Matofali yaliyotumika kujengea baadhi ya nyumba za wasanii Mkuranga
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib (kulia)akifuatiwa na Mzee Chilo, King Kikii na Viongozi wa Shiwata
Kijiji cha Mwanzega Kimbiji Tarafa ya Mkuranga kinatengeneza historia mpya baada ya Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kupata uhalali wa makazi kwa ajili ya wasanii wa filamu, muziki, wanamichezo na waandishi wa habari Tanzania.
Hii imethibitishwa baada ya maneno ya watu wasio na mapenzi mema na SHIWATA kueneza uzushi kwamba wasanii wametapeliwa fedha zilizochangwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zao!
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SHIWATA, MUNGU WABARIKI WASANII
Kumbe inawezekana? Lakini warekebishe jina kuondoa mkanganyiko kati yao na Tanzania Film Federation (TAFF), yaani, Shirikisho la Filamu Tanzania, kwani kimsingi, kwa mujibu wa Sheria za nchi, Shirikisho husajiliwa kwa minajili ya kusimamia tasnia moja tu ya sanaa, si zaidi ya moja. Kwa hiyo, wasanii wa filamu wanapaswa kuwa wanachama wa vyama vilivyopo chini ya TAFF, wasanii wa muziki wanapaswa kuwa wanachama wa vyama vilivyopo chini ya Shirikisho la Muziki Tanzania/Tanzania Music Federation (TAMF), na halikadhalika, waandishi wa habari wanapaswa kuwa wanachama wa vyama vyao vya msingi, na wanamichezo pia. Kuhusu kuwa wanachama wa mradi huo, SHIWATA iunde kampuni au NGO itakayosimamia mradi, na wadau wote wawe wanachama wa NGO hiyo. Ni maoni yangu tu.
ReplyDeleteYawezekana, ni nia tu inahitajika
ReplyDeletemawazo mazuri sana @Aziz Mongi
ReplyDelete