Msanii
Steven Mengele 'Steve Nyerere' akiwasili katika viwanja vya CCM
Bwawani, kuongea na wananchi wa eneo hilo, kwa ajili ya kutangaza nia ya
kugombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni, ikiwa pamoja na kuhamasisha
wananchi wajitokeze kujiandikisha. Msanii wa filamu Tanzania Steven
Mengele 'Steve Nyerere' na mkewe wakisalimia na wananchi waliojitokeza
katika mkutano wake wa kutangaza kuwania jimbo la Kinondoni.
Steve Nyerere akipongezwa kwa uamuzi wake wa kutangaza nia
MSANII
wa filamu nchini Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kulia) ametangaza nia
ya kugombea ubunge wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es salaam, huku
akiwataka Watanzania wenzake kujitokeza kuandikisha katika daftari la
wapiga kura, ili wasikose kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza
katika mkutano maalum wa kutangaza nia na kuhamasisha watu
kujiandikisha, alisema kujiandikisha ni haki ya kila Mtanzania hivyo kwa
vijana na wazee hakuna sababu ya kukaa na kuacha muda unapioga bila ya
kuutumia. Nyerere alisema ni haki kwa kila Mtanzania kwenda
kujiandikisha hivyo hakuna sababu ya kuacha kipindi hicho kinapita bila
ya wao kukitumia.
"Mama
zangu, Baba zangu, Vijana wenzangu, jitokezeni kujiandikisha ni haki
yenu ya msingi, hasa katika uchaguzi mkuu ujao"alisema Steve Nyerere.
Pia
Nyerere alisema atahakikisha anatatua changamoto za wananchi wa jimbo la
Kinondoni pindi atakapopata ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo.
Hayo
aliyasema mwishoni mwa juma wakati akitangaza nia ya kuwania ubunge wa
Kinondoni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Msanii
huyo alisema wilaya hiyo ina changamoto nyingi ambazo zinapaswa
kutatuliwa ili wananchi waweze kuishi maisha ambayo hayana kero.
Alisema huu ni wakati wa mabadiliko na mabadiliko yataletwa na yeye kwa kuwa anazijua changamoto nyingi ambazo zinawakabili wananchi hao.
Alisema huu ni wakati wa mabadiliko na mabadiliko yataletwa na yeye kwa kuwa anazijua changamoto nyingi ambazo zinawakabili wananchi hao.
"Mimi
Steve Nyerere nimeamua kwa dhati kujitoa na kutangaza nia ya kuwania
ubunge ili nisaidiane na wananchi wa Kinondoni kwa ajili ya kuijenga
Kinondoni mpya," alisema Steve.
Alisema Kinondoni inapaswa kuwa ya mfano kwa kuwa na mitaa iliyopangwa katika mpangilio maalumu na mitaro iliyosafishwa vyema.
Alisema licha ya hilo, Kinondoni inapaswa kuboreshwa miundombinu ili kuzuia mafuriko ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kuharibu sifa ya jimbo hilo linaloubeba mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema licha ya hilo, Kinondoni inapaswa kuboreshwa miundombinu ili kuzuia mafuriko ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kuharibu sifa ya jimbo hilo linaloubeba mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment