ,Dubai, mahali ambapo  palionekana duni kidogo cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa  kurejesha pochi kama ilivyo, na hali eliendelea hivyo mara kadhaa. Jarvis anasema wameshafanya utafiti kama huo katika mji wa London nchini  Uingereza. Na huko walistaajabu walipoidondosha tu aliyeiokota alianza  kukimbia nayo wa nako hakuna aliyethubutu kuichukua pochi hiyo. Jarvis, alivalia suti nadhifu na kuigiza kudondosha pochi anaonekana  kwenye video hiyo anaeleza hisia za kurejeshewa kitu ulichondondosha  kuwa ni raha iliyoje .lakini akaendelea kusema kuwa anadhani vyombo vya  habari hupotosha ukweli,kwakuwa kulikuwa na kichwa cha habari kuwa kuna  mtu alihukumiwa miaka 15 jela kwa kuiba mdoli wenye taswira ya dubu,  utafiti wetu umegundua tofauti na wayasemayo. Trollstation ina wanachama wapatao 230,000 na utafiti wao kutoka Falme  za Kiarab unaelekezwa Ulaya, Marekani na hatimaye Afrika . Inawezekana katika maeneo watakayopita kuvunja rekodi ya Dubai tusubiri  wakati uwadie, ni kauli yake Jarvis

VIA-BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...