09 May, 2012

Sajuki aelekea India kwa matibabu!















Msanii wa Bongo Movie Sajuki amesafirishwa mapema kuelekea India kwa ajili ya matibabu zaidi, msanii huyo ambae anasumbuliwa na maumivu ya tumbo amechangiwa na wasamalia mbali mbali zaidi ya kiasi cha Shilingi  Millioni kumi na sita, Fedha hizo zimetumika kununua tiketi tatu na matibabu yake huko  India.

Hata hivyo michango mingine inazidi kuchangishwa na zitatumwa kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.

Akizungumza na wanahabari, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba alisema mbali na kushukuru kwa misaada iliyopatikana, alibainisha kuwa ugonjwa wa Sajuki umewafumbua macho na kuwafanya kama shirikisho kuwa na mikakati mipya ya kuwasaidia wasanii wanachama wa shirikisho hilo.

Alisema kuwa kwa sasa shirikisho hilo limeingia makubaliano na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhakikisha kuwa wasanii wanajiunga na bima ya afya ambapo watakuwa wakichangia Sh 20,000 kila mwezi.

Alisema kuwa katika kuchangia fedha hizo wasanii pamoja na ndugu zao watatu watakuwa wakitibiwa ambapo aliwasihi wasanii kujitokeza kwa wingi kujiunga na shirikisho hilo.

“Najua wasanii wengi wanaishi maisha ya ujana na kushindwa kuangalia hatima ya uzee wao itakuwaje,” alisema.

Alisema, shirikisho limekubaliana na NSSF katika kuhakikisha kuwa wasanii wanaingia makubaliano ya mikopo ya nyumba. Sajuki anasumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni.
 

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...