Mchungaji Ambakile Mwasapile wa Loliondo – Arusha Tanzania anazidi kushangaza watu baada ya kutibu magonjwa sugu yakiwemo Ukimwi, Kisukari, Kansa na mengine mengi ambayo madaktari wameshindwa kuyatibu.
Hali hii imesababisha wachungaji maarufu hapa Dar es Salaam kupata wasiwasi wa kutoaminiwa na waumini wao hasa kwa kile kinachodaiwa wagonjwa wanamiminika kunywa maji ambayo kwa imani unapona kabisa!!
Pamoja na hayo, hali imekua tata kwa hofu kwamba watu wengi wataendelea kufia njiani kwasababu ya umbali na kukosa huduma wawapo njiani kuelekea huko; hii ni kutokana na pori kubwa kuelekea Loliondo.
Mpaka sasa imeripotiwa watu sita wamefariki. Hali ni mbaya kwani hata malazi, chakula vimekua tabu. Achilia mbali usafiri wa kwenda Loliondo sasa imekua dili!! Nauli ya kwenda na kurudi inabidi usiwe na chini ya laki 3!!
Tunaomba serikali iingilie kati ili watu wengi wakapate huduma hii adimu kwa gharama ya shilingi 500 tu!!
Miundo mbinu kuboreshwa kwani barabara ni mbovu, network pia imekua shida. Ikiwa ni pamoja na vyombo ili kukidhi mahitaji ya wahitaji wanaokwenda kupata dawa hiyo.
Ni vema pia wizara ya afya iache mara moja zoezi la kumsimamisha Mchungaji Ambakile kwa madai ya kufanya uchunguzi wa dawahiyo. Kama madaktari wameshindwa, basi muacheni Mtumishi wa Mungu aokoe maisha ya walio wengi
No comments:
Post a Comment