15 January, 2015

WAJUMBE WA ARSENAL KUTUA TANZANIA

             Balozi Peter Kallaghe, akiwa na maafisa wa masoko wa Arsenal. 

Klabu ya Arsenal imepanga kutuma maofisa biashara wake jijini Dar es  Salaam, Tanzania kwa ajili ya kujadili fursa za ushirikiano na  wafanyabiashara kadhaa wakubwa nchini Tanzania. Huu utakuwa ujumbe wa kwanza kabisa wa Arsenal nchini Tanzania, ambapo  klabu hii kubwa ya England inataka kujenga ushirika mkubwa kabisa katika  maeneo ya masoko na chapa zake, ili kutanua mafanikio yaliyofikiwa  kwenye nchi nyingine za Afrika kama Kenya, Uganda na Nigeria.   Washika Bunduki hao wa London wanataka kutoa fursa kwa benki za Tanzania  pamoja na kampuni za simu na taasisi nyingine kuweza kupata rasilimali  zihusianazo na Arsenal, kama vile bidhaa zilizosainiwa kwa majina ya  wachezaji, tiketi za mechi. Safari hii kwa kiasi kikubwa imefanikishwa na Ubalozi wa Tanzania katika  Uingereza, Kupitia kwa Mhe Balozi Peter Kallaghe, ambaye binafsi  ameshiriki kuwaarifu maafisa hao, mazingira ya nyumbani, na ukuaji wa  sekta za binafsi katika kukuza uchumi wa Tanzania. Arsenal wanasema kwamba wanaweza kuwapatia washirika wao hao uwanja  mpana wa masoko kwa ajili ya kuwasaidia kutimiza malengo mbalimbali ya  kibiashara. Ofisa Biashara Mkuu wa Arsenal, Vinai Venkatesham amesema kwamba  wameichagua Tanzania kwa sababu wana washabiki wengi, na kwa  kushirikiana na taasisi za Tanzania, watakuwa karibu zaidi na washabiki  wao kuliko ilivyokuwa awali. “Katika bara lenye nchi zaidi ya 50, tumechagua kuzuru Tanzania  kimkakati kwa sababu tunaiamini nchi hiyo. Arsenal ina mamilioni ya  Watanzania ambao ni washabiki waaminifu na wenye mapenzi makubwa nayo. “Kwa kushirikiana na taasisi za huko, tutaweza kuisogeza klabu karibu  zaidi na washabiki hao kuliko ilivyokuwa awali, huku tukizipatia taasisi  husika fursa pekee za kuifikia klabu yetu,” akasema Venkatesham. Wajumbe hao wa jopo la Maendeleo ya Ushirikiano ya Arsenal wanatarajia  kuwasili nchini Tanzania Januari 18 mwaka huu, ambapo watakaa kwa wiki  moja jijini Dar es Salaam, kuitisha mikutano kadhaa ya awali ya  kibiaashara na kuzindua rasmi mchakato wa kutafuta washirika wa kwanza  kabisa nchini Tanzania.


Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...