09 March, 2015

UKATILI HUU, MPAKA LINI???



Tarehe 8 mwezi wa tatu, (jana) tuliadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka duniani kote. Nchini Tanzania siku ya wanawake duniani; kitaifa iliadhimishwa mkoani Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi mmoja, mgeni rasmi akiwa ni Mama Salma Kikwete, mke wa Rais wa Tanzania.

Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Taasisi za kidini, asasi zisizo za kiserikali na serilali kwa ujumla kuhamasisha haki sawa, pia kukemea ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto lakini hali bado ni tete kwani ukatili bado unaendelea, takwimu zinaonyesha wanawake wananyanyaswa kijinsia kwa namna mbalimbali ikiwemo kupigwa, kuchomwa moto, kunyang'anywa mali zilizoachwa marehemu mumewe, kubakwa n.k

Licha ya kwamba mwanamke ni sehemu ya maendeleo, kwani wanawake wengi wanachangia uchumi wa familia kwa kusaidiana na wenzi wao, achilia mbali ni pambo la nyumba na chachu ya maendeleo kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa kwa ujumla.. Wanawake wengi wamekua wakiteswa, kupigwa, kunyanyaswa, kudhalilishwa, kudharauliwa na kunyang'anywa haki yao hasa pale ikitokea wenza wao au waume zao wamefariki.
Pamoja na sheria kuwepo lakini hatua dhidi ya wanaume wanaofanya ukatili hawaadhibiwi ipasavyo ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hizi, ni wajibu wa serikali pia kutoa elimu kwa wanaume ili kuondoa kabisa tatizo hili la unyanyasaji na mauaji kwa wanawake.

Sababu kubwa ya ukatili unaofanywa kwa wanawake ni kwasababu za wivu wa kimapenzi. Ni wajibu wa kila mwana jamii kukemea ukatili dhidi ya wanawake, kwani pasipo mwanamke hatutaweza kupata familia bora. Serikali itoe adhabu kali kwa wale wote watakaothibitika wamehusika na ukatili kwa mwanamke.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...