17 January, 2015

KICHEKESHO CHA SIKU

Jamaa kanunua mashine kaipeleka nyumbani. Kazi ya mashine ni kila ukisema uongo inagundua ni uongo na inakukandamiza makofi hapo hapo. Wakati wa msosi wa usiku jamaa akaileta mashine imekaa kama roboti akaiweka karibu na meza. Akaanza: Mwanangu, leo wakati wa shule ulikuwa wapi? Mtoto akajibu: nilikuwa shule baba (Twaaaaaap, mashine ikamlamba vibao). Samahani baba ila kwa kweli nilienda kuangalia sinema kwa kina Mudi. Dingi: Sinema gani? Dogo: Aki na Ukwa. (Twaaaaaaaap, mashine ikamlamba makofi), samahani baba, kiukweli ilikuwa ni sinema ya zile picha mbaya za wakubwa. Dingi: toto pumbavu sana, enzi zangu mimi hata sikutamani kuangalia picha za kijinga kama hizo. (Twaaaaaaaaap, mashine ikamzaba dingi makofi). Mama akaingilia huku anacheka: Hahahaha, ndo mtoto wako huyo (Twaaaaaaaaaaaaaap, mashine ikamkandamiza mama makofi)

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...