25 April, 2014

HAYA NDIO MAAJABU YA DUBAI

 
 
Dubai ni nchi mojawapo inayopatikana bara la Asia ndani ya umoja wa falme za kiarabu (UAE).
Yapo mambo makubwa  na ya ajabu yanayofanywa na serikali hii kupitia utajiri wake ambayo ama hayajawahi fanywa na serikali ya nchi yoyote ile au hayapo kabisa kokote kule ila Dubai peke yake. Na lengo kuu la serikali ya nchi ya Dubai lipo katika kukuza utalii wa ndani ya nchi lakini vilevile kutengeneza vyanzo vya mapato vikuu zaidi ya kubakia kutegemea biashara ya mafuta.
Maajabu yaliyofanywa na nchi hii na kuvunja rekodi ya dunia ni haya hapa.
1. Burj Khalifa
Hili ni jengo linalipatikana ndani ya nchi ya Dubai, limevunja rekodi ya kuwa kitu chenye urefu zaidi kuliko chochote duniani kilichojengwa na binadamu (the tallest man made structure in the world), jengo hili lina urefu wa mita zinazofikia 830. Jengo hili.lina ghorofa zinazofikia 163 hiyo ni bila kuhesabu parking za magari na floor nyingine ambazo tunaziita maintanance floor. Jengo lililokuwa refu zaidi kabla ya hili lilikua ni lile la world trade centre ambalo lilikua na ghorofa 110, kama mnakumbuka hili jengo halipo tena kwani lililipuliwa na magaidi tarehe 11/09/2001.
Jengo hili ni refu sana kiasi kwa sehemu yake ya juu kabisa kwa kipindi fulani hufunikwa na mawingu. jengo hili liliigharimu serikali kiasi cha dola billioni 1.5. ni jengo lenye mjumuiko wa nyumba za kuishi, hoteli, supermarkets, maduka na ofisi

Full Floor in Burj Khalifa
2. The Palm Islands
Hivi ni visiwa vya kutengenezwa vilivyopo Dubai, visiwa hivi vimejengwa na kutengeneza umbo la mti wa mnazi, kisiwa hiki kimejengwa kwenye kina kirefu cha maji kiliunganishwa na man made peninsula yenye urefu wa kilometa nne. Kisiwa hiki kimejengwa kwa kutumia mawe makubwa yaliyotupiwa majini pamoja na kiasi kikubwa sana cha mchanga, baada ya kukamilisha ujenzi wa kisiwa hicho juu yake zilijengwa nyumba za makazi za kuishi (residential houses) ambazo ziliuzwa kwa watu kwa gharama kubwa sana, na inasemekeana David Bekham ni mmoja wa wamiliki wa moja ya nyumba hizo. Pia ndani ya kisiwa hicho kuna mahoteli makubwa, maghorofa pamoja na sehemu nyingi za starehe, na ni sehem inayowavutia sana watalii, kisiwa hiki kilijengwa kwa muda wa miaka 5, na kiliigharimu serikali kiasi cha takribani dolla  billioni
12. Visiwa hivi vinaonekana vizuri hata ukiwa juu sana angani.

 World Island Dubai Artificial Island in Dubai


 
3.The Dubai Mall
Hii ni muunganiko wa majengo yanayounda sehemu moja ya biashara kama vile mlimani city Dar es salaam, hii ndiyo sehemu ya kibiashara na manunuzi kubwa kuliko zote duniani ( the dubai mall is the world largest shopping mall), Dubai shoping mall ina ukubwa unaolingana na viwanja 50 vya mpira wa miguu, ina maduka na huduma nyingine zinazokadiriwa kupita 1200, ina car parking zaidi ya 14000.


 
Dubai Aquarium
Ina sehemu ya kuhifadhia viumbe wa majini iliyojengwa kwa vioo kwa ajili ya maonyesho kubwa kuliko zote duniani, kwani ujazo wa maji ndani ya contena hilo ni.lita millioni 10 na inahifadhi viumbe wa majini wanaokadiriwa kufikia 33000 ikiwa ni samaki aina mbalimbali na papa. Ndiyo sehemu ya manunuzi na biashara inayotembelewa na watu wengi zaidi kuliko yoyote ile duniani, kwa mfano ndani ya mwaka mmoja baada ya kufunguliwa ilivunja rekodi ya kutembelewa na watu millioni 37, na hutembelewa na wageni 750000 kila wiki.

4. Dubai Police cars
Dubai imevunja rekodi ya kuwa nchi ya kwanza duniani kwa polisi wake kutumia gari za gharama zaidi katika shughuli zao za kipolisi na usalama wa kiujumla, polisi wa dubai wanatumia gari aina ya Lamborgin, Bughatti, Ferrari, Astoni Martini, na nyingine nyingi za kifahari, gharama ya magari hayo kila moja kama inavyofahamika ni kati ya shilingi billioni moja hadi tatu;  inasemekana kwamba baadhi wa wakazi wa Dubai huwalazimisha polisi wawakamate ili tu watu hao waweze kupanda gari hizo.

Vitu vingine ni kama hvi hapa chini...........................................................

 

No comments:

Post a Comment

UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Horace Mann - Binadamu wa kwanza kugundua wazo la elimu Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni ...