SHERIA inawataka watu wote
wanaoingia katika jiji la Wildwood, New Jersey, Marekani kuhakikisha suruali
zao hazishuki zaidi ya inchi 3 chini ya kiuno cha mvaaji ambapo atakaekiuka sheria
hiyo kwa mara ya kwanza atawajibika kulipa faini ya dola 25 hadi dola 100.
Imefafanua kuwa atakayekiuka mara ya pili na kuendelea atatoz
wa faini ya mpaka $200.
Adhabu
nyingine inayoweza kutolewa ni pamoja na kufanya kazi za jamii kwa saa 40.
Mmoja wa ma rapper waliokerwa na sheria
hiyo mpya iliyopitishwa na jiji la Wildwood huko New Jersey Marekani ni The
Game.
Akiongea na mtandao wa TMZ Game ameonekana kuchukizwa na sheria hiyo na
kusema kuwa hawawezi kuwapangia watu jinsi ya kuvaa nguo na kuongeza kuwa hizi
sio enzi za utumwa.
“They trying to get people to not sag, please. Can’t tell
people how to wear their f***ing clothes. What time are we in? This ain’t the
f***ing slave days. F*** that.”
Game aliongeza kuwa yeye ataendelea kuvaa mlegezo na watu watano wa
kwanza kukamatwa kwa kosa hilo atawalipia faini yeye na ataenda huko huku akiwa
amevaa kata K, “I am with the sagging movement. First five people to get fines,
I will pay their tickets … I will go there and sag cause I am a sagging
Sagittarius.”
Rapper mwingine kutoka kundi la Bone
Thugs-n-Harmony aitwaye Bizzy Bone aliuliza kama sheria hiyo inawalenga watu
weusi na kusema huo ni ubaguzi na ujinga “Are they talking about black people?
How can they do that? This is racist and ridiculous.”
Rapper mwingine aliyeonekana
kutokubaliana na sheria hiyo ni Mac Miller ambaye hajatofautiana na Game na
Bone kwa kusema huo ni ujinga na kuongeza kuwa yeye ataendelea kuvaa mlegezo
popote aendapo, “I just think that’s ridiculous because no one has time to do
that much community service.
I sag and will sag anywhere I go.”
Sheria hiyo inategemewa kuanza kufanya
kazi mwezi ujao (June) katika jiji la Wildwood, New Jersey nchini Marekani.
Kama wewe ni mzee wa ‘Kata K’ na unampango wa kuwa huko kuanzia mwezi
ujao na kuendelea habari ndio hiyo.
No comments:
Post a Comment