Vifaru na wanajeshi wa Urusi karibu na mpaka wa Ukraine. REUTERS/Gleb Garanich |
Jeshi la Urusi linaendelea na harakati zake kwenye mpaka wake na Ukraine
ili kujibu operesheni ziliyoanzishwa na viongozi wa Kiev dhidi ya
wapiganaji wenye silaha wanaounga mkono serikali ya Urusi mashariki mwa
Ukraine.
Hali iliendelea kutanda jana alhamisi, baada ya shambulio liliyotokea
katika mji wa Slaviansk, ambalo lilisababisha vifo vya watu watano
kutoka upande wa wapiganaji wenye silaha wanaounga mkono serikali ya
Urusi, viongozi wa Ukraine wamethibitisha.
Wanajeshi wa Ukraine wakishika ulinzi katika mji wa Slaviansk, mashariki mwa Ukraine.
REUTERS/Marko Djurica
Hayo ya kijiri waziri mkuu wa Ukraine, Arseni Iatseniouk ameituhumu leo
Urusi kutaka kuanzisha vita vya tatu vya dunia kwa kuunga mkono
wapiganaji wenye silaha mashariki mwa Ukraine, huku akitoa wito kwa
jumuiya ya kimataifa kujiunga pamoja dhidi ya chokochoko hizo za Urusi.
“Majaribio hayo ya jeshi la Urusi kwa kuishambulia Ukraine yatasababisha
mgogoro kusambaa barani Ulaya. Urusi inataka kuanzisha vita vya tatu
vya dunia wakati dunia haijasahau vita vya pili vya dunia”, amesema
waziri huyo mkuu, wakati wa kikao cha baraza la mawaziri.
Arseni Iatseniouk, amesema uungwaji mkono wa Urusi kwa magaidi nchini
Ukraine ni uhalifu wa kimataifa, huku akitoa wito kwa jumuiya ya
kimataifa kujiunga pamoja dhidi ya mashambulizi ya Urusi.
Rais wa Marekani, Barack Obama akiionya Urusi. REUTERS/Larry Downing |
Wakati huohuo rais wa Marekani Barack Obama ameituhumu Urusi kuwa chanzo
cha vurugu nchini Ukraine na kizuizi kwa makubaliano yaliyoafikiwa
mjini Geneva, huku waziri wake wa mashauri ya kigeni John Kerry akiionya
Urusi dhidi ya vikwazo zaidi iwapo itaendelea na msimamo wake wa
kuchochea vurugu na kuendelea kuunga mkono wapiganaji mashariki mwa
Ukraine.
Marekani imeionya nchi ya urusi kuhusiana na kitendo chake cha kuingilia
mambo ya ndani ya nchi ya Ukraine na kwamba jumuiya ya kimataifa
itachukua hatua zinazostahili kukabiliana na urusi.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema kuwa Urusi
inauhadaa ulimwengu kwa kushindwa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa
mjini Geneva nchini Uswisi.
Kerry amesema kuwa Urusi imeshindwa kuondoa majeshi yake katika mpaka na
Ukraine kama ilivyokubaliwa huko Geneva hatua ambayo ni kinyume na
mikataba ya kimataifa.
Ameeleza kuwa dunia inashuhudia kile kinachoendelea na hivyo lazima
Urusi ichukue hatua za kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa Geneva
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
No comments:
Post a Comment