Jeshi
la Nigeria limesema limewaokoa watoto wa kike mia mbili na tisini na
tatu kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa,
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema watoto hao
waliokolewa si kati ya wale waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la
kiislamu katika eneo la Chibok.
Jeshi limeiambia BBC kwamba
wanawake na watoto hao wa kike walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo
silaha pia zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana
hao baada ya kuziharibu kambi hizo."ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."
No comments:
Post a Comment