16 January, 2015

MAGAZETI YA AFRIKA YAOMBA RADHI

                                       Gazeti la The Star lina ushawishi Kenya

Magazeti mawili ya Afrika yameomba radhi kwa kuchapisha ukurasa wa juu wa jarida la  Charlie Hebdo likiwa na kibonzo cha Mtume Muhammad, baada ya wasomaji wa Kiislamu kulalamika.

Gazeti la Kenya The Star na The Citizen la Afrika kusini yamesema yanajuta kwa kuwakosea Waislamu.  

Chombo cha kudhibiti vyombo vya habari Kenya kimemwita shaurini mmiliki wa gazeti la Star baada ya kulishutumu kukiuka sheria ya kuheshimiana. 

Nchini Senegal, serikali imepiga marufuku usambazaji wa jarida hilo la Charlie Hebdo. 

Gazeti la pili la Kenya, Business Daily, nalo limechapisha ukurasa huo wa mbele wa jarida hilo la Ufaransa.

Katika toleo lake la Alhamis asubuhi, The Star lilisema wasomaji wengi wa Kiislamu wamelalamika juu ya “uzalishaji mdogo” wa ukurasa wa mbele wa Charlie Hebdo siku ya Jumatano.  

Wakiomba radhi, gazeti hilo, la tatu kwa ukubwa Kenya, limesema “linajuta sana kwa kosa na uchungu uliosababishwa na picha hiyo”.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...