12 May, 2015

LULU NA VAN VICKER KUNANI??!

Lulu Amganda Van Vicker!
Staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anadaiwa kumganda mwigizaji kutoka nchini Ghana, Van Vicker!
Habari zimethibitisha kuwa Lulu amekuwa na mawasiliano ya karibu na Van Vicker tangu walipokutana Septemba, 2013 kwenye Jengo la Akade, Posta jijini Dar ambapo jamaa huyo alitua nchini kurekodi filamu na mastaa wa Bongo.
“Kwa taarifa yenu Lulu sasa hivi mambo yake na Van Vicker ni bambam na wanawasiliana usiku na mchana, nadhani kuna kitu kikubwa kinakuja. Yaani Lulu amemganda jamaa japokuwa sijajua kamili kama wana project gani.
“Kama mtakumbuka kipindi kile Van Vicker alikuja Bongo kucheza filamu ya Hashim Kambi (mwigizaji wa Bongo) ndiyo walifahamiana.
“Inawezekana anataka kufanya naye kazi kama Wema (Sepetu) ambaye hivi karibuni alikwenda Ghana na picha zikasambaa wakifanya yao,”
Lulu alipoulizwa juu ya ishu hiyo alikiri kuwa ni mtu wake wa karibu na kwamba ni kweli amekuwa akiwasiliana naye.“Van Vicker ni mtu wangu, nimekuwa nikiwasiliana naye, kusalimiana na kuulizana maendeleo ya kazi zetu za sanaa,” alisema Lulu.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...