Katika mambo makuu yanayomfanya mtu kukosa raha katika maisha ni pamoja na
i) Kuugua
ii) Kufiwa
iii) Kukataliwa / Kuachwa
Lakini jambo kubwa ni kuhakikisha unakabiliana na yote hayo na unasonga mbele. Tunaelekea kuumaliza mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2012. Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kukusaidia kuishi mpaka leo, ukiwa na afya njema.
Pengine wewe ni shahidi wa magharika yanayotokea lakini unapona au kunusurika na majanga mbalimbali. Hii si kwasababu wewe ni bora kuliko wengine. Mwaka mmoja ni usiku wa giza! Ni kipindi kirefu ambapo matatizo mbalimbali huweza kujitokeza.
Samehe, sahau ili uanze mwaka mpya , jiwekee malengo yako upya na yale ambayo hukuweza kuyatimiza mwaka 2011 hakikisha mwaka 2012 usipite bila kuyatimiza. Wale uliowakosea hakikisha unawaomba msamaha ili uweze kuanza mwaka ukiwa na baraka za Mungu.
Hakikisha unatimiza malengo yako yote. Usikubali kurudishwa nyuma kwasababu ya kuachwa/ kukataliwa, usiruhusu huzuni itawale maisha yako kwasababu ya kufiwa au maradhi. Nawatakia mafanikio, afya na amani katika kipindi chote cha mwaka 2012.
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba linaanza vikao vyake tena leo mjini Dodoma, huku kukiwa na jitihada kubwa za kujaribu kuweka udh...
No comments:
Post a Comment