Hebu tazama jinsi usemi wa duniani viwili viwili, sasa nilikuwa najiuliza Bongo moviz pacha wake nani……hatimaye nina jibu sasa.
KUFANANA KWA STORI. Kama ilivyo filamu za kibongo kufanana stori na huku facebook ni vilevile, huyu ataandika ‘Goodmorning’ mwingine ‘Habari za asubuhi’, ikiwa ijumaa kila mtu Ijumaa Kareem kama wameambizana, mpira ukiwa unachezwa kila mtu anapest matokeo bila kujalisha mwenzake naye amepost hivyohivyo
TATIZO LA LUGHA. Hakuna kitu kigumu kama lugha ya kiingereza kwenye bongo muviz msanii akipewa Scene ya kuongea kiingereza atajiumauma mpaka huruma, na huku facebook yale yale, mtu anaandika ‘Gays’ akimaanisha ‘Guys’ halafu anaona yupo sawa, wengine wanachanganya fans na funs.
KAVA ZURI NDANI HEWA. Makava ya filamu za kibongo yanavutia na kutamanisha kununua kazi zao lakini ndani utumbo mtupu, huku facebook picha za wadada na wakaka zinavutia sana na unaweza kudhani wapo kama walivyo, ila ukikutana naye unaweza kutafuta pa kukimbilia, hasahasa wadada.
MAJINA YA KIZUNGU NDANI KISWAHILI. Filamu za kibongo majina yake huwa ya kiingereza ndani Kiswahili, mfano TRUE LOVE…TWINS, FAKE SMILE…na huku facebook haya majina yanakuja kwenye GROUPS…makundi mengi yanakuwa na majina ya kiingereza mfano, LOVE AND RELATIONS, ukiingia kundini Kiswahili tupu.
MASTAA KUSHOBOKEWA. Filamu za kibongo kwenye kava akiwepo Ray na Kanumba (R.I.P), watu hushobokea bila kuangalia ndani nzuri au mbaya. Vile vile facebook, wale watu maarufu wakiandika status iwe pumba tupu au ujinga utaona shobo za ku-like na ku comment kwa fujo. Mfano flani nadhani mnamjua…..anaweka status hata ya kiajabu ajabu tazama coment anazopata sasa.
VYENYE UJUMBE HAVINUNULIWI. Jifanye kutunga filamu juu ya kifua kikuu ama malaria, hakika utamuuzia bibi na babu yako kijijini tena kwa punguzo la bei, hapa facebook ukitaka upachukie andika status ya kuelimisha hata kama una marafiki 5000 watajidai hawaioni. Utapata like kadhaa na comment mbili tatu. Andika maujinga ujinga vichekesho na mapenzi uone.
VYA UCHI UCHI VINAUZA. Makava ya wasichana wakiwa wamejiuza kimahaba yanauza zaidi, hata humu zile picha za mapaja nje ama mdada kageuza mgongo kitako kinachungulia zina mashabiki wengi mno. Tazama comments zake uone. Vaa baibui sasa au manguo marefu
MAKAVA KUFANANA. Makava mengi ya bongo moviz yanafanana mno. humu facebook makava ni profile pictures…wanaume wengi ukitazama picha zao utakuta wameweka ishara ya vidole viwili kama Chadema kama waliambiana vile halafu wasichana wanasimama na kugeuza kimgongo, kujishika kiuno…..
HAKUNA UHALISIA Waigizaji wengi wa bongo movies hawauvai uhalisia yaani wanaigiza katika kuigiza. Humu facebook, watu kibao wanaigiza kuwa ni watoto wa kishua, wanapiga picha na magari ya baba zao, wanapost wapo Mahoteli makubwa makubwa kumbe wauswazi tu, wakiwa hawajapendeza hawapigi picha wanataka vizuri tu ndo wavitangaze.
WANAFICHA UMRI. Wasanii wa bongo muviz ukitaka mgombane muulize kuhusu umri, kama akikujibu basi atadanganya. Humu facebook vilevile sio wadada wala wakaka wote walewale, kila siku ‘AIEMU EITINI YIAZI’ he!! We hukui?? KILA MMOJA ANAUPENDA UTOTO aisee!! Kwenye profile mtu yupo radhi kuandika tarehe na mwezi lakini mwaka hapana!!! Na kwa wengine wanajidai kuandika wamezaliwa mwaka 1911 mara 1905 kumbe uhalisia ni wa 1976 na 77
WAPENDA SIFA. Msanii wa filamu za kibongo akipata kajina kidogo tu, anachagua watu wa kusalimia , anajifanya bize sana. Humu facebook napo yaleyale, mtu akiona anashobokewa hasahasa na jinsia tofauti anajibu pale anapojisikia unapost kwenye wall hakujibu. Inbox hana muda…online ndo usiseme kama hakuoni vile.
UNDERGROUND HAWAKUBALIKI. Kati ya filamu zinazofanya vibaya sokoni basi ni za wasanii wanaoanza. Hata humu facebook ukiwa ndo unajiunga ndugu hata status iwe nzuri vipi hupati comment. Kama ukiwa mkataji tamaa waweza kujikuta unajiondoa
MAKUNDI. Mara Bongo muviz mara Taff. Na huku facebook hivyo hivyo, kuna makundi zaidi ya mia. Tatizo huku ni kwamba unajiunga kwenye kundi bila kupenda unajikuta ndani!!!
MAPENZI YA UONGO NA KWELI. Kati ya maskendo yanayoongoza kuuza magazeti ni haya ya mapenzi wengi wanaokabiliwa ni wasanii wa filamu, mara leo yuko na huyu kesho yuko na yule. Humu facebook pia mambo ni yale yale, tunawajua ambao hadi sasa wamepita na mabwana zaidi ya wanane na wale wenye wasichana zaidi ya kumi.
UZUNGU SANA. . Ukimfanyia mahojiano msanii wa bongo films wewe unamuhoji kwa Kiswahili, yeye anajibu ‘aah!! You know mimi, may be , its true na mengineyo. Huku facebook mchezo uleule, mswahili kabisa unamuuliza maswali Kiswahili anakujibu kiingereza. Sijui wanahisi wote tumesoma Inglishi kozi???
SKENDO KILA KUKICHA. Wale wa bongo moviz tushazoea kuwasoma kwenye magazeti na maskendo yao. Na huku facebook yapo hayo maskendo. Mara flani msagaji, fulani ni mwanaume lakini ana akaunti yenye jina la kike n.k.
COPY AND PASTE. Filamu za kibongo nyingi ni za kukopi na kubadilisha lugha kutoka nchi nyingine na kuzifanya za kiswahili. Huku facebook watu wanabadili status kutoka katika kiingereza wanatafsiri katika Kiswahili kisha wanajifanya wamezitunga. Ukiwaumbua wanakasirika haoo.
WIZI. Huku wasanii na wadau wakilia juu ya kuibiwa kazi zao na kuzikuta zinauzwa bukubuku mjini, na huku facebook watu wanaiba status tena kwa ujasiri bila kuona aibu, mtu kama flani yeye kazi yake kupitia wall za watu akipata status inayomvutia anaichukua na kuifanya yake. Anapongezwa naye anasema asante!! Kama ya kwake. Siwataji hata wewe unawajua.
BASI KWA UPANDE WANGU facebook na bongo movies ni kitu na pacha wake. kama unazichukia movies za kibongo basi unakosea maana hata wewe ni muigizaji kama haohao unaowachukia, kwa hiyo kwa nia moja tujitahidi kuifikisha tasnia hii mbele zaidi. Sasa swali linakuja humuhumu nani Ray, nani marehemu, nani Uwoya,nani Monalisa, nani Ndauka Rose, Wolper, Jb,………
©George Iron, 2012

No comments:
Post a Comment