Habari kutoka kwenye blogu ya Habari Mseto inasema:
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amepigwa na kujeruhiwa vibaya, damu zinamtoka puani.
Amepigwa na vijana wa Kisomali, katika eneo la Zaburi kata ya Makuyuni Jimbo la Monduli.
Taarifa
za awali zinasema baada ya Nassari kuondoka na gari jingine, waliokuwa
wanafuatana naye Kiongozi wa CHADEMA aliyetambulika kwa jina la Teddy
Ndossi na dereva wa Nassari walienda kujibanza sehemu.
Dereva
wa Nassari Guardian Palangyo amepigwa mdomoni amevunjwa meno mawili,
na kwa sasa wamempiga Katibu wa CHADEMA wa eneo hilo anayeitwa
Kilongola, wapo Kituo cha Polisi Makuyuni kutafuta msaada zaidi.
No comments:
Post a Comment