18 January, 2015

MAKANISA YACHOMWA!

                   Maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed nchini Niger

Ripoti kutoka Niger zinasema kuwa makanisa matatu yamechomwa katika mji mkuu wa Niamey katika siku ya pili ya maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa na gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo. Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange. Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwao
                                                  Waandamanaji wachoma makanisa Niger

Polisi wa kukabiliana na ghasia kwa sasa wameweka ulinzi mkali katika kanisa la Cathedral mjini humo ambapo makundi ya vijana wanaowarushia mawe. Siku ya ijumaa watu wanne walifariki huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya waandamanaji kuyapekua makanisa matatu kabla ya kuyachoma mbali na kukichoma kituo kimoja kilicho na utamaduni wa Ufaransa huko Zinder.


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...