Wafanyakazi wa tanzania wanaumizwa sana katika kodi kuliko wafanyakazi wa nchi zote za afrika mashariki.
Wastan wa kodi ya mfanyakazi Tanzania ni 18%, Uganda11%,
Kenya 6.8%, Burundi 10.3 %na Rwanda 5.6%. ( global tax comparison report
2014-WB)
Wastani wa kodi ya mfanyakazi
duniani kwa mujibu wa ripoti hiyo ni 16.2%. Kwa takwimu hizi sio tu
kwamba wastani wa kodi ya mfanyakazi Tanzania ni kubwa kuliko nchi
yoyote Afrika Mashariki bali ni zaidi ya wastani wa kodi ya mfanyakazi
duniani.
Ikumbukwe chama tawala Tanzanja asili yake ni harakati za
wafanyakazi na wakulima wadogo na ndio tafsiri ya alama ya jembe na
nyundo kwenye bendera ya CCM. Hivyo ni aibu chama kilichoasisiwa na
wafanyakazi leo kinaongoza kunyonya wafanyakazi kwa kodi kubwa kuliko
nchi yoyote afrika mashariki.
Nashauri wafanyakazi waombe CCM iondoe nembo ya nyundo
kwenye bendera yake kwani ni kejeli kwa wafanyakazi. CCM kwasasa ipo kwa
maslahi ya wafanyabiashara wakubwa wasio waaminifu. Hao ndio wanafaidi
uchumi kwa misamaha ya kodi na ukwepaji mkubwa wa kodi.
Ni maoni yangu kwamba kodi ya mshahara inapaswa kushuka kwa 50%. Itoke 18%mpaka9% wastani kwa kuanzia.
Kwa mujibu wa taarifa za TRA mwaka jana, tukishusha kodi hiyo kutoka wastani wa 18-9% tutapoteza mapato kiasi cha 704billion.
Ni maoni yangu kwamba mapato hayo yanaweza kufidiwa kwa
kutekeleza sheria ya kodi ya majengo ambayo mpaka sasa utekelezaji wake
ni 3% na tunakusanya 25billioni. Hii maana yake tukiteleleza kwa 100%
tutakusanya zaidi ya 800billion.
No comments:
Post a Comment