Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza mara
baada ya kupokea Fomu zilizorudishwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni baada ya kukamilisha
mchakato wa kutafuta wadhamini katika Mikoa 10 ya Tanzania na kutimiza
masharti yote ya Uchaguzi, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume
hiyo, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akimkabidhi,
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, nyaraka mbalimbali
zitakazotumika wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, kwenye Ofisi za Tume
hiyo, Jijini Dar es salaam leo Agosti 21, 2015. Kushoto ni Mgombea Mweza
wake, Dkt. Juma Haji Duni.CHANZO OTHMANI MICHUZI
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kutangazwa rasmi na Tume ya Uchaguzi kuwania nafasi hiyo, leo
Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam. Pembeni
yake ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mgombea
Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni pamoja na viongozi wengine
waliowasindikiza, wakitoka kwenye ofisi za Tume ya Uchaguzi baada ya
kurudisha fomu leo Agosti 21, 2015.
No comments:
Post a Comment