30 May, 2012

WEMA SEPETU AVISHWA PETE JANA USIKU NDANI YA CLUB!!



 
Ndani ya ukumbi wa Maisha Club usiku wa kuamkia leo ndipo watu waliposhuhudia Wema akivishwa pete ya uchumba na mwimbaji Mwinyi kutoka Machozi band ambapo kwa tafsiri ya haraka kwa baadhi ya watu walizani hili ni tukio la uhalisia lakini lahasha!. Mwigizaji Wema yuko kwenye harakati zake za kurekodi filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Supastaa akiwa anayaweka maisha yake halisi hadharani hasa yale ya kiuhusiano wake wa kimapenzi na wanaume tofauti akiwemo Diamond ambapo Mwigizaji Minyi kwenye filamu hiyo anacheza nafasi ya Diamond wakati akiwa kwenye mapenzi na Wema, Jana usiku ndani ya Maisha club Mwinyi alitamka maneno haya ambayo aliyatamka Diamond wakati akimvisha Wema pete ndani ya ukumbi huohuo "Huyu ndiye mwananmke niliyetulia naye baada ya kuzunguka huko kote na nahitaji awe wangu wa maisha". Bajeti ya kutengeneza filamu hiyo ni milioni 30 ambapo alianza kuitengeneza March mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...