28 April, 2015

WATU 7 WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA DARAJA LINALOJENGWA!


Watu saba waliokuwa ndani ya teksi siku ya Jumapili wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na daraja ambalo bado lilikuwa halijakamilika kujengwa katika jiji la Kano huko kaskazini magharibi Nigeria.
Malam Ibrahim, shahidi wa ajali hiyo, sehemu ya daraja iliangukia gari hilo ilipokuwa likipita chini yake.
Msemaji wa polisi Magaji Musa Majia aliyesema kuwa polisi walitumwa eneo la ajali hiyo iliyotokewa saa kumi na moja jioni. Majia alisema kuwa sehemu ya gari ilinaswa chini ya daraja hilo lililoanguka na kwamba waathirika walikuwa wameshafariki wakati wafanyakazi wa uokozi walipowasili eneo hilo.
Shahidi mwingine, Ahmed Kaka alisema kuwa iliwachukua wafanyakazi wa uokozi takriban saa mbili u nusu kuwatoa maiti.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...