17 January, 2015

YOU ARE PROBABLY RICHER THAN YAHOO! BUT YOU DON'T KNOW.. INAWEZEKANA WEWE NI TAJIRI KULIKO YAHOO LAKINI HUJAJUA.. YOU ARE PROBABLY RICHER THAN YAHOO! BUT YOU DON'T KNOW.. INAWEZEKANA WEWE NI TAJIRI KULIKO YAHOO LAKINI HUJAJUA


Ngoja niongee tena na waajiriwa leo.. Je, unawafahamu hawa jamaa wawili kwenye hii picha? Ungeokota picha hii barabarani ungeweza kudhania ni kina nani? Huenda ungefikiri ni watu tu kama wewe sema tu huwajui kama wao wasivyokujua. Au siyo? And you would be right! Lakini pengine ungekuwa hujui kuwa hawa jamaa wawili wana influence juu ya maisha yako pengine ya kila siku sasa hivi! Ladieees and Gentlemen, my honour to introduce to you ndugu BRIAN ACTON hapo kushoto and ndugu JAN KOUM hapo kulia.. Do these names ring the bell? No? Ok. Hawa ndiyo waanzilishi wa 'mtandao' wa WatsApp miaka takribani 6 tu iliyopita in 2009! Na sasa ni mabilionea. In just 6 years. Akili ya mwanadamu yeyote Mungu aliiumba kwa "akili" sana yaani! Sema tu akili zingine zinaamuaga kuchungulia upande wa pili kukoje na zingine zinaamua kubakia hivyo hivyo ndani ya "fence". Ukitaka ujue akili yako iko katika kundi lipi basi upate matatizo ndo kipimo cha kujua unawazawazaje! Kama wewe una comfortable life toka utotoni yaani ukikohoa tu dakika sifuri mko Agakhan kuchek afya hebu sasa jaribu kujipa matatizo angalau madogo madogo.. kama kwenda sehemu bila nauli ya kurudia uone wewe unawazaje kichwani. Utaweza kurudi? Utapata option ngapi za kusolve ishu ya nauli ya daladala kwa mfano. Wengine watasema huo ni uchizi. Hahaaaa. Basi sawa. Sasa bana hawa jamaa wamesoma kiasi kama wewe labda, umewazidi usikute. Hawa jamaa walikuwa waajiriwa kama wewe. Waliajiriwa na kampuni moja maarufu kweli kweli siyo tu huko kwao bali dunia nzima. Yahoo! Kuna mtu anayesoma hapa hajui Yahoo! ? Huyo mrefu kabla ya Yahoo alifanya kazi pia Ernst & Young! So.. Walipiga kazi hapo Yahoo! kwa takribani miaka 10! Mwenye Yahoo alikuwa bilionea wao walikuwa wafanyakazi wa bilionea. Kumbe hawakujua kuwa wao nao walikuwa ni mabilionea tena zaidi ya bilionea aliyekuwa kawaajiri. Siku walipojitambua wakaacha kazi Yahoo! Unajua kuacha kazi Yahoo inahitaji uvute pumzi kwenye mapafu mara tatu tatu. Au nakosea. Nadhani kuacha kazi "Juakali Enterprises" ni rahisi kuliko kuacha kazi Yahoo. Imagine kama hapo ulipo tu sasa hivi kuacha kazi haijawahi kukujia akilini je ungekuwa Yahoo? Jamaa wakaacha. Cousin yangu Haruni Leonard huwa anasema waliQUIT!! Hahaaa, dogo bana. Yeah. Tena waliacha kwa kuanza na likizo ya mwaka mzima ili wasafiri kuiona dunia ya Mungu. Kufumba na kufumbua hao wakaibuka na kitu cha WATSAPP mwaka 2009. Tena ilianza kama free app then ndo wakaweka tozo kidogo ili kucontrol ukuaji wa kutisha wa WatsApp!! Boooy! Hivi Unajua ndo maana wengine Mungu huwa sometimes anachafua hali ya hewa kazini kwako ili utoke ukawe tajiri huko nje. Wewe kesho yake unaanza maombi ya kufunga na kuhamishwa bosi. Wanasema Mungu si "Asumani". Wiki haifiki bosi kahamishwa. Unapeleka ushuhuda kanisani bila kujua kule mawinguni Mungu anakuangaliaaaaa.. Halafu anakuacha kama ulivyo. Unabaki na utajiri mkubwa kichwani mwako umeufungia kwenye Yahoo yako. Iangalie Yahoo yako vizuri. Usijekuta kuna WasApp yako miaka miwili tu mbele yako. Hawa jamaa wakaanzisha WatsApp yao ikagrow then mwaka jana tu FACEBOOK ikaamua kuwanunua kwa USD 19 BILLION. Si una calculator. Ni trilioni ngapi za bongo? Wangekuwa bado wako Yahoo je. Itazame upya Yahoo yako usikute inakufungia utajiri mkubwa tu. Sasa hivi ni board members wa Facebook. Na shares juu. Yaani hivi unavyosoma hii post hapa fb wao wanaingiza hela hivo. Cha ajabu walipoacha kazi Yahoo wakiwa likizo bado wanawaza wafanye nini hasa, waliapply kazi Facebook wakapigwa chini wote. Huyo Acton akaona isiwe tabu Facebook 'kitu gani' akaapply TWITTER nako akakosa! Dah. Unajua sometime ukiwa karibu "kutoka" kimaisha ndo vishawishi vya kurudi maisha yako ya zamani (mfano kuajiriwa) huwa vinashika kasi kweli kweli.. Wakati mwingine Mungu atakukosesha kazi nzuri qualifications unazo na experience unayo lakini unakosa kazi. Mungu anajua.. usilalamike tu ooh niliapply sehemu mbili nikakosa Mungu anataka utumie akili yako banaa.. Sasa Mfano wangepata kazi Facebook ingekuwaje? Wangekuwa na hisa za Facebook leo kweli? By mwezi wa nne mwaka jana (2014) WatsApp ilikuwa na Active Users milioni 500 kwa mwezi na kila siku kulikuwa na picha milioni 700 na video milioni 100 watu wanazoshare watsapp kila siku mpaka mwaka jana mwezi wa nne. Imagine mwezi wa nne mwaka huu itakuwaje? Watumiaji wa WatsApp kwa siku ilikuwa watu 833,000! (India ikiwa ndo inaongoza kwa kutumia WatsApp duniani). Mtu yuko Marekani hela zinatoka India na kila kona ya dunia. Wewe uko Magomeni hela hata ya Ubungo tu hupati. Mpaka uende hapo Yahoo ulipoajiriwa. Buni basi hata kitu tu cha ziada. Yahoo siyo mbaya wewe tu unaichukuliaje. Kwamba umefika au unapita? So my friend. Narudia tena, ingalie upya Yahoo yako. Miaka 10 bado upo hapo "Yahoo" umeufungia utajiri humo kwa mwajiri wako. Unazidi kuogopa kutoka. Tafakari vizuri. You are probably 5 times richer than your employer's worth. And 10 times richer in the next 10 years. But not if you will still be on that desk. Hakuna tajiri aliyeajiriwa. Ila kuna mabilionea lukuki bado wako "Yahoo"! Asante sana. ANDREA G. MUHOZYA DAR ES SALAAM, TANZANIA. Ngoja niongee tena na waajiriwa leo.. Je, unawafahamu hawa jamaa wawili kwenye hii picha? Ungeokota picha hii barabarani ungeweza kudhania ni kina nani? Huenda ungefikiri ni watu tu kama wewe sema tu huwajui kama wao wasivyokujua. Au siyo? And you would be right! Lakini pengine ungekuwa hujui kuwa hawa jamaa wawili wana influence juu ya maisha yako pengine ya kila siku sasa hivi! Ladieees and Gentlemen, my honour to introduce to you ndugu BRIAN ACTON hapo kushoto and ndugu JAN KOUM hapo kulia.. Do these names ring the bell? No? Ok. Hawa ndiyo waanzilishi wa 'mtandao' wa WatsApp miaka takribani 6 tu iliyopita in 2009! Na sasa ni mabilionea. In just 6 years. Akili ya mwanadamu yeyote Mungu aliiumba kwa "akili" sana yaani! Sema tu akili zingine zinaamuaga kuchungulia upande wa pili kukoje na zingine zinaamua kubakia hivyo hivyo ndani ya "fence". Ukitaka ujue akili yako iko katika kundi lipi basi upate matatizo ndo kipimo cha kujua unawazawazaje! Kama wewe una comfortable life toka utotoni yaani ukikohoa tu dakika sifuri mko Agakhan kuchek afya hebu sasa jaribu kujipa matatizo angalau madogo madogo.. kama kwenda sehemu bila nauli ya kurudia uone wewe unawazaje kichwani. Utaweza kurudi? Utapata option ngapi za kusolve ishu ya nauli ya daladala kwa mfano. Wengine watasema huo ni uchizi. Hahaaaa. Basi sawa. Sasa bana hawa jamaa wamesoma kiasi kama wewe labda, umewazidi usikute. Hawa jamaa walikuwa waajiriwa kama wewe. Waliajiriwa na kampuni moja maarufu kweli kweli siyo tu huko kwao bali dunia nzima. Yahoo! Kuna mtu anayesoma hapa hajui Yahoo! ? Huyo mrefu kabla ya Yahoo alifanya kazi pia Ernst & Young! So.. Walipiga kazi hapo Yahoo! kwa takribani miaka 10! Mwenye Yahoo alikuwa bilionea wao walikuwa wafanyakazi wa bilionea. Kumbe hawakujua kuwa wao nao walikuwa ni mabilionea tena zaidi ya bilionea aliyekuwa kawaajiri. Siku walipojitambua wakaacha kazi Yahoo! Unajua kuacha kazi Yahoo inahitaji uvute pumzi kwenye mapafu mara tatu tatu. Au nakosea. Nadhani kuacha kazi "Juakali Enterprises" ni rahisi kuliko kuacha kazi Yahoo. Imagine kama hapo ulipo tu sasa hivi kuacha kazi haijawahi kukujia akilini je ungekuwa Yahoo? Kufumba na kufumbua hao wakaibuka na kitu cha WATSAPP mwaka 2009. Tena ilianza kama free app then ndo wakaweka tozo kidogo ili kucontrol ukuaji wa kutisha wa WatsApp!! Boooy! Hivi Unajua ndo maana wengine Mungu huwa sometimes anachafua hali ya hewa kazini kwako ili utoke ukawe tajiri huko nje. Wewe kesho yake unaanza maombi ya kufunga na kuhamishwa bosi. Wanasema Mungu si "Asumani". Wiki haifiki bosi kahamishwa. Unapeleka ushuhuda kanisani bila kujua kule mawinguni Mungu anakuangaliaaaaa.. Halafu anakuacha kama ulivyo. Unabaki na utajiri mkubwa kichwani mwako umeufungia kwenye Yahoo yako. Iangalie Yahoo yako vizuri. Usijekuta kuna WasApp yako miaka miwili tu mbele yako. Hawa jamaa wakaanzisha WatsApp yao ikagrow then mwaka jana tu FACEBOOK ikaamua kuwanunua kwa USD 19 BILLION. Si una calculator. Ni trilioni ngapi za bongo? Wangekuwa bado wako Yahoo je. Itazame upya Yahoo yako usikute inakufungia utajiri mkubwa tu. Sasa hivi ni board members wa Facebook. Na shares juu. Yaani hivi unavyosoma hii post hapa fb wao wanaingiza hela hivo. Cha ajabu walipoacha kazi Yahoo wakiwa likizo bado wanawaza wafanye nini hasa, waliapply kazi Facebook wakapigwa chini wote. Huyo Acton akaona isiwe tabu Facebook 'kitu gani' akaapply TWITTER nako akakosa! Dah. Unajua sometime ukiwa karibu "kutoka" kimaisha ndo vishawishi vya kurudi maisha yako ya zamani (mfano kuajiriwa) huwa vinashika kasi kweli kweli.. Wakati mwingine Mungu atakukosesha kazi nzuri qualifications unazo na experience unayo lakini unakosa kazi. Mungu anajua.. usilalamike tu ooh niliapply sehemu mbili nikakosa Mungu anataka utumie akili yako banaa.. Sasa Mfano wangepata kazi Facebook ingekuwaje? Wangekuwa na hisa za Facebook leo kweli? By mwezi wa nne mwaka jana (2014) WatsApp ilikuwa na Active Users milioni 500 kwa mwezi na kila siku kulikuwa na picha milioni 700 na video milioni 100 watu wanazoshare watsapp kila siku mpaka mwaka jana mwezi wa nne. Imagine mwezi wa nne mwaka huu itakuwaje? Watumiaji wa WatsApp kwa siku ilikuwa watu 833,000! (India ikiwa ndo inaongoza kwa kutumia WatsApp duniani). Mtu yuko Marekani hela zinatoka India na kila kona ya dunia. Wewe uko Magomeni hela hata ya Ubungo tu hupati. Mpaka uende hapo Yahoo ulipoajiriwa. Buni basi hata kitu tu cha ziada. Yahoo siyo mbaya wewe tu unaichukuliaje. Kwamba umefika au unapita? So my friend. Narudia tena, ingalie upya Yahoo yako. Miaka 10 bado upo hapo "Yahoo" umeufungia utajiri humo kwa mwajiri wako. Unazidi kuogopa kutoka. Tafakari vizuri. You are probably 5 times richer than your employer's worth. And 10 times richer in the next 10 years. But not if you will still be on that desk. Hakuna tajiri aliyeajiriwa. Ila kuna mabilionea lukuki bado wako "Yahoo"!

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...