Baadhi ya watu wamekuwa wanachukulia kirahisi ulaji wa matunda, lakini unapaswa kujua kwamba matunda ni muhimu kwa afya zetu kwani yanatukinga na magonjwa mbali mbali na pia hutengeneza muonekano mzuri wa ngozi ya miili yetu.
Kunakila sababu za kukubali kuwa matunda ni muhimu sana kwa afya zetu kwa sababu huongeza vitamin kibao; zifuatazo ni sababu zinazokufanya ule matunda kila siku:
AVOCADO:
Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juice, lakini huenda
watu wakawa hawalipendi kwasababu ya kutokuwa na sukari katika ladha
yake. Tunda hili pia huongeza mafuta mwilini,
kwa wale walitumialo mara kwa mara. Unashauriwa kula au kunywa juice ya
avocado wakati wowote endapo kama huna matatizo yoyote yanayohusiana na
kuzidi kwa mafuta mwilini. Pia tunda hili huongeza uzito endapo
utalitumia mara kwa mara.


APPLE:
Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini
tunda hili pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamini
na madini kibao, pia lina kazi kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri
wa ngozi ya mwili wako. Tunda hili husaidia kuboresha mzunguko wa damu
mwilini pamoja na kuhifadhi ngozi isipoteze uhalisia wake. Kunakila sababu za kukubali kuwa matunda ni muhimu sana kwa afya zetu kwa sababu huongeza vitamin kibao; zifuatazo ni sababu zinazokufanya ule matunda kila siku:



NDIZI: Hili pia ni tunda lenye jina kubwa kwa watu wengi wanaojali ulaji wa matunda, kwani nitamu na lenye ladha safi. Tunda hili husaidia kulainisha ngozi ya uso iliyokauka, kwa mfano utakuta kuna baadhi ya mafuta au losheni zimecholwa ndizi. Kula ndizi ili urekebishe ngozi ya uso wako pamoja na kuupa uwezo mzuri wa kumeng'enya chakula.


No comments:
Post a Comment