16 January, 2015

ULIYAJUA! KUWA FIDEL CASTRO NI MTOTO WA HOUSIGEL!

Aliyekuwa Rais wa Cuba  kwa takriban miongo minne, Fidel Alejandro Castro Ruz maarufu kama Fidel  Castro. Ni Rais anayependwa zaidi na wanaharakati za kimapinduzi.  Moja ya vitu vinavyompa sifa katika ulimwengu huu ni ujasiri wake wa  kutoafikiana na Taifa kubwa duniani, Marekani kiasi cha kuandamwa na  kutengenezewa mitego au majaribio mbalimbali ya kumwangamiza pasipo  mafanikio. Miongoni mwa vitu vingi ambavyo havijulikani miongoni mwa wengi ni  historia yake. Huyu jamaa alizaliwa nje ya ndoa. Ni ‘mwanaharamu’  halisi, kama unaweza kumuita hivyo kwa lugha sanifu ya Kiswahili. Baba yake Castro aliyejulikana kama Angel Castro ArgĂ­z alikuwa ni  Mhispania aliyehamia Cuba wakati wa harakati za uhuru wa nchi hiyo  katika kipindi kati ya mwaka 1895 na 1898. Mkewe ni Maria Luisa Argota. Angel alikuwa ni mkulima wa miwa wa kipato cha kati aliyeishi katika  Kitongoji cha Biran, mashariki mwa nchi hiyo pamoja na familia yake  iliyokuwa na kijakazi aliyeitwa Lina Ruz Gonzalez. Kijakazi huyo alikuja kughilibiwa na Angel kuwa na uhusiano wa kimapenzi  na ndiyo uliyosababisha kuzaliwa kwa Castro. Katika muda wote wa ndoa ya Angel na Maria hawakufanikiwa kupata mtoto  mpaka Agosti 13, 1926 baba huyo alipompa ujauzito binti huyo wa kazi za  ndani (housegirl). Baada ya kuzaliwa kwa Castro, Angel alilazimika kuivunja ndoa yake na  Maria na kuamua kuishi na Lina ambaye alizaa nae watoto watano. Castro alionekana kuwa na akili nyingi huku akiwika katika michezo hasa  ule wa magongo. Kutokana na uelewa wa haraka aliokuwa nao tangu akiwa  shule ya msingi, alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Havana. Akiwa hapo alivutiwa na siasa hivyo kujiunga na chama cha Orthodox,  kilichokuwa kinapinga masuala ya ufisadi serikalini. Mara tu alipohitimu, mwaka 1950 alifanyakazi ya uwakili akivutiwa zaidi  za kesi za kisiasa. Kutokana na mapenzi yake katika siasa, alikuwa ni mgombea wa ubunge  katika Uchaguzi Mkuu uliotarajiwa kufanyika Juni, 1952. Lakini kabla uchaguzi huo haujafanyika, yalitokea mapinduzi ya kijeshi  yaliyoongozwa na Generali Fulgencio Batista na kuzima ndoto za Castro  kuwatumikia wananchi kwa njia za kidemokrasia. Castro hakukubaliana na mapinduzi hayo na tangu mwanzo alikuwa miongoni  mwa walioupinga utawala wa Batista na mara kadhaaa alijaribu kutumia  sheria pasipo mafanikio.


No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...