29 December, 2013

USIWASIKILIZE WAKATISHA TAMAA…

Dunia imejaa wakatisha tamaa kuliko watia moyo. Unapoingia shuleni kwa mara ya kwanza utaambiwa masomo ni magumu sana; ukiingia chuo mwaka wa kwanza utaambiwa wahadhiri wanakamata balaa (lakini utashangaa watu
wanahitimu na wanapata A za kutosha); ukipata nafasi ya kazi baada ya masomo unaowakuta watakwambia mazingira ya kazi ni mabaya na magumu sana hapa; ukitaka kuoa utaambiwa eti
siku hizi hakuna wanawake wa kuoa, wote ni Beijing (Mchina); dada ukitaka kuolewa utaambiwa wanaume wa siku hizi sio watu (sasa sijui ni viumbe gani); ukitaka kujenga nyumba watakwambia kujenga si lelemama, unaweza kuishia kwenye msingi tu; hata ukitaka kuanza biashara utakaowakuta watakwambia biashara ni ngumu sana na unahitaji mtaji wa milioni
100 ili ufanye hii biashara (wakati wenyewe walianza na milioni 2, mtaji ukakua taratibu); na mambo mengine kibao..!!!

Inawezekana kuwasikiliza watu wa aina hii ni moja ya sababu zilizokufanya usifanye vizuri mwaka 2013. Tunapoumaliza mwaka 2013 na kuingia mwaka 2014 badilisha mwelekeo, anza kusikiliza habari zenye matumaini na uchukue hatua katika yale uliyoyapanga. Safari ya maili 1,000 huanza kwa hatua 1!
MUNGU awabariki, nawatakia
mafanikio makubwa mwaka 2014.

kwa hisani ya A lucky

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...