*Yajigamba kufanya mashambulio muda wowote
*Watanzania wapewa mafunzo ya ugaidi nje ya nchi
*Polisi nchini wasema vyombo vya ulinzi viko macho
*Mtanzania akamatwa Kenya akihofiwa gaidi
WAKATI wananchi wa Afrika Mashariki
wakijawa na hofu ya mashambulio yanayopangwa kufanywa na vikundi vya
ugaidi vya Al Qaeda na Al Shabab, imebainika kuna Watanzania waliopewa
mafunzo ya ugaidi wanaojiandaa kufanya maovu.
Hayo yamebainika siku chache baada ya
wanamgambo wa kundi la Al Shabab kufanya mashambulio katika Jengo la
Biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya 70 na kuacha
mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa.
Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania,
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliyasema hayo jana
katika mahojiano maalumu na MTANZANIA.
Alikuwa akizungumzia kauli ya hivi
karibuni iliyotolewa na Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu
Muscab aliyetoa tahadhari kwamba kundi lake linapanga mashambulio
mengine Tanzania na Uganda.
Babile alisema taarifa zinaonyesha
vijana wa Tanzania waliojiunga na mafunzo ya ugaidi yanayotolewa na
vikundi vya Al Qaeda na Al Shabab, wamefanya hivyo baada ya kushawishiwa
watapata utajiri wa haraka.
Alisema hali hiyo imevifanya vyombo vya ulinzi na usalama nchini kutoipuuza kauli hiyo ya Sheikh Abdulaziz Abu Muscab.
“Tunajua wapo Watanzania wanapewa dozi
za ugaidi, na sisi siyo kisiwa, watu ni hao hao… tumejipanga kuyakabili
haya na kuushirikisha umma katika ulinzi,” alisema.
Babile alisema kauli ya msemaji wa kundi
la Al Shabab ya kuivamia Tanzania siyo ya kupuuza na kusisitiza kuwa
vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko tayari kukabiliana na lolote
litakalotokea.
“Tumeisikia kauli yake kwenye mitandao
ya jamii, imetufanya kuwa alert (macho) vya kutosha, imetuweka sawa na
imetukumbusha kuwa tunaweza kuvamiwa wakati wowote.
“Hatuja-relax hata kidogo, tumejiweka
sawa kwenye human resources zetu, materials resource na hata frontline
officers wetu wako makini mno.
“Mfano kwenye viwanja vya ndege ambako
ni muhimu, kuna mitambo inayoweza kugundua hati za kusafiria za
washukiwa wa uhalifu wanaotafutwa kimataifa na tutawakamata tu.
“Lakini hata kwenye mipaka yetu yote
hatuko peke yetu, tumepanua wigo wa kupata taarifa za kiintelijensia na
katika kufanya kazi hii tunashirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na
usalama,” alisema.
Baada ya kufanya mashambulio mjini
Nairobi Jumamosi iliyopita, Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu
Muscab, aliripotiwa kwenye mitandao ya jamii akisema shambulio hilo
lilikuwa ni la kulipiza kisasi baada ya majeshi ya Kenya kuvamia kundi
hilo lenye makazi yake mjini Kismayu, Somalia.
Mitandao ya jamii pia ilimnukuu Sheikh
Abu Muscab akijigamba kuwa wakati wowote mashambulio ya kikundi hicho
yataelekezwa Uganda na Tanzania.
Wakati huohuo, Babile amesema Mtanzania mmoja alikamatwa Kenya akishukiwa kuwa ni mmoja magaidi waliovamia jengo la Westgate.
Bila kumtaja jina, alisema mtu huyo ni
mkazi wa Arusha na alikamatwa muda mfupi baada ya kuingia Kenya akitoa
Tanzania, akitumia usafiri wa mabasi ya abiria.
“Walipomkamata wakatuletea taarifa sisi,
tukatafuta kwenye database zetu na information za ndani zikatuonyesha
hakuwa mtu hatari, tukamuachia.
“Kilichowatia hofu na kumshuku mtu huyu
ni muda alioingia Kenya na muda wa tukio lilipotokea… lakini tumeangalia
taarifa zote tukagundua hakuwa na shaka,” alisema Babile.
Chanzo:udakuspecial
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba linaanza vikao vyake tena leo mjini Dodoma, huku kukiwa na jitihada kubwa za kujaribu kuweka udh...

No comments:
Post a Comment