Katika mapenzi wivu unahusika kwa
asilimia kubwa lakini ukizidi unaweza kuwa matatizo,, kuna tukio
limetokea huko mkoani Mara wilayani Bunda Mfanyabiashara mmoja
anadaiwa kumgonga kwa gari mkewe na kumjeruhi kwa kile kilichodaiwa
kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoani Mara Robert
Boaz amesema mwanamke huyo anayeitwa Nasra Mohamed mkazi wa mjini
Bunda alipatwa na mkasa huo ambapo siku ya tukio mwanamume huyo
aliyekuwa anaendesha gari yake aina ya Nissan T 400 BBC, alimkuta mke
wake akiwa anatembea katika barabara kuu ya Mwanza , Musoma mjini
Bunda, Imeelezwa kuwa alipomuona mkewe alisimamisha gari lake na kisha
akamuita lakini alipomsogelea aliendesha gari kwa kasi na kumgonga na
kuanza kuuburuza mwili wake umbali wa zaidi ya mita 150.
Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa licha
ya mwanamume huyo kumgonga mkewe hakusimama na kwamba alilitelekeza
gari lake katika kijiji jirani baada ya kupasuka gurudumu moja la
mbele.Aidha imedaiwa kuwa mwanaume huyo amekuwa akimtuhumu mke wake
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine mjini hapo. Polisi
wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamsaka mtuhumiwa
huyo ili sheria ichukue mkondo wake.
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba linaanza vikao vyake tena leo mjini Dodoma, huku kukiwa na jitihada kubwa za kujaribu kuweka udh...

No comments:
Post a Comment