Staa mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu amemaliza utaa wa picha zake zilizozagaa mtandaoni akiwa amavalia shera kwa kuweka wazi kuwa ni kweli ameolewa.
Leo akiongea na kituo kimoja cha radio, Wema ameeleza kuwa yeye tayari ni mke wa mtu, na kwamba yeye na mwenza wake huyo wameshafunga ndoa ya bomani kwani mume wake ni mkatoliki na mme wake huyo amekubaliana na hali yake ya kutoweza kushika ujauzito. Wema aliongeza kuwa mwisho wa mwezi wa tano watafanya party rasmi kwani harusi yao hiyo ya siri ilihusisha watu wachache sana wasiozidi wa tano .
Hongera sana Wema.
No comments:
Post a Comment