Chanzo cha Ebola
Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo
kwa lugha ya kitaalamu “Ebola Virus”.Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa
yajulikanayo kwa ujulma kama Homa za Virusi zinaazosababisha kutokwa na Damu
mwilini,(Viral Haemorrhagic Fevers)Chanzo kamili cha virusi vya ugonjwa huu
hakijulikani.Hali inayosababisha mlipuko wake pia haijulikani.Ugonjwa huupia
hauna tiba wala chanjo.Hata dawa za jadi hazijathibitika kutibu ugonjwa huu.
Dalili za Ebola
Dalili za ugonjwa huu ni:-
· Homa kali,inayoambatana
na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kam pua,njia ya haja kubwa na
dogo,mdomoni,masikioni,machoni n.k.
· Kutapika damu
· Kuharisha damu
· Fizi kuvuja damu
· Kutokwa na damu na kuvia
chini ya ngozi.Kwasababu ya kutokwa na damu sehemu za haja kubwa nandogo,choo
namkojo pia vitaonekanakuwa na damu.
Kuenea kwa Ebola.
Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na haraka
kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine kupita njia mbali mbali.
Njia hizi ni:-
· Kuingia mwilini au
kugusana na:-
· Mate
· Damu
· Mkojo
· Machozi
· Kamasi
· Majimaji mengine ya
mwili,ikiwa ni pamoja na jasho.
· Kugusa mtu aliyekufa kwa
ugojnwa wa Ebola
· Kushika/kugusana na
wanyama jamii ya nyani.
· Kuchomwa na sindano au
vifaa ambavyo havikutakaswa
· Uginjwa huu pia
huambukizwa kwa njia ya kujamiiana.
· Kugusa taka ngumu au
maji taka yaliyotokana na kumhudumia mgonjwa Ebola.
Athari za ebola
· Unasambaa kwa haraka
sana
· Unasababisha vifo vingi
kwa muda mfupi
· Jamii huingiwa na hofu
na wasi wasi na kushindwa kufanya shughuli zao za kawaida
· Ni gharama
kuwahudumia/kutibu wagonjwa.
· Mipaka inaweza kufungwa
na watu wakashindwa kusafiri kutoka eneo/nchi moja hadi nyingine.
Kinga ya Ebola
Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika.Ni muhimu hapa Tanzaniatuweke
mikakati thabiti inayotekelezeka ya kukinga na kudhibiti ugonjwa huu mapema.
Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu:-
· Kuepuka kugusa au
kuingiwa na mate,damu,mkojo,jasho,kinyesi,machozi na maji majimengine
yanayotoka mwilini mwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.
· Kwa kuwa ugonjwa huupia
huambukizwa kwa njia ya kujamiiana,epuka kuwa na mpenzizaidi ya mmoja.
· Kutoa taarifa mapema kwa
viongozi wa serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea
mtummwnye dalili za Ebola
· Kuwahi katika vituo vya
huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu.
· Wananchi
wanatahadharishwa kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa kwa Ebola;badala
yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri.
· Kufanya ufatiliaji
madhubuti wa ugonjwa huu.
· Wananchi waepuke mila na
desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa
wa Ebola
· Zingatia usafi wa mwili
na tabia na kiroho.
KUMBUKA
Ugonjwa wa Ebola ni hatari sana.
Unasambaa haraka na unasababisha
Madhara na vifo vingi.
Epukana
nao.
No comments:
Post a Comment