18 March, 2011

Tunaishi kama kuku, tunafanana nao


NATUMAINI wasomaji wa makala haya watajiuliza, watakapokuwa wakiisoma, ni kwa nini nimeamua kutumia tabia za kuku nikiziainisha na za binadamu?
Lakini jibu ni rahisi na nilitoe mapema; kuku ni ndege tumfugaye majumbani, hivyo ni rahisi kueleweka kwa haya machache nitakayoandika.
Pili, ni ule uzoefu nilionao katika ufugaji kuku; ninawafahamu vizuri viumbe hawa kama ninavyowafahamu binadamu.
Uzoefu wangu umeonyesha kuwa staili ya maisha ya kuku inafanana, kwa kiwango kikubwa, na staili ya maisha yetu Watanzania.
Kwa kawaida kuku ana tabia ya kutoridhika; mfano ukimpa pumba ale kamwe haachi kuchakura. Hii inadhihirisha kutorithika na kile anachokiona kwani hufikiri kuwa chini kuna kizuri zaidi.
Sasa, swali la msingi la kuwafananisha binadamu na kuku ni hili: watumishi wasioridhika na mishahara yao , wanaotumia nyadhifa zao kupora rasilimali za nchi yetu, mafisadi na waporaji kura nyakati za chaguzi mbalimbali, hawafanani na kuku?
Kwa wanaowafahamu kuku, kama ninavyowafahamu mimi, wana tabia ya kupiga kelele wanapoona hatari mbele yao bila kukimbia toka eneo hilo . Kwa mfano, akitokea mwewe ama kicheche kumkabili kuku na vifaranga vyake, utasikia kuku anapiga kelele lakini haondoki mahali alipo, baadaye hunyamaza na ndipo hushambuliwa.
La kutafakari hapa kama binadamu anafanana na kuku katika hili ni kwamba ni mara ngapi tumepiga kelele kuhusu vitendo vya rushwa pasipo kuchukua hatua, malalamiko juu ya wizi wa kura, viongozi wasiofaa, ahadi hewa na hata ufisadi? 
 
 
Kuku ana tabia ya kuahidi aonapo kuna mlo, kwa mfano ulishapo mitetea utasikia wakitetea kwa kushinda, kama ilivyo tabia ya kuku kuwa ateteapo basi anakuwa amekaribia kutaga, kwa kufanya hivyo kuku humuaminisha mfugaji kuwa baada ya kula atataga. Lakini inaweza kuwa kinyume, baada ya kula anaweza kukaa hata zaidi ya wiki mbili akitetea bila kutaga.
Hali hii naifananisha na kauli za wanasiasa wetu wanapokuwa majukwaani wakijinadi kuomba kura na kuahidi mambo mengi mazuri huku wakiwaamisha wapigakura wao kuwa baada tu ya kushuka kutoka jukwaani au baada tu ya kuchaguliwa, watatekeleza ahadi zao. Jambo ambalo ni kinyume.
Kuku wana tabia ya kuwapiga na kuwafukuza wahitaji pasipo kuwaelekeza wapi waende; kwa mfano, ni vigumu kuku kukumbatia vifaranga vya kuku mwingine, badala yake hukumbatia vifaranga vyake pekee na kuwafukuza wa kuku mwenzake.
Tabia hii haina tofauti na jinsi tunavyobaguana kidini, kisiasa, kimadhehebu na hata kikabila na kiukoo. Sasa tunayaendekeza haya kwa faida ya nani? Ni nini hatima yake?
Tena, kuku huwa na tabia ya kuficha alichokula, na hili huthibitika mara amalizapo kula. Hakika kuku alapo kamwe hawezi kusahau kujifuta mdomo. Na hata akijifuta pasipo kutakata kuku wenzie huweza kuyachukua mabaki yaliyosalia. 
 
 
                                        

Je, ni mara ngapi tunasikia watu wanajinufaisha peke yao hata kwa kuandika majina ya ndugu zao kama wamiliki wa mali ? Na hata wakati mwingine kutotaka kuhusishwa na mali zinazowahusu wao wenyewe. Kwa mfano, utawezaje kukataa kuwa wewe si mshirika katika ubadhirifu unaofanywa na mume au mke, ikiwa wewe ni mmoja wa wanafamilia?
Mwisho wa siku ukimwona kuku anaonekana sehemu za chini ya shingo akiwa amevimba baada ya kujikusanyia chakula, na hii haina tofauti na jinsi yalivyo matumbo ya wale wanaokalia viti vya kuzunguka, ofisi za viyoyozi na kutembelea 
 
 
                                     

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...