29 September, 2013

HAYA NDIYO ALIYOYAANDIKA ZITTO KABWE KWENYE FACEBOOK BAADA YA GAZETI LA MTANZANIA NA MWANANCHI KUFUNGIWA



Absalom Kibanda Mhariri Mkuu wa gazeti la Mtanzania aliyenusurika kuwawa baada ya kuteswa kwa kung'olewa kucha, meno, jicho na vidole sasa anakuwa hana kazi kwa miezi 3 baada ya gazeti lake kufungiwa na Serikali. Wamemkosa kwa kumtesa sasa wanafuata kwenye kazi yake. Hawataki kumwua Kibanda kwa njaa, wanataka kuwanyima habari Watanzania.
Wanataka tusome Uhuru na HabariLeo tu.
Unafungia gazeti la mwananchi eti kwa kuandika kuhusu mishahara ya Serikali, wapuuzi hawa hawajui mishahara ni kodi za wananchi na wana nchi wana haki ya kujua mishahara ya watumishi wao. Serikali lazima ijutie uamuzi huu wa kibabe na kidikteta. Kama hupendi habari ya gazeti nenda mahakamani. Kufungia gazeti ni tendo la woga. Cowards behave this way

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...