04 August, 2012

Usaili Epiq BSS wafungwa rasmi!















Pazia la usaili wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, limefungwa rasmi jana katika fukwe za Coco jijini Dar es Salaam, kukamilisha zoezi la miezi miwili la kusaka vipaji katika mikoa nane nchini.
Usaili huo umefungwa huku kukiwa na mafanikio makubwa katika kuvipata, kuvitambua na kuviendeleza vipaji nchini.
Jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen, alisema kuwa usaili umekuwa ni wa mafanikio makubwa na wameweza kuvipata vipaji vingi vya muziki.
Alisema katika usaili wa mwaka huu wameweza kuvipata vipaji vya vijana wenye umri wa chini ya miaka 18 tofauti na miaka iliyopita ambapo walikuwa wanaangalia miaka 18 na kuendelea.
"Tumepata vipaji vingi na hivyo watu wajiandae kuangalia kwenye runinga kuanzia kesho (Jumapili) saa tatu na nusu usiku kupitia ITV," alisema.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...