Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ametangaza kuwa ataliamrisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) kuongoza mapambano dhidi ya ujangili wa tembo na faru na ukataji
haramu wa miti kwa shughuli za biashara ambao umefikia kiwango kikubwa
Tanzania.
Aidha, Rais Kikwete amesema kwamba sekta ya utalii katika Tanzania
sasa imeanza kutishiwa kweli kweli na uuaji wa wanyama hao na biashara
haramu ya meno ya tembo na faru na kuwa tishio hilo ni kubwa kwa sababu
sekta ya utalii inachangia kiasi cha asilimia 17 katika Mapato ya Taifa
na inaajiri kiasi cha watu 300,000.
Rais Kikwete ametangaza uamuzi huo makini jioni ya leo, Alhamisi,
Septemba 26, 2013 wakati alipozungumza kwenye Mkutano wa Viongozi wa
Nchi na Serikali kuhusu biashara haramu ya wanyama na bidhaa zake pamoja
na biashara haramu ya bidhaa za miti na mbao.
Rais Kikwete ameuambia Mkutano huo ulioandaliwa na Rais Ali Omar
Bongo Ondimba wa Gabon na Serikali ya Ujerumani kwenye Makao Makao ya
Umoja wa Mataifa kuwa mwaka 1960, Tanzania ilikuwa na tembo kiasi cha
350,000 lakini kutokana na ujangili idadi hiyo ya tembo ilishuka hadi
110,000 ilipofika mwaka 2009. Kuhusu faru, Rais Kikwete amesema kuwa
mwaka 1974 walikuwepo faru 700 katika Tanzania na sasa wako chini ya 100
kwa sababu ya vitendo vya kijangili.
“Katika miaka ya 1980 na 1990 wakati wa kilele cha ujangili katika
mikonga ya wanyama, tulilazimika kutumia jeshi kutuliza hali hiyo.
Tuliona matokea mazuri na tulikuwa na utulivu wa aina fulani. Lakini
katika miaka minne iliyopita, tumeshuhudia kuongezeka kwa vitendo vya
ujangili kwa ari na kasi mpya. Kwa mfano kati ya mwaka 2010 na Julai,
mwaka, 2013, zaidi ya tembo 1,386 waliuawa katika Tanzania.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Tumechukua hatua kali za kupambana na
ujangili ikiwa ni pamoja na sera, sheria na kanuni za kupambana na
ujangili. Aidha, tumetia saini mikataba mbali mbali ya kimataifa ya
kupambana na ujangili huu.” Amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Vile vile, tumechukua hatua za kukamata majangili na hata kukamata
silaha zinazotumika katika ujangili. Kati ya mwaka 2010 hadi katikati ya
mwaka huu, 2013, jumla ya majangili 5,189 wametiwa mbaroni na silaha
kiasi cha 1,952 zimekamatwa. Isitoshe, vipande vya 3,788 vya meno ya
tembo vimekamatwa vikiwa na uzito wa kilo 10,756 zilikamatwa nchini.
Nimeamuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania kukabiliana na hali hiyo na
naamini kuwa tutapata mafanikio makubwa zaidi katika operesheni
inayoandaliwa.”
Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa bado shughuli za kupambana na
ujangili, zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na mahitaji
ya watumishi 4,800 wapya kwa ajili ya kupambana na ujangili hata kama
wameajiriwa wafanyakazi 500 tu mwaka huu.
“Pamoja na kwamba tuna matatizo ya watumishi, bado pia tuna matatizo
ya raslimali fedha. Bajeti ya sasa ya dola za Marekani 6.9 milioni kwa
ajili ya Idara ya Wanyamapori haitoshi kutimiza yote haya. Tunahitaji
dola za Marekani milioni 19.4 kwa ajili ya shughuli hiyo na nyongeza ya
dola milioni 30 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na ujenzi wa nyumba za
wafanyakazi. Tukiachiwa pekee yetu hatuna uwezo. Tunaomba twende pamoja
katika hili.”
Chanzo:Kibonde
Never afraid to try on your own; No matter what, you can keep it real. Trust yourself...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?
Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...
-
Ee Mungu Mwenyezi uliyekubali Mwanao Yesu Kristu ateswe mpaka kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu naomba uwe nami. Ee Msal...
-
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba linaanza vikao vyake tena leo mjini Dodoma, huku kukiwa na jitihada kubwa za kujaribu kuweka udh...

No comments:
Post a Comment