Penny ambaye ni mpenzi wa zamani wa Naseeb Abdul "Diamond"
haonekani kujutia kitendo cha kumwagana na msanii huyo na
badala yake sasa ameanza kuzipa uzito hoja za kumpiga chini
Diamond ambaye walidumu naye kimapenzi kwa takribani mwaka
mmoja....
Kwa mujibu wa watu wa karibu na Penny, kitendo cha Diamond
kumpandisha jukwaani Wema Sepetu pale Leaders Club kilipata kila
aina ya laana toka kwa mama mzazi wa Diamond kwani hakuridhia
jambo hilo.....
"Mama alilalamika sana kuhusu Diamond kumpandisha Wema pale
leaders Club, kimsingi ni kwamba hataki kabisa uhusiano kati ya
Diamond na Wema Sepetu"...Kilisema chanzo kimoja ambacho ni
rafiki damu na familia hiyo.
Wakati hayo yakijitokeza ndani ya familia ya Diamond, kwa upande wa
Wema, mama yake pia anadaiwa kulalamikia kitendo cha mwanaye
kutumika kila mara kumbusti Diamond pale umaarufu wake
unaposhuka...!
"Mama Wema naye analalamika mwanaye kutumika kama daraja la
kuwavusha watu kwenye umaarufu halafu wakishafanikiwa wanamgeuka
na kumdhalilisha, kifupi ni kwamba hataki kabisa kusikia
mahusiano ya Wema na Diamond" Kilifunguka chanzo hicho.
Aidha imeelezwa kuwa Diamond amekuwa akimpgia simu Penny mara
kwa mara kumuomba wayamalize lakini Penny amekuwa akimjibu kwa
kifupi kuwa "Nimekuachia Wema Wako"
Taarifa nyingine toka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa Penny
amekuwa akijisifu kuachana na Diamond kwa hoja kuu tatu:
1-: Kuondokana na skendo zisizo na faida kwake.
2-: Kupunguza malalamiko toka kwa familia yake.
3-: Penny aliingia katika mahusiano
na Diamond si kwa ajili ya mapenzi, bali kulipa kisasi kwa
Wema ambaye aliwahi kumchukulia mpenzi wake.
"Hata kutoa mimba ya Diamond amekuwa akisema kwamba kama
angezaa naye watoto wake wangekuwa na sura mbaya na midomo ya
ajabu".Kilimalizia chanzo hicho:
No comments:
Post a Comment