huo alisema:-
"Tumeshindwa
kuwazuia WANADAMU wasiende kwenye nyumba za IBADA"
Tumeshindwa
kuwazuia wasisome VITABU vyao vitakatifu na kufahamu ukweli"
Tumeshindwa
hata kuwazuia wasiwe na mapenzi ya kweli kwa MITUME yao " "Mara
wapatapo muungano wa kweli kwenye MAHUBIRI ya DINI zao, mamlaka yetu yatakuwa
yamefika mwisho."
Kwa hiyo kuanzia sasa waacheni waende kwenye nyumba zao za IBADA, waacheni
waendelee na karamu zao za upendo,
LAKINI waibieni
muda, ili wasipate nafasi ya kudumisha IBADA za kweli kweli kwa MOLA WAO
MUUMBA...."
"Hiki ndicho ninachotaka mfanye." Alisema Lucifer:
"wataabisheni
WANADAMU WOOTE wasipate kamwe kushikamana na DINI zao na wasifungamane katika
KUMCHA MUNGU"
"Tutafanyaje jambo hilo?" mashetani yalimwuuliza
kwa jazba.
LUCIFER aliwajibu:"Tutafanyaje jambo hilo?" mashetani yalimwuuliza
kwa jazba.
"hakikisheni wanakuwa 'BUSY' (BUSY= Being Under Satan's York )katika mambo yasiyokuwa na umuhimu katika maisha yao na muwaanzishie mipango mingi sana isiyohesabika ili kujaza akili na ufahamu wao. "Washughulisheni na kutumia, na kutumia, na kutumia; na kukopa, nakukopa, na kukopa."
“Washawishini
wake zao waende kufanya kazi kwa siku na kushinda huko kwa masaa mengi sana kwa
siku na Waume zao wafanye kazi kwa siku sita hadi saba kwa wiki, na masaa 10
hadi 12 kwa siku, ili wasiweze kupata nafasi ya kutulia na kutafakari chochote
kulingana na mfumo huo wa maisha." "Wazuieni wasiwe na nafasi ya
kukaa na watoto wao"
"Wachocheeni zaidi akili na fahamu zao ili kuhakikisha kwamba hawaiskii ile sauti ndogo tulivu ya Mungu wao."
"Washawishini
walize radio au kaseti au muziki kwenye simu, popote wanapoendesha gari au
wanapotembea kwa miguu.
Waache
TV,VCR, CD na KOMPYUTER zikiwa zimewashwa kama kawaida majumbani mwao na
mhakikishe kwamba kila duka na mgahawa kote duniani linapiga muziki usiokuwa wa
KIDINI tena mfululizo bila kukoma." "Hii itasonga akili na
fahamu zao na kuvunja ule muungano kwa MOLA
WAO."
"Jazeni magazeti na vijarida mbalimbali vya upuuzi kwenye meza zao za kahawa na chai Duniani kote."
"Shindilieni
habari na matukio mbalimbali ndani yafahamu zao kwa muda wa masaa 24."
"Ingilieni
kwenye muda wao wa kuendesha barabarani kwa kuwaonyesha mabango na matangazo.'
"Kwenye masanduku ya posta na barua pepe jazeni vipeperushi
na majarida na kila aina ya
matangazo ya habari za vitu na hudumu yanayowapa matumaini ya uongo."
"Wekeni
wanawake warembo sana mitaani, club, kwenye mitandao ya kijamii, maofisini na kwenye Televisheni na
majarida ili kwamba Wanaume walioko kwenye ndoa wadanganyike na kuamini kwamba
urembo wa nje ndio muhimu, na wasiridhike na wake zao."
"Wafanyeni
wake zao wachoke sana wasiweze kuonyesha upendo kwa waume zao nyakati za
usiku.Wapeni maumivu ya kichwa ili wasiwape waume zao upendo wanaouhitaji
sana,ili waanze kutazama kwingine. Wafanyeni Wanawake wawadharau Waume zao na
kuwapuuza.
"Hiyo
itaparaganyisha familia zao haraka sana !
"Wapeni WANADAMU
Waalimu wa uongo ili wawapotoshe wasifundishe maneno ya MUNGU ya kweli kwa
watoto wao na waumini wao." 
"Hakikisheni
wanakuwa 'BUSY' na kusongwa na mambo kiasi kwamba hawapati muda wa kutafakari
wema wa Mungu. Badala yake wapeni kutalii
kwenye maeneo ya ajabu, matukio ya michezo, matamasha, kumbi za sinema na
video."Wafanye wawe 'BUSY,' 'BUSY,' 'BUSY,! Yaani wasongwe na kusongwa na
kusongwa na kazi kwelikweli!"

"Jazeni visababishi vingi vya mambo katika maisha yao ili wasiwe na nafasi ya kutafuta msaada na nguvu za MUNGU. Muda si mrefu watakuwa wakitegemea akili zao wenyewe, badala ya maelekezo ya MUNGU, huku wakihatarisha afya zao na za familia zao kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe."
"Itafanya
kazi" "Itafanya kazi!
"Huu
ni mkakati kweli kweli. Mashetani yaliondoka kwenye mkutano yakiwa na hamu
kubwa sana ya kutekeleza majuku hayo waliyopewa na kuanza kuwafanya WANADAMU
wawe wa kukimbia na mambo huku na huko. Watakuwa na muda
mdogo
sana kwa ajili ya Mungu wao na familia zao. Wakakosa muda wa kuwaeleza wengine
kuhusu MAMBO YA IBADA na kubadili maisha ya wanadamu.
SWALI:- JE SHETANI AMEFANIKIWA
KATIKA MIPANGO YAKE HIYO? WEWE NDIYE HAKIMU !!!!!!!! TAFAKARI KUANZIA SASA KUTATHMINI UMETOKA WAPI, UKO WAPI NA UNAKWENDA WAPI. PIA UNA MKAKATI GANI WA KUPAMBANA NA MIKAKATI YA SHETANI.
SWALI:- JE SHETANI AMEFANIKIWA
KATIKA MIPANGO YAKE HIYO? WEWE NDIYE HAKIMU !!!!!!!! TAFAKARI KUANZIA SASA KUTATHMINI UMETOKA WAPI, UKO WAPI NA UNAKWENDA WAPI. PIA UNA MKAKATI GANI WA KUPAMBANA NA MIKAKATI YA SHETANI.
No comments:
Post a Comment