20 January, 2015

NCHI ZA UMOJA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI( EAC) KUTUMIA SIMU MOJA IFIKAPO JULAI!

NCHI za Umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zitaanza kutumia mtandao mmoja wa simu za mkononi Julai mwaka huu hali ambayo itasaidia kurahisisha huduma za mawasiliano katika nchi hizo. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Dk , Enock Bukuku wakati akizindua mfumo wa malipo kwa nchi za EAC kwa kutumia kadi ya Umoja iliyofanyika mjini hapa. Alisema hivi sasa wamekuwa wakitumia mitandao tofauti ya simu kwa kila nchi ambapo mchakato wa kuwepo kwa mtandao mmoja wa simu kwa nchi za EAC itarahisisha huduma za mawasiliano. Aliongeza pamoja na nchi hizo kutumia mtandao mmoja wa simu, pia wataweza kutumia kadi za Umoja kwa kupata huduma za kibenki katika nchi zote za EAC katika benki ambazo zimeunganishwa na mfumo wa Umoja Switch. Alisema mteja yeyote mwenye kadi ya Umoja ataweza kupata huduma za kibenki kwa benki yoyote katika nchi hizo za EAC na kuepuka usumbufu wa kuwa na kadi nyingi. Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mitandao ya Umoja, Danford Mbilinyi alisema walianza na benki sita zilizoanza kutumia huduma ya Umoja Switch ambapo hadi sasa hivi zimefikia benki 27 huku wakianza na ATM za Umoja 30 hadi kufikia 2,000 katika nchi za EAC.

A

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...