11 December, 2012

KIKWETE ASAMEHE WAFUNGWA 3,814

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete aliwasamehe wafungwa 3,814 siku ya Jumapili (tarehe 9 Disemba) kwa heshima ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania, Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi alitangaza.
"Serikali inatumai kuwa wale waliochiwa huru wanakwenda kujiunga na jamii katika ujenzi wa taifa na kuepuka uhalifu ili wasirejee tena gerezani," Nchimbi alisema katika taarifa.
Kikwete aliwasamehe wafungwa wanaotumikia vifungo vya miaka mitano na tayari walishatumikia robo ya adhabu ya zao, gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti. Wafungwa wanaoteseka na maradhi ya muda mrefu, ikiwa ni pamoja na VVU/UKIMWI, kifua kikuu na saratani pia walisamehewa, wakisubri kuthibitishwa na jopo la taalamu wa afya. Wengine walioachiliwa ni pamoja na wanawake wanaonyonyesha, watu wa zaidi ya umri wa miaka 70, watu wenye ulemavu wa kimwili au kiakili.
Wafungwa wanaotumikia vifungo vya muda mrefu kwa makosa makubwa, ikiwa ni pamoja na biashara ya madawa ya kulevya, wizi wa magari au uharibifu wa miundombinu, au kosa lolote ambalo linachukua kifungo cha maisha, hawakusamehewa.
Kikwete pia aliwatunukia nishani watumishi bora wa umma 40 kwa kazi zao za mfano kwa taifa, ikiwa ni pamoja Nishani 11 za Ushujaa kwa wanajeshi walioiokoa meli iliyokuwa imetekwa na maharamia katika Ziwa Tanganyika.

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...