16 April, 2015

HATARI!!!!! HATARI!!!!

Katika kukua kwangu nimejifunza matumizi ya rasilimali na kuset priorities (vipaumbele). Kama nina laki moja mfukoni, halafu nikawa na matumizi yanayohitaji zaidi ya hiyo hela nitaangalia lile la muhimu ndio nianze nalo. Yani kama umepanga kununua radio halafu mama yako akaugua, ukaacha kumpeleka mama yako hospitali ili pesa ukanunulie "sub woofer", wewe ni goigoi.!

One of the cardinal principles of Economics is Opportunity Cost. Do the fast thing first, and those which can wait let them wait. Ni mwendawazimu pekee anayeweza kununua Jeans mpya ya laki moja wakati hajalipa kodi ya nyumba. Ukiwa na akili timamu utafanya yale ya muhimu kwanza kwa rasilimali kidogo uliyonayo kabla ya kufikiria kufanya anasa.

Nasema haya kwa sababu kuna kituko cha mwaka kimetokea leo. Kituko cha aibu kufanywa na mtu mkubwa kama huyo aliyefanya. Lakini kwa kuwa alishazoea kufanya vituko vingi sikustajaabu kusikia na leo kafanya tena kituko.

Kituko chenyewe ni hiki. Leo "mkuu wa kaya" kateua wabunge wawili kwa mujibu wa Mamlaka aliyopewa kikatiba. Katika tangazo la Ikulu lililotolewa na Ndg.Premi Kibanga (Afisa Habari msaidizi) inasema "mkuu wa kaya" kateua wabunge hao ili kutimiza idadi ya wabunge 10 wanaotakiwa kikatiba.

Kwa lugha nyingine ni kuwa hakuna sababu yoyote ya msingi ya uteuzi wao zaidi ya kutimiza matakwa ya kikatiba ya kufikisha wabunge 10. Yani hakuna impact yoyote hao wabunge wanayoweza kuleta bungeni kwa kipindi hiki kilichobaki, wala hakuna kazi yoyote maalumu iliyochochea uteuzi wao, itz just that "mkuu wa kaya" amejisikia kumalizia nafasi zake 10 alizopewa.

Swali nililojiuliza ni "hivi ni lazima wafike 10?" Hivi asingewateua kuna mahali popote angeshtakiwa kwa kushindwa kutumia haki yake kikatiba to the maximum? (Hapa naomba ufafanuzi wa kisheria kwa wale waliosoma Constitutional Law).

Kama sivyo, uteuzi huu una mantiki gani? Bora akina Muhongo na Saada Mkuya au Makame Mbarawa ambao waliteuliwa Ubunge wa ghafla ili wapewe kazi maalumu ya Uwaziri na Unaibu Waziri. Sasa hawa walioteuliwa leo ni kwa mantiki gani?? Tena ukizingatia kuwa imebaki miezi mitano tu bunge kuvunjwa.

Hebu tujaribu kufanya hesabu ndogo za kugawanya na kuzidisha za darasa la tano. Ni hivi, wabunge wawili walioteuliwa watalipwa mishahara ya miezi mitano bure maana hatutegemei jipya watakalolifanya huko bungeni. Mshahara kwa mbunge mmoja ni Mil.11 mara miezi mitano watakayofanya kazi ni jumla ya Sh.Mil 55 kwa kila mmoja. Kwa wote wawili ni Mil.110.

Wabunge hawa walioteuliwa leo watalipwa kiinua mgongo kwa viwango vya wabunge wa kawaida Sh.Mil.90 kila mmoja ifikapo tar.31 mwezi July mwaka huu. Kwa wote wawili ni Mil.180.

Taarifa ya Ikulu inasema uteuzi wao unaanza tarehe 20, hivyo basi kuanzia tar.21 wataanza kulipwa posho za vikao vya bunge kwa siku 10 zilizobakia kwenye bunge hili linaloendelea. Posho ya siku moja ni Sh.330,000/= kwa siku kumi ni Mil.3 na laki 3.

Kwenye bunge la bajeti Watalipwa posho ya 330,000/= kwa siku. Bunge hilo litatumia jumla ya siku 60. Hivyo mbunge mmoja atalipwa Mil.19 na laki 8, kwa muda wote wa bunge la bajeti. Kwa wote wawili watalipwa mil.39 na laki 6.

Wabunge hawa "watakopeshwa" magari ya kifahari ya kutembelea. Yani kama walikua wakitumia usafiri wa umma, kuanzia tar.20 March wameambiwa stop. Watapanda Mashangingi yanayokadiriwa kugharimu Mil.120 kwa moja, kwa wote wawili ni Mil.240.

Kwa ujumla makadirio ya gharama zote za wabunge hawa wawili kwa miezi mitano tu watakayofanya kazi watatumia jumla ya Shilingi Milioni 573 na laki 2.

Pesa hizi zinatosha kulipia mikopo ya elimu ya juu kwa semister moja kwa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza Chuo kikuu cha St.Augustine, au Chuo Kikuu Dodoma kwa wanafunzi wanaosoma Social Science.

Pia pesa hizi zingeweza kujenga maabara za kisasa katika shule 12 Tanzania. Zingeweza kulipa mishahara ya waalimu (daraja la pili) 1,432 wa shule mbalimbali za sekondari nchini. Pia fedha hizi zingeweza kutolewa kama mkopo kwa vijana wanaohitimu vyuo vya Elimu ya juu nchini na kukosa ajira. Jumla ya vijana 573 wangenufaika kwa mkopo wa Mil.1 kila mmoja.

Lakini cha ajabu pesa zote hizi zitatumiwa na wabunge wawili tu tena kwa kipindi cha miezi mitano tu, with no expectation of return. Hatutegemei wabunge hawa watafanya lolote jipya huko bungeni litakalogharimu hizo Mil.573 watakazotumia.

Kwa lugha rahisi ni kuwa hatutegemei output ya wabunge hawa izidi input. Hakuna mbunge yeyote atakayeweza kutoa hoja zitakazo-value hizo Mil.573 watakazotumia, hata wakisaidiwa na huyo aliyewateua.

Sasa nimejiuliza, hivi katika mazingira haya ambayo hatuna rasilimali za kutosha kulinganisha na mahitaji tuliyonayo, je kulikua na ulazima wowote wa kuteua wabunge hao?

Tunahitaji pesa za kujenga maabara, kujenga shule, kulipia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mikopo, kulipa mishahara, kununua madawa etc. Lakini tumeacha vyote hivyo tumetoa kipaumbele kwa wabunge tena wa kuteuliwa.

Yani mkuu wa kaya ameona heri wagonjwa wafe kwa kukosa dawa, wadogo zetu wateseke vyuoni kwa kukosa mikopo just for the expense of two appointed Mp's

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...