23 February, 2012

HAKIMU ALIYEMTIA HATIANI MTU ALIYEPOFULIWA MACHO

Hivi yule Hakimu aliyemtia hatiani mtu aliyepofuliwa macho yake kisha kubambikizwa kesi ya wizi wa kutumia silaha, ANALALA USINGIZI KWELI? Kesi ilipoendelea baadae, mtu huyo aliachiwa huru kwa kuwa hakukuwa na ushadidi wa kumtia hatiani. Nadhani DPP aliliona hilo. Lakini mtu huyo aliyepofuliwa macho yake na Askari Polisi, anapaswa kufidiwa na nani? Serikali iwajibike. LHRC mko wapi? Hivi sasa mtu huyu yu fukara wa kufukarika. Hawezi kufanya kazi yoyote! Tukio hili liliripotiwa na The Guardian.
Askari alijichukulia sheria mkononi. Yeye na wenzake sita walimkamata mtu wa watu, wakamtesa, huku wakiwa wamemfunga mikono na miguu kwa kamba, yeye akamchoma sindano yenye tindikali kwenye macho yake. Hapo ndipo ndugu yetu huyu alipoacha rasmi kuona.  
Sio ndugu yetu lakini tuna wajibu wa KUPIGA KELELE ili haki itendeke, mtu huyu afidiwe. Serikali haiwezi kukwepa lawama hapa. 

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...