Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul
Makonda akizungumza na wakazi wa Mbezi na Kawe Ukwamani ambao nyumba zao
zilibomoka kutokana na mmomonyoko wa ardhi uliosababishwa na shughuli
za kibinadamu kama vile uchimbaji wa mchanga katika mto huo hali
iliyosababisha kingo za mto huo kupanuka hadi kwenye makazi ya watu.
Makonda aliwatembelea wakazi hao Dar es Salaam jana.
DC Makonda akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wakati alipo watembelea waathiriwa hao.
Wananchi wakiwa katika maeneo hayo yaliyoathiriwa na mmomonyoko huo.
Baadhi ya nyumba zilizobomoka kutokana na mmomonyoko huo.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda amepiga marufuku uchimbaji mchanga katika mto Mbezi na Kawe
Ukwamani kutokana na uharibifu wa mazingira ambao umesababisha nyumba
zilizo kando ya mto huo kubomoka kutokana na mmomonyoko wa ardhi.
Makonda alipiga marufuku wakati
akizungumza na wananchi walioathiriwa na mmomonyoko huo alipofika kuwapa
pole na kuona jinsi ya kuwasaidia Dar es Salaam jana.
"Wakati tunaangalia namna ya kuwasaidi
naomba kuanzisha leo shughuli za uchimbaji wa mchanga katika mto Mbezi
ukome na mtu atakaye bainika anaendelea kuchimba mchanga atachukuliwa
hatua za kisheria" alisema DC Makonda.
Makonda alisema wataalamu wa Manispaa
hiyo watafika katika eneo hilo ili kuona nini kifanyike kupunguza tatizo
hilo kwa siku za mbele kama walivyofanya maeneo ya Tegeta yaliyokumbwa
na mafuriko ambapo kutajengwa karavati kubwa ili maji yaweze kupita.
No comments:
Post a Comment